"By Tukuyu' Tazara ndiyo reli bora zaidi kwa usalama na miundombinu. Bado inaendelea kuelezwa kuwa stesheni ya Dar es Salaam ni kubwa zaidi kuliko stesheni zote Afrika. Namaanisha kubwa kijengo. Lakini ni reli yenye huduma mbovu kabisa. Jana nimesikia redioni kuwa safari iliyokuwa ifanyike jana 13.50hrs imeahirishwa hadi leo 13.50hrs. Delay ya masaa 24. Wananchi wanateseka vipi?
Mkuu kuna wakati nilitembelewa na rafiki yangu kutoka nchi ya ng'ambo, wakati tuko garini kutoka kiwanja cha ndege alipo liona jengo la station ya TAZARA akaniuliza eh Bwana eh, hivi hapa Dar-Es-Salaam mna International Airports ngapi! Nikamwambia ni moja tu-kaniuliza kwani jengo hili kumbe ni la kitu gani nikamwabia hilo ni jenga la station ya TRAIN siyo Airport. We fikilia wageni wanasifia mchango mkubwa na azina kubwa tulio achiwa na Wachina, lakini sisi hilo atulioni - tumekazana ku-uproot kila kitu. Tukija kuhusu kuahirishwa kwa safari ya TRAIN jana, siwezi kushangaa nikisikia tatizo lilikuwa na kukosekana (kukosekana kwa fedha za kununulia mafuta on time) ni ajabu na kweli.
"By Tukuyu" Mfanyakazi akifanya jitihada ajiinue kidogo kwa juhudi binafsi, viongozi watamwandama sana. Viongozi wa Tazara hawataki mfanyakazi hata ajiendeleze kitaaluma. Wakisikia unasoma lazima upewe uhamisho kwenda stesheni za mbali huko porini. Shirika limejaa chuki na ubinafsi.
Kwa maisha hayo tija itatoka wapi? Tazara kuna miungu-watu. Watu wanaogopwa kuliko Mungu aliye hai muumba wa mbingu na dunia. Uongozi wa Tazara umejaa roho mbaya kuliko maana yenyewe ya neno mbaya.
Nakuhunga mkono katika hilo, inasikitisha sana na hii limechangia vile vile kudumaza hari/wafanyakazi kuwa frustrated unnecessarily, niliwahi kushudia vijana zaidi ya mmoja wakipewa majibu ya kimkato na ujeuri kutoka kwa Human Resorces Manager as if kwenda kwao kujiendeleza ki-elimu hakuwezi kuinufaisha chochote TAZARA, kumbuka hao wote walikuwa wana taaluma za kiufundi! Si hilo tu mfanyakazi anaweza kuhamishiwa HQ kwa mfano lakini HRM kama ana chuki nawe unaweza kukaa pale bila ya kupata barua yoyote ya uhamisho hata kama Head wa Dpt husika amukumbushe vipi anakaa kimya au kuficha faili lako, mtu huwezi kuamini mambo haya! Walikuwa wanafikia hatua ya kuficha mafaili ya watu chini ya carpet, and he didn't give a damn! lakini Mungu mkubwa naye alikuja kuondolewa pale kwa shinikizo la wafanya kazi, lakini alikuwa amejisahau mno mtu ungefikili labda na yeye ni share holder wa TAZARA-very arrogant.
'By Tukuyu' Tazara walikuwa na rasilimali nyingi. Zote wameuza. Pale Kurasini kulikuwa na Material Base, yadi kubwa ya kuhifaddhia mizigo. Kubwa kuliko hata bandari. Wamemwuzia mhindi wa Tanzania Road Haulage (TRH). Leaders club ilikuwa mali ya Tazara, wameuza. Lile jengo la Tanzania Heart Institute lilikuwa hostel ya Tazara, wameuza. Wameuza mali nyingi mno hado aibu. Tazara inasikitisha.
Mkuu we fikilia walikazania kuhuza mali karibu zote za TAZARA upande wa TANZANIA na siyo Zambia kwa nini? mimi wala si walahumu Wazambia, kumbe wafanye nini kama sisi Watanzania hatujali mali zilizo upande wa kwetu. Mkuu unajua dalali mkubwa aliyesuka deal hizi, kwa kushirikiana na viongozi ambao hawajali mali za TAZARA upande wa TANZANIA wakahuza mali hizi kwa bei ya chee! Je mtu huyu alikuwa ni nani?- MTANZANIA aliye ajiliwa TAZARA, kwa sasa hivi amekwisha ondoka lakini mtu mwenyewe alikuwa na eti "taluma ya SHERIA!"
Sasa kama Serikali zetu ziko serious na jambo hili la kuhuza mali ya SHIRIKA ki holela na kwa bei ya sawa na kutupwa, basi wa-revisit procedures zote zilizo tumika ku-despose off mali za shirika-watafute an indepedent mthamini (Govt Agency preferrably) a go-through mali zote zilizo kwisha huzwa aone kama fedha zilizo lipwa na watu/makampuni kwa TAZARA zinalingana na thamani halisi za mali hizo. Nakuhakikishia watakuta mambo ya hajabu sana, alafu mtu na akili zako timamu unawezaje kuhuza Kurasini material BASE? Mimi sijuhi Wachina watatuona sisi ni binadamu wa aina GANI! Kuhuza Kurasini material base nijanga la kitaifa lakini naona Serikali zetu hilo hawalioni au sijuhi hawajuhi hiyo Material Base alijengwa pale na Wachina kwa madhumuni GANI!
Ignorance wakati mwingine inaweza ku-cost an arm and leg; bila BASE hile unafikili uendeshaji wa Shirika utakwenda sawa sawa kweli? Nachelea kusema kwamba uhuzaji wa Kurasini ni hujuma na kosa la jinai, wote walio husika na hujuma hiyo wanapashwa kufikishwa kwa Pilato. Huyo Mhindi anapashwa kuwekwa to-task mpaka aeleze alivyo huziwa Kurasini na ni nani walihusika hili wachukuliwe hatua FASTA. Nchi hii haiwezi kuendelea huku inahujumiwa na watu wasio wahaminifu na ukosefu wa
UZALENDO. Kurasini ni janga la kitaifa lakini sijawahi kusikia mtu yeyote analizumgumzia hilo.
'ByTukuyu' Leo Tazara wanakodi mabehewa toka Railways System of Zambia (RSZ) shirika la Zambia wakati wao wana mabehewa zaidi ya 1400. Wanakodi hadi injini (locomotives) kutoka RSZ wakati injini za Tazara ni U30C zenye horse power 3000 zilizotengenezwa na General Electric ya USA na Krupp ya German. Ni injini zenye nguvu kuliko zozote zinazotumika Afrika. Tazara imelaaniwa.
Mkuu wala hilo husilishangae Wazambia ni wajanja wanataka kunufaisha Taifa lao, kwani mabehewa na locomotives zikikodishwa kutoka shirika la Zambia (RSZ) wanao faidi ni nani - Wazambia of course. Nakwambia hawa jamaa walisha tusoma siku nyingi na kujua hulka zetu sisi Watanzania za kutokua makini sana kwa kuhoji mambo yanayo kwenda ndiyo sivyo. Kwani kazi ya Deputy Managing Director ni nini si kuangalia maslahi ya Tanzania kwanza alafu TAZARA, huyu ni mtu mwenye akili sana lakini sijuhi Wazambia huwa wanamzidi kete kivipi au na yeye anajikuta yuko peke yake nini? Kwa nini swala kama hili alifikishi Serikalini! Kuna wakati fulani mtu na mkewe wakawa among ya
ma-signatory wa cheque za TAZARA-wewe uliwahi kusikia wapi dunia hii ethics za ajabu kama hizo kikazi, hilo linafanyika wakati Deputy Managing Director Mtanzania (ambaye amekwisha retire) yupo lakini alikaa kimya anaona kitu kama hicho ni sawa tu.
Titizo kubwa lingine ni hili la kupoteza muda mwingi kwenye mambo ya
witch hunting kwa ku-instigate trade union kuleta vurugu kwamba Wazambia hawafahi as if wakiondoka ndiyo TAZARA itafanya kazi ki-ufanisi hiyo siyo kweli
(nakubali kuna baadhi ya Wazambia kama ilivyo kwa Watanzania wanafanya mambo ya kulihujumu shirika lakini si wote), nakwambia bila ya attitude za sisi Watanzania kubadilika hakuna kitakacho endelea. Trade unions zinapashwa kuwa makini sana, watu crafty wanaweza kuwatumia bila ya wao kujijuwa kwa ajili ya maslahi yao binafsi na wala si kwa manufaa ya TAZARA, mimi nilisha fanya analysis kuhusu hili kwa muda mrefu sana nikagundua kwamba kunaweza kuwa na tatizo kweli lakini mambo mengi ni kwa ajili ya ku-serve self interests za watu fulani na si kitu kingine; kuweni wangalifu.
'By Tukuyu' Mabehewa ya Tazara yanatia huruma. Tazama mabehewa ya abiria yaliyoletwa 1995 leo ni scrapper na mitambo ya tetanus. Tazara haioni aibu kwa Rovos Train ya South Afica ambayo mabehewa yake ya miaka ya 1947 lakini bado ni mazuri sana.
Mkuu wewe si unajua karakana ya TAZARA ya DSM licha ya ku-repair mabehewa na ma-coach ina huwezo mkubwa wa kuhunda mabehewa kuanzia kwenye super structure, si wana kila kitu pale in terms of machinary a modern carpentary shop and what have you, kitu ambacho wangeagiza nje ni wheel sets tu labda na shock absorbers lakini springs za aina zote wana machine za kuzi-coil na kuzi-heat treat(komaza), kupiga rangi etc, Wachina walikuwa wamefundisha watu ufundi wa hali ya juu sana kwani nani anajali hilo? hapa tunazungumzia wagons zote including Tanks za mafuta, nazo zinaweza kuhudwa pale Karakana machine za kukunja mabati ya saizi zote zipo, hawashindwi chochote pale - kinacho takiwa ni ubunifu na kuona mbali.
'By Tukuyu' Nina mengi sana ya kueleza juu ya Tazara. Nitaeleza wakati mwingine nitakapopata nafasi. Mara nying nafikiria kuandika kitabu kuelezea hili shirika ambalo waasisi wake Mwalimu Nyerere, Kaunda na Mwenyekiti Mao walikuwa na dhamira nzuri sana ya kulianzisha.
Katika hilo tutasaidiana Mkuu, kama tunayo eleza humu yanaweza kumaliza umangameza wa TAZARA na Shirika likafanya kazi ku-ufanisi mbona ntafurahi sana-tusiwachie watu wachache wasiyo
wazalendo kulifanya shirika kama shamba la BIBI. Mungu ibarika Tanzania na Jakaya kwa kuona mbali, maanake bila effort zake Wachina wasingetia mguu TAZARA eti
"KUIFUFUA" - niliwahi kuzungumza na mama mmoja Professor wa Kichina aliye kuwa ameolewa na Managing Director (Mchina) counterpart wa MD wa TAZARA, aliniambia wazi wazi kwamba Chinese Govt haiko interested na kuhiendesha TAZARA kwa hali ilivyo, akasema China haina kipingamizi kama watapatikana watu Private wakuliendesha Shirika -
well and good. Wachina walisha fikia kukatishwa tamaa na undeshaji husiyo ridhisha wa TAZARA.
Kwa hiyo nikisema Jakaya must have played a big role kubadirisha mawazo ya Wachina najuwa ninacho zungumza, nimelisema hili maanake watu wanaweza kuleta mambo ya siasa kwenye mambo serious kwa kudhani nampigia debe Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, huyu mtu anaona mbali sana ingawa watu wengine wanamfikilia vitu vingine tofauti kabisa.