China yarusha chombo kwenda Sayari ya MARS

China yarusha chombo kwenda Sayari ya MARS

CHINA YARUSHA CHOMBO KWENDA MARS

Jamhuri ya watu wa China imefanikiwa kurusha chombo chake aina ya Tianwen_1 kuelekea katika sayari ya Mihiri {Mars} jana saa 6 na dakika 41 mchana kwa saa za nchini humo.

Chombo hiko kimerushwa kwa kutumia roketi yao aina ya Long_March5 kutoka katika kisiwa cha #Hainan na kutumia dakika 36 kufika nje ya dunia {#space} tayari kwa kuanza safari ndefu ya kuelekea katika sayari hiyo.

Tianwen-1 kina uzito wa kilogramu 5000 {Tani 05} huku vikiwa jumla ya vyombo tofauti vitatu ikiwemo Orbiter, Lander na Rover na kinategemewa kufika mwezi February2021.

Taarifa za wanasayansi mbalimbali wa anga wa juu wanasema endapo itafanikiwa, China itakuwa imethubutu kufanya misheni ngumu ya kujitegemea kuelekea katika sayari hiyo kwa kupeleka vyombo vitatu vyenye majukumu tofauti.

'Orbiter' itabaki angani kuzunguka muhimili nje ya sayari hiyo kisha kuachia 'Lander' itakayoenda kutua kwenye ardhi ya sayari hiyo pia nayo itashusha 'Rover' kwa ajili ya kutembea kuanza kufanya tafiti za kisayansi.

Umoja wa falme za kiarabu hivi majuzi {Emirates} ilirusha chombo chake ambacho kitaenda kufanya tafiti zake kwa kuzunguka nje ya sayari hiyo.

#rtView attachment 1515642View attachment 1515643View attachment 1515644View attachment 1515645
Kama namuona Trump alivyokunja sura...
 
Hawa ndio wanaoiharibu ulimwengu hawa. Tutakosa kuwa na kasi ya mabadiriko ya hewa duniani hivyo?. Halafu vyombo vyote hivyo huyu arushe chake na huyu arushe chake ipo siku vitagongana huko juu,mshuko wake sasa kutokea huko juu. Nafikiri itabaki nchi moja tu kupeleka huko chombo,nchi moja inawekeza upande wa kukandamiza upinzani tu
 
Ngoja uone akipitwa vumbi atakalo achiwa adi sasa amesha lijuwa ilo una juwa bora mtu akupite kwa kitu kimoja inakuwa bora ila mchina anataka kumpita kwa kila kitu kwa speed ya rocket !
Kumbe bado "anataka"?
 
Umesema nanukuu. "...ila mchina anataka kumpita kwa kila kitu...". Ndo nikauliza bado anataka nikimaanisha hajaanza.
Aja maliza vyote mkuu ndio ana pambana
Usiku na mchana !
 
Mrejesho jamani tuko mwezi wa march sasa,vipi misheni yao imetimia au wamepotea njia?
Nalog off
 
Leo ni March bila Shaka mission ilibuma. Mkubwa mkubwa tu.
Mkuu chombo kimeshaingia orbit ya Mars kinazunguka na kupeleleza, mwezi May ndo inategemewa Lander itatuwa kwenye ardhi ya Mars na Rover itakuwa released kufanya utafiti pale kwa siku 90 then mzigo unarudi Beijing
 
Mbona mataifa mengine yaliisha fanya hili kitambo, sasa cha ajabu nini hapo?
 
Mkuu chombo kimeshaingia orbit ya Mars kinazunguka na kupeleleza, mwezi May ndo inategemewa Lander itatuwa kwenye ardhi ya Mars na Rover itakuwa released kufanya utafiti pale kwa siku 90 then mzigo unarudi Beijing
Wale wengine wao walisema wao watafanya utafiti huko kwa miaka 2 wana stori sana
 
Mkuu chombo kimeshaingia orbit ya Mars kinazunguka na kupeleleza, mwezi May ndo inategemewa Lander itatuwa kwenye ardhi ya Mars na Rover itakuwa released kufanya utafiti pale kwa siku 90 then mzigo unarudi Beijing
Najua mnamsifia mchina sababu hamumpendi Mmarekani.
Ila tambueni America is America na kuwa Superpower kuna mengi unapaswa uyakamilishe kwanza.

Mchina bado sana kushindindana na Mmarekani, na rudia tena Mchina bado sana
 
Mi natoa update ya nini kinaendelea kwa chombo cha China we unaleta ligi za kishamba! Wapi naongelea kuwapenda China au kuwachukia Marekani?
 
Back
Top Bottom