China yalegeza sera ya uzazi wa mpango na kuruhusu wanandoa kuwa na watoto watatu

ldleo

Senior Member
Jan 9, 2010
163
250
VCG111332846251.jpeg

Hivi karibuni, China ililegeza zaidi sera yake ya uzazi wa mpango, na kutangaza kuunga mkono wanandoa wanaopenda kupata mtoto wa tatu. China ni nchi inayoongoza duniani kwa idadi kubwa ya watu, lakini pia ni nchi inayoongoza kwa idadi kubwa ya wazee.

Matokeo ya Sensa ya saba ya watu nchini China yaliyotolewa hivi karibuni yanaonyesha kuwa, idadi ya watu nchini humo imefikia bilioni 1.4118, ambapo watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60 imefikia milioni 264, na wale wenye umri wa zaidi ya miaka 65 wakifikia milioni 191, na hivyo kuchukua asilimia 13.5 ya idadi ya jumla ya watu nchini humo.

Ofisa mmoja kutoka Tume ya Afya ya Taifa ya China amesema, utekelezaji wa sera hiyo ya watoto watatu unaweza kuongeza nafasi halisi ya idadi ya watu katika maendeleo ya uchumi na jamii. Sera hiyo pia inaweza kuboresha mfumo wa umri wa watu nchini China na kupunguza idadi ya wazee kutoka kwenye kilele chake.

Mwaka 2011, China ililegeza sera ya mtoto mmoja, na kuruhusu wanandoa ambao walizaliwa kwenye familia za mtoto mmoja kuwa na watoto wawili. Miaka minne baadaye, sera ya kuwa na mtoto mmoja iliyoanza kutekelezwa mwaka 1982 ili kudhibiti ongezeko la idadi ya watu, ilifutwa, na nafasi yake kuchukuliwa na sera ya kuwa na watoto wawili. Ikumbukwe kuwa, sera ya kuwa na mtoto mmoja ilitambulishwa kwa lengo la kuweka uwiano kati ya ongezeko la idadi ya watu na maendeleo ya kiuchumi.

Hata hivyo, licha ya sera ya watoto wawili kupata matokeo mazuri, lakini idadi ya wazee nchini China imeongezeka zaidi katika miaka ya karibuni. Takwimu zinaonyesha kuwa, idadi ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 65 imeongezeka kutoka asilimia 8.9 ya mwaka 2010 hadi asilimia 13.5 mwaka jana. Ongezeko hili la wazee nchini China lina athari kubwa katika maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii nchini humo, kutokana na kupungua kwa idadi ya watu wanaofanya kazi, huku kukiwa na idadi ndogo ya vijana wanaoweza kuziba pengo hilo. Lakini kulegeza sera hiyo pekee haitoshi, na habari kuhusu sera ya watoto watatu zimepokelewa kwa hisia tofauti nchini China.

Tofauti kubwa kati ya sera ya watoto wawili, ambayo ilishindwa kubadili mwelekeo wa kupungua kwa kuzaliwa kwa watoto nchini China kutokana na gharama kubwa ya kulea watoto kwa wanandoa walio mijini, na sera mpya ya watoto watatu ni kwamba, serikali sasa inafuatilia zaidi na kuwasaidia wanandoa kupata watoto zaidi.

Sera hii inatarajiwa kuboresha mfumo wa idadi ya watu nchini China, kutekeleza kivitendo mkakati wa kitaifa wa kukabiliana na ongezeko la wazee, na kudumisha faida za utoaji wa nguvu kazi.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,720
2,000
Tuliwaonya hapo kabla kwamba wajifunze kilichotokea Ujerumani na baadhi ya nchi nyingine ughaibuni lakini sidhani kama hata maandishi yetu walisoma.

Ishu ya uzazi ni jambo la kiasili sana na linaendeshwa na nguvu iliyo juu ya uwezo wa kibinadamu.. Kampeni yoyote ya kutaka ku control uzazi haina matokeo chanya in the long run.

Sasa hivi inapoelekea kuwa super giant inahitaji nguvu kazi ya damu changa lakini kwa bahati mbaya sana kampeni ya kudhibiti uzazi imewafanya vijana wengi wasitamani kuzaa. Kwahiyo uwiano wa wazee na vijana umekuwa na ombwe kubwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom