Mheshimiwa Nundu ambaye nina imani naye, kwamba ana nia thabiti ya kujaribu kuleta ufanisi kwenye
reli hii ambayo aina mfano we katika Africa nzima save Egypt na South Africa. Tatizo kubwa la shirika hili ni Uongozi mbovu uliyo jaa majungu wizi na kupigana vita na blantant nepotism, TAZARA is more of scientific entity lakini imegeuzwa na viongozi wake ambao hawana uchungu na reli hii na wengi wao wanawekwa pale kwa shinikizo la marafiki zao HUKO JUU. Wanacho sahau ni kwamba it takes ages to train a railwayman - Wachina hawakuwa wajinga! Huwezi kumleta mtu kutoka barabarani ukafanya make shift on the job training alafu ukategemea kwamba kiumbe huyu atafanya miujiza, how? Mambo ya TAZARA yanashangaza sana; we fikilia Wachina walikuwa na uzoefu wa zaidi ya miaka sabini na ushee katika uendeshaji wa Reli nchini mwao, walipomaliza ujenzi wa reli ya TAZARA waliacha wame-establish ORGANIZATION CHART(ORGANOGRAM) ya jinzi ya ku-run TAZARA kwa ufanisi; Wachina walipo ondoka TOP Management ikaona CHART inawabana sana wakafanya mbinu za kutafuta consultant of "questionable merit" hili waifumulie mbali, nini kilitokea baadae - viongozi waliambiwa kila kiongozi atafute mfanyakazi ambaye ataelewana nanaye kikazi!!! Dunia ya leo mtu unawezaje kutoa a skewed directive kama hizo, matatizo ya TAZARA yalianzia tangu hapo na chati imebadilishwa mara lukuki kutegemea who is in POWER - Mh Waziri Nundu (MB) wambie uongozi wa TAZARA ukupatie ORGNOGRAM iliyo achwa na Wachina, wasikuletee zao za kuhunga hunga - nalisema hila kwa nia safi kwa sababu niko attached na shirika hili morally na wala simsemi mtu vibaya.
Juzi juzi nilimsikia Mheshimiwa Raisi wa JMT Mh.JK akisema wazi wazi kwamba tatizo la TAZARA ni Uongozi si kitu kingine, hiyo ni kweli tupu. Kwa nini Wizara inakubali kulete mtu kutoka nje ya Shirika au mtu ambaye hajawahi kukaa kwenye shirika kwa muda mrefu na wala hana handon experience ya kuendesha reli (ambaye si-railman perse) mkakubali kumkabidhi reli bila ya kufikilia mara mbili! Unategemea nini mtu ambaye hana ujuzi wowote katika uendeshaji wa reli kawekwa tu pale kwa kujuwana na Higher Authority bila ya merit zozote katika uendeshaji wa reli; watu wa aina hiyo at the end of the day wanakuwa obssed kuangalia ni mtu gani ambaye ni tishio kwake hili amuondoe kwa mbinu zozote zile kwa kuwa ajiamini aliwekwa pale kwa upendeleo tu. Tatizo hili limei-cost sana TAZARA, kuna wafanyakazi ambao wanajulikana kwa ubunifu wao mkubwa lakini wamewekewa kibano au wanatupwa tu in the middle of nowhere. We viongozi wambie mambo ya TENDER na kuhuza mali za TAZARA kwa bei chee mpaka viwanja na majengo kidogo wahuze karakana, wamekazania kuhuza mali za shirika upande wa Tanzania lakini upande wa Zambia mali zao ziko intact; shirika limekuwa shamba la bibi no accountability hawana ubunifu wowote KIBIASHARA zaidi ya political rhetoric, kuwalaumu Wazambia kila saa as if wakiondoka wao basi Shirika lita anza ku-tic, Uwongo mtupu. Call Zambians anytime of the day utakuta wote wako highly organised na ndiyo maana wanakuwaga na hoja za kuwapiku waswahili-take a look kwa Watanzania ukihitisha mkutano wa kushtukiza say, utasikia kila mtu anazungumza la kwake completely out of SYNCH, wenzetu wanakaaga kila wiki kupanga mikakati i.e the way forward, waswahili walaa! wako kupigana vita wenyewe kwa wenye na kuharibiana sifa; Wazambia wanacho fanya ni ku-exploit to maximum kutoelewana kwa Watanzania kwa Watanzania, we are not justified kuwalahumu Wazambia-kumbe wafanyeje?
Wapunguze endless production meetings ambazo huwa hazina tija na nyingine hazina minutes, na cha kushangaza Serikali zetu zinaonekana kusuwa suwa katika swala la ku-address ombwe la Uongozi katika Shirika, aibu tupu maika hii 30 plus tangu kuanzishwa kwa TAZARA bado tunakwenda kukinga bakuri kwa Wachina!
Siku nyingine ntazungumzia karakana ya Tazara ambayo ni one of the biggest in Eastern and Southern Africa save Egypt and South Africa, inahuwezo wa kuhunda kuanzia sindano ya kushonea nguo mpaka a BATTLESHIP, nenda kaingalie sasa hivi imukuwa kama mahame, ubunifu wa kuitumia kwa ufanisi hakuna! wanashindwa na vijikarakana vya wasomali vinavyo hunda Fuel/Oil Tanks, matrailer and what have you, mashine za ku-fabricate vitu hivyo ziko idle TAZARA karakana, they have a modern laboratory ya (Metallugy,metrology, Chemical na Insrumentation) a modern forge and foundary Shop - mtu mwenye ubunifu akiwa na hazina kama hiyo atahunda kitu chochote Duniani, inauma sana. Niliwahi kutembelea kiwanda cha kutengeza magari ya FORD kule Liverpool na cha Landrover Solihull Midland - nakwambia eneo la viwanda hivyo aliwezi kuzidi Tazara karakana-all Chinese efforts have gone to waste under our watch- tatizo letu ni nini hasa!