Michezo ya 24 ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yafunguliwa

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
微信图片_20220204211359.jpg
Hafla ya ufunguzi wa Michezo ya 24 ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing imefanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa taifa wa Beijing. Rais Xi Jinping wa China atatangaza kufunguliwa kwa michezo hiyo.

Wakuu wa mashirika ya kimataifa wakiwemo mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Bw. Thomas Bach na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres, na viongozi wa zaidi ya nchi 30 akiwemo rais Vladmir Putin wa Russia wamehudhuria ufunguzi huo.

Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ni michezo mikubwa ya kwanza inayofanyika kama ilivyopangwa tangu kutokea kwa mlipuko wa janga la COVID-19, na inawashirikisha wanamichezo karibu 3000 kutoka nchi takriban 90. (Picha: Xinhua)
 
Back
Top Bottom