China yarusha chombo kwenda Sayari ya MARS

China yarusha chombo kwenda Sayari ya MARS

Hujamwelewa mtoa post
Swala sio kumuelewa anapotosha, mfano kwa population distribution ya u.s electric train hazina faida kwa hiyo hawawez invest kwenye vitu visivyokuwa na faida

China ana population kubwa sana kwa hiyo train ya umeme ni muhimu mji Kama Shanghai municipality Ina watu mill 39+, the same kwa Japan kwenye miji ya tokyo, kwa hiyo huwezi sema wamewapita ulaya ambayo Wana population declined
 
Watuoneshe picha zao wakiwa huko Mars na iwe na kivuli cha jua.
 
CHINA YARUSHA CHOMBO KWENDA MARS

Jamhuri ya watu wa China imefanikiwa kurusha chombo chake aina ya Tianwen_1 kuelekea katika sayari ya Mihiri {Mars} jana saa 6 na dakika 41 mchana kwa saa za nchini humo.

Chombo hiko kimerushwa kwa kutumia roketi yao aina ya Long_March5 kutoka katika kisiwa cha #Hainan na kutumia dakika 36 kufika nje ya dunia {#space} tayari kwa kuanza safari ndefu ya kuelekea katika sayari hiyo.

Tianwen-1 kina uzito wa kilogramu 5000 {Tani 05} huku vikiwa jumla ya vyombo tofauti vitatu ikiwemo Orbiter, Lander na Rover na kinategemewa kufika mwezi February2021.

Taarifa za wanasayansi mbalimbali wa anga wa juu wanasema endapo itafanikiwa, China itakuwa imethubutu kufanya misheni ngumu ya kujitegemea kuelekea katika sayari hiyo kwa kupeleka vyombo vitatu vyenye majukumu tofauti.

'Orbiter' itabaki angani kuzunguka muhimili nje ya sayari hiyo kisha kuachia 'Lander' itakayoenda kutua kwenye ardhi ya sayari hiyo pia nayo itashusha 'Rover' kwa ajili ya kutembea kuanza kufanya tafiti za kisayansi.

Umoja wa falme za kiarabu hivi majuzi {Emirates} ilirusha chombo chake ambacho kitaenda kufanya tafiti zake kwa kuzunguka nje ya sayari hiyo.


#rtView attachment 1515642View attachment 1515643View attachment 1515644View attachment 1515645
Hongereni sana China,ingawa hii inawa weka Wamarekani kwenye taharuki kubwa sana.Nadhani sasa hawalali usingizi,maana hawataki kabisa taifa lingine liwazidi kitechnolojia na kiuchumi. Kwa wivu,ujinga na kasumba mbaya waliyo nayo wanadhani kila scientific achievement taifa lingine linayofanya,basi taifa hilo litakuwa limewaibia technology.Ni mawazo ya ajabu na finyu sana.Kwani wao hizo tekinolojia wanapata wapi,au wanadhani wao ni wanadamu zaidi ya wengine?Ni hivi majuzi tu Marekani imefunga ubalozi wa China Houston kwa sababu hizo hizo.Ni upuuzi mtupu.
 
Mfukua Makaburi Sexer Root Frank Wanjiru Sela Son

Nawaomba mtie neno hawa mabwana bila yashaka nahii tech Wameiibiia US [emoji14]
CC: Sexer Frank Wanjiru

Wakati wale jamaa wakulia lia DT na mwenzie pompeo wakijifanya kuweka vikwazo ... Jamuhuri ya watu wachina wala hawana Wasiwasi ndio kwanza wanazidi kuzidisha homa kwa mahasimu wao katika nyanja ya technology
Naona Mchina anafuata nyayo za India.
Wababe wa anga US na Russia wanafanya mission huko toka miaka ya 1960. Sisi wabongo katuzidi hatuna budi kumpongeza.
 
Acha uongo Nani alikua ambia mwenye 5 g ni mchina pekee yake acha upotoshaji, Erikson, Nokia, Samsung Wana 5g technology

Kinachombeba Huawei ni subsidy anayopewa na Chinese government ndo maana equipment zake ziko Bei ya chini
Hiyo pekee kwenye 5G umeiweka wewe. Lengo kuu la comment liko mwishoni.
 
Kutangulia ni kutangulia, hao wazungu walitangulia, afu wahindi, wachina na akina sie waswahili tunafuata.
Ngoja uone akipitwa vumbi atakalo achiwa adi sasa amesha lijuwa ilo una juwa bora mtu akupite kwa kitu kimoja inakuwa bora ila mchina anataka kumpita kwa kila kitu kwa speed ya rocket !
 
Ngoja uone akipitwa vumbi atakalo achiwa adi sasa amesha lijuwa ilo una juwa bora mtu akupite kwa kitu kimoja inakuwa bora ila mchina anataka kumpita kwa kila kitu kwa speed ya rocket !
Hata sisi ni donor country, tunataka tuwapite wote hao kwa kila kila kitu, na Sasa tumeanza na nchi ya viwanda na uchumi wa Gas.
 
Alexander Bell aligundua simu lakini leo mwenye 5G ni mchina.
Stevenson aligundua train ila leo mwenye mtandao mkubwa wa train za mwendokasi ni mjapani na mchina sio mwingereza.
So kutangulia kuanza kitu sio kila kitu
Kenya (Moi) walitangulia kujua kuiba kura lakini leo tumewapiga bao.
 
Hata sisi ni donor country, tunataka tuwapite wote hao kwa kila kila kitu, na Sasa tumeanza na nchi ya viwanda na uchumi wa Gas.
Na Corona ni mafua ya kawaida😂
 
Back
Top Bottom