kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
BAADA ya kuuawa kwa Kiongozi wa Kundi la Al Qaeda, Osama Bin Laden na makomandoo wa Marekani wiki iliyopita walisema nchi hiyo sasa inahofiwa kuifanya China kuwa adui wake namba moja na kuuteka uchumi wake. Mtandao wa AlJzeera umewanukuu wachambuzi na wanasiasa wa Nchi ya China wakidai kuwa hali hiyo inaweza kutokea kutokana na Marekani kukataa kupingwa.
Walisema nchi hiyo inataka kufanya juu chini kuinyamazisha hata kuua uchumi wa nchi hiyo bila ya kujali maslahi ya wengine. Mtandao huo ulisema kifo cha Osama Bin Laden kinaelezwa kuwa kithibitisho tosha kuisogeza China kuwa adui mkubwa wa Marekani kutokana na kushamiri kwa kasi katika biashara na uchumi duniani.
Inelezwa kwamba upo uwezekano kwamba upo uwezekano Marekani ikaamua kutumia mabavu kuwanyang'anya uchumi Wachina. Kwa mujibu wa Mtandao wa Al-Jazeera, Wachina hao sasa wanahofia kutekwa uchumi wao kwa mabavu. Taarifa zinasema Marekani huangalia eneo au nchi gani yenye mafanikio zaidi ambapo baada ya kugundua hali hiyo huingia kwa kutumia mabavu na kupora utajiri kwa vigezo vya kubuni.
"Marekani wanakuja na kigezo cha ugaidi ,kumbe wanachokiangalia ni manufaa yao, hivyo Wachina watakuwa ni maadui wakubwa wa Marekani baadaye, kwa sababu ya uchumi wa nchi hiyo," alisema mmoja wa wachambuzi wa Uchumi wa China.
Wachambuzi hao walihoji pia kwamba kwa nini Marekani haikumkamata Osama akiwa hai badala yake waliamua kumuua ambapo walisema hilo lilifanyika kwa kisingizio cha vita dhidi ya ugaidi nje ya mipaka ya Marekani. Hata hivyo habari zinasema kuwa kabla ya kifo Bin Laden, tayari China ,ilionyesha hofu kwamba mikakati ya Marekani ni kuelekeza hisia zao kutoka vita dhidi ya ugaidi kwenda kwa nchi zenye ongezeko kubwa la uchumi.
Mchambuzi Lin Limin, alisema kuwa Marekani imekuwa na nia ya kuchukua jukumu la kuongoza katika vita nchini Libya kwa sababu inajua kuna manufaa ya vita hivyo.
"Hatimaye wakaanza kuwa na wasiwasi kwa nchi nyingi kujitokeza, kama msimamo wa Marekani juu ya Libya siyo tu mkakati wao, ni lazima si kupoteza nguvu za kijeshi na nishati 'kueneza demokrasia'?," alihoji Lin na kuongeza: "Lakini lazima wataanza kuelekeza mawazo yao juu ya nchi zilizojitokeza kwa kupanda kiuchumi, basi sisi ndio maana tunakuwa na wasiwasi. "
China ilijiunga na vita dhidi ya ugaidi wa kimataifa baada ya Osama kuanzisha na kudhamini ugaidi uliotoa tishio la moja kwa moja katika eneo lake lenye waislamu kaskazini-magharibi ya Xinjiang, alinukuliwa Jiang Yu shirika la habari Xinhua baada ya kifo cha Bin Laden.
Nchi hiyo ilisema kuwa ugaidi ni adui wa kawaida kwa jamii ya kimataifa, ambapo nayo imekuwa ni mwathirika. Alisema Beijing ilikuwa na uhusiano wa vita vya kimataifa dhidi ya ugaidi na mapambano yake ya kukomesha hisia katika mkoa wa Kiislamu, wapiganaji kusisitiza wapate msaada kutoka nje.