China yaipatia Tanzania msaada wa TSh. Bilioni 35

China yaipatia Tanzania msaada wa TSh. Bilioni 35

Nunaomba kufahamu hii mikopo Huwa inalipwa vipi.. je huwa tuailipa kupitia bajeti zetu za kifedha au kwa njia gani wakuu?

Sio vibaya kukopa pale unapo kwama.. binafsi nadhani ingekuwa ni vizuri pia kama kuna namna ambavyo sisi huwa tunawasaidia tuwe tunatangaza pia kwenye media kama hivi itapendeza sana.

Au huwa hawafaidiki na sisi??..
Inalipwa kupitia bajeti ya serikali kuu mfano bajeti ya serikali 2020/2021 ni trilion 30 trilion 3 zinaenda direct kulipa deni
 
Sisi ni donor country mpk sasa,makubwa gani hayo unayaongelea tena?
Mathalani, napouza chai ghafi Kenya, korosho ghafi India na Vietnam baadae Kenya akaongeza thamani ya chai akauza UK na Dubai, then Vietnam nae akaongeza thamani ya korosho kwa kubangua tu, then akauza Marekani na Canada;
Maana yake hatujataka kujihangaisha kutumia financial instruments ili kupata know how na technology ya kuongeza thamani agro produce zetu.

Sri Lanka ina ukubwa wa sqm 65,000 less than Moro region yenye sqm 72,000.

Yet foreign earnings zao kwenye pamba na chai far big more than Li-Tanganyika lote hili.

Kuna pahala hatujaamiua kutumia akili zetu vya kutosha na kuachana na story za msaada wambao ni chini ya makusanyo 1% ya makusanyo ya mwezi.

Hii ni aibu ila basi, siku tukifunguka akili na kuzitumia sawasawa bila shaka tutafanya tofauti
 
Huu ni msaada au mkopo? What do they want in return? Wachina hawaaminiki, hawatowi pesa bila kutaka something in return. Kwa nini bado Tanzania baada ya miaka yote hii ya uhuru bado tunaendesha nchi kwa mikopo na misaada tu! Naona ule mseo wa "ina hatari misaada" unazidi kusahaulika kila miaka ikizidi kwenda.
 
Dola milioni 15 zinagawanywa vipande vipande weeee, hata kazi itakayofanyika haitaonekana!

Hela ndogo hiyo wangechagua palipo na uhitaji mkubwa ambao kama ungetekelezwa vyema uweze kulete matokeo chanya.

Hivyo vipande vipande hata havitaleta mabadiliko yoyote; na pengine hata nusu ya pesa hiyo isijulikane imekwenda wapi.
 
Mtonyo huu ni sawa na 2% ya makusanyo wakati wa JK au 0.7% ya makusanyo wakati wa mwendazake.

Kuna issues kama nchi tuwe serious. Hii misaada ya 15bn ni makusanyo tu ya Manispaa ya Kinondoni.

Tunaposaidiwa hela ndogo au kujengewa matunduni huu wa bakuli "saia saidia" kuna pahala akili zinalala.

Nchi hii ina potential ya kufanya makubwa ila imekosekana creative & innovative brain ili makubwa yafanyike na hela zizalishwe.
Mkuu Freddie Matuja, nilipoandika mchango wangu hapo juu nilikuwa sijakusoma, lakini naona tunazungumza lugha moja kati yetu.

Hivi vimisaada vinatupofusha sana, hadi hapo tutakapoanza kujitambua ndipo tutakapoona ni kiasi gani tulivyokuwa vipofu.

Na hawa jamaa wanaojipambanua kuwa marafiki na kupenda sana kutupa vimisaada kama hivi, nadhani moyoni wanatucheka.

Sasa ngoja nikwambie:huyu rafiki yetu China, angekosa kitu gani kwa kutusaidia na soko lake tu la maparachichi yetu. Tutahitaji maparachichi kiasi gani kupata hela hiyo, ambayo ingekwenda moja kwa moja kwa wakulima wetu?

Ukimwambia atufungulie soko, utasikia visingizio chungu nzima, halafu hapa anafurahi sana kuonekana akitupa hivi vipesa!
 
Back
Top Bottom