China yarusha chombo kwenda Sayari ya MARS

China yarusha chombo kwenda Sayari ya MARS

Mr pianoman

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2019
Posts
2,649
Reaction score
6,485
CHINA YARUSHA CHOMBO KWENDA MARS

Jamhuri ya watu wa China imefanikiwa kurusha chombo chake aina ya Tianwen_1 kuelekea katika sayari ya Mihiri {Mars} jana saa 6 na dakika 41 mchana kwa saa za nchini humo.

Chombo hiko kimerushwa kwa kutumia roketi yao aina ya Long_March5 kutoka katika kisiwa cha #Hainan na kutumia dakika 36 kufika nje ya dunia {#space} tayari kwa kuanza safari ndefu ya kuelekea katika sayari hiyo.

Tianwen-1 kina uzito wa kilogramu 5000 {Tani 05} huku vikiwa jumla ya vyombo tofauti vitatu ikiwemo Orbiter, Lander na Rover na kinategemewa kufika mwezi February2021.

Taarifa za wanasayansi mbalimbali wa anga wa juu wanasema endapo itafanikiwa, China itakuwa imethubutu kufanya misheni ngumu ya kujitegemea kuelekea katika sayari hiyo kwa kupeleka vyombo vitatu vyenye majukumu tofauti.

'Orbiter' itabaki angani kuzunguka muhimili nje ya sayari hiyo kisha kuachia 'Lander' itakayoenda kutua kwenye ardhi ya sayari hiyo pia nayo itashusha 'Rover' kwa ajili ya kutembea kuanza kufanya tafiti za kisayansi.

Umoja wa falme za kiarabu hivi majuzi {Emirates} ilirusha chombo chake ambacho kitaenda kufanya tafiti zake kwa kuzunguka nje ya sayari hiyo.


#rt
FB_IMG_1595588390008.jpg
FB_IMG_1595588397277.jpg
FB_IMG_1595588400471.jpg
FB_IMG_1595588404804.jpg
 
...
Tianwen-1 kina uzito wa kilogramu 5000 {Tani 05} huku vikiwa jumla ya vyombo tofauti vitatu ikiwemo #Orbiter, #Lander na #Rover na kinategemewa kufika mwezi #February2021.
...
... Ok. Noted.
 
Wenzake wamesharusha mpaka Pluto tokea 2015 yeye ndo Yuko mars
Alexander Bell aligundua simu lakini leo mwenye 5G ni mchina.
Stevenson aligundua train ila leo mwenye mtandao mkubwa wa train za mwendokasi ni mjapani na mchina sio mwingereza.
So kutangulia kuanza kitu sio kila kitu
 
Alexander Bell aligundua simu lakini leo mwenye 5G ni mchina.
Stevenson aligundua train ila leo mwenye mtandao mkubwa wa train za mwendokasi ni mjapani na mchina sio mwingereza.
So kutangulia kuanza kitu sio kila kitu
Acha uongo Nani alikua ambia mwenye 5 g ni mchina pekee yake acha upotoshaji, Erikson, Nokia, Samsung Wana 5g technology

Kinachombeba Huawei ni subsidy anayopewa na Chinese government ndo maana equipment zake ziko Bei ya chini
 
Back
Top Bottom