China wajenga daraja kubwa kuliko yote duniani

China wajenga daraja kubwa kuliko yote duniani

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
63,621
Reaction score
107,637
Wametumia miaka mitatu na nusu tu kujenga na kumaliza kabisa daraja lote, kwa mwendo huu ndio maana Wachina wameridhika na utawala wa uimla wa Wakomunisti maana ni kama wanawatendea raia wao miujiza katika maendeleo.
Screenshot_20251005_171717_X.jpg

20251005_083158.jpg
 
Sipendi sana siasa za ukomunisti kwa namna fulani kuhusu watawala lakini wachina kuna namna wanafanya maendeleo ambayo hata wananchi hawajaomba.

Nafikiri unanielewa naposema wanafanya maendeleo ambayo hata wananchi hawajaomba sisi huku wananchi tutasema tunataka sijui maji,barabara,hospitali,shule sasa serikali ya China kuna vitu inafanya ambavyo hata wananchi wao hawajataka.

Hawa watu wanaweza fanya mradi wa billions of money katika eneo ambalo hata huo mradi hauwezi lipwa na mapato ya watu wa eneo hilo lengo tu shughuli za kiuchumi na kijamii zi rahisike kwa watu wa eneo husika na ndio maana wengine wanasema mradi wao wa HSR ni wa hasara tu lakini wao wanasema hawatazami leo wala kesho pia hawajengi kwa lengo la kutengeneza faida kubwa lengo ni huduma za kiuchumi,kijamii kurahisika kwa watu na hivyo ndivyo uchumi hukua.

Mfano hilo eneo la Guizhou ni moja ya maeneo yaliyo na GDP ndogo sana China na pia yamekaa vibaya kutokana na milima lakini miradi wanayo fanya hawa wakomunisti kwenye hilo eneo ya pesa nyingi na kitu kimoja pekee wana amini wao hilo eneo lita inuliwa kiuchumi kwa huduma za kiuchumi na kijamii kurahisika kwa watu wa Guizhou mfano hilo daraja
 
Binafsi sina shida CCM kuwa madarakani muda mrefu maana wao sio chama cha kwanza wala hakitokuwa chama cha mwisho kuwa madarakani muda mrefu. japan,China,Vietnam,Singapore kuna vyama vimekaa madarakani muda mrefu tu shida yangu na CCM wana kaa madarakani muda mrefu halafu wanafanya nini ukilinganisha na hao wajapan,wachina,wavietnam,wasingapore ?
 
Maajabu ya ujenzi ni kitu ipo ndani ya DNA za wachina toka enzi za mababu zao hawa wa sasa wanaendeleza tu walipoishia wazee wao na ndio maana wachina wengi wanaona kawaida tu japo kwetu hatuoni hivyo
Ndio ndio
 
Binafsi sina shida CCM kuwa madarakani muda mrefu maana wao sio chama cha kwanza wala hakitokuwa chama cha mwisho kuwa madarakani muda mrefu. japan,China,Vietnam,Singapore kuna vyama vimekaa madarakani muda mrefu tu shida yangu na CCM wana kaa madarakani muda mrefu halafu wanafanya nini ukilinganisha na hao wajapan,wachina,wavietnam,wasingapore ?
Huna shida na CCM kukaa na madarakani muda mrefu, bali wamefanya nini huo muda mrefu?....(very logical)

......Kwenye nchi za wenzetu vyama vya siasa vikongwe kama UMNO kule Malaysia, PAP kule Singapore na CCP kule China raia wamekuwa wakivichagua mara kwa mara kwa sababu vimewaletea mapinduzi mengi sana ya kiuchumi,kijamii na kiteknolojia.... hizi nchi tatu nilizotaja hapo milongo mitano nyuma zilikuwa ni omba omba kama sisi, lakini leo hii hakuna hata moja ambayo inaishi kwa kutegemea misaada, na ndio maana hata kwenye uchaguzi vyama hivyo havina haja ya kuiba kura au kutumia mapolisi hili vishinde, maana raia wanavichagua wenyewe sababu vina deliver kile ambacho wanainchi wanakihitaji.

Ukija Afrika hapa mavyama makongwe kama ZANU PF kule Zimbabwe,LWP kule Liberia na CCM hapa kwetu malawi yana miaka kibao madarakani ila hakuna la maana walilofanya kiasi cha kuashawishi wanainchi waendelee kuyaunga mkono, yamebaki kutumia dola tu kubaki mada... imagine chama kimekaa madarakani tangu uhuru yaan zaidi ya milongo sita, lakini eti mpaka leo bado wanatoa ahadi za MAJI na UMEME kweli? mahitaji ambayo yalipaswa kuwa yamesahaulika kabisa, ila wao bado ndio ajenda yao kuu ya kuombea kura kwa wanainchi, sasa hicho ni chama cha siasa au chama cha majizi yanayotumia uongo wa siasa kujilimbikizia mali?

Binafsi mimi sasa hivi ukianiambia nichagua moja kungozwa kwa hiyari na CCM hii ya sasa ya genge la wahuni au niishi kwenye anarchy nitachagua kuwa anarchist.
 
Lishabomoka hilo tayari, cha mchina muachie mchina mwenyewe...

1763057785893.png

  1. China's newly constructed Hongqi bridge collapses after massive landslide | WATCH
Edited By: Isha Bhandari @IshaBha94705282
Published: November 11, 2025 23:40 IST, Updated: November 12, 2025 5:30 IST

New Delhi:
A section of the recently inaugurated Hongqi Bridge in China’s Sichuan province reportedly collapsed into a river after a powerful landslide on Tuesday. Dramatic footage circulating online shows the bridge crumbling as the mountainside beneath it gave way. Authorities confirmed there were no casualties, and an investigation is underway into the cause of the disaster.




Bridge crumbles into river after landslide​

Videos shared on social media captured the terrifying moment when the bridge’s concrete pillars tilted and collapsed, sending a large section plunging into the river below. A huge cloud of dust and debris filled the air as soil and rocks from the hillside engulfed the bridge’s foundation. According to reports, the Hongqi Bridge, part of a national highway connecting central China to Tibet, partially collapsed on Tuesday afternoon.





Bridge closed before collapse​

Authorities said the bridge had been closed to traffic a day earlier, after cracks appeared on nearby slopes and roads and experts detected movement in the adjacent mountain. Despite preventive measures, the terrain deteriorated further, triggering a massive landslide that destroyed part of the 758-metre-long bridge and its approach road.

Preliminary findings indicate that geological instability in the steep mountain area was the likely cause. The region reportedly has a history of landslides. Officials have begun a technical investigation to determine whether any structural or engineering flaws also contributed to the collapse. The Hongqi Bridge, built by the Sichuan Road & Bridge Group, was considered a crucial link between Sichuan and Tibet and had only been recently completed.

The incident comes just months after another infrastructure failure in China a railway bridge collapse in Qinghai province in August, which killed 12 workers and left four others missing, according to Newsweek.

​

China's newly constructed Hongqi bridge collapses after massive landslide | WATCH​

Preliminary findings indicate that geological instability in the steep mountain area was the likely cause. The region reportedly​

 
Lilijengwa kichina china. Nasikia hata maghorofa yao yana dondoka sana, ni kwa vile hawaruhusu taarifa kutoka nchini mwao.

Nilisoma sehemu wanayakoroga kichina china sana.
 
Lilijengwa kichina china. Nasikia hata maghorofa yao yana donfoka sana, ni kwa vile hawaruhusu taarifa kutoka nchini mwao.

Nilisoma sehemu wanayakoroga kichina china sana.
Magorofa yao huwa yanaanguka mazimamazima, sijui wanajengea na maboksi....

1763512909032.webp

1763512925898.webp
 
Wachina hata wao ni feki, kuna mtu alisema huwa hawafi hahaha.
 
Back
Top Bottom