China isingemchelewesha Lowassa

Namshangaa sana Makufuli kugombea wakati aligawa nyumba za serikali kwa mahawara zake, amelisababishia taifa hasara kubwa kwa kukamata meli ya uvuvi bila ushahidi, kutowalipa makandarasi pesa zao kwa wakati na hivyo kukuwa kwa riba...

Hizo nyumba alihongwa mamako? au ulihongwa wewe kimada. mijitu mingine! ndo maana mnaitwa ma mbumbumbu na malofa kumbe ni kweli
 
Ila jembe si ameshatangaza kiama kwa mafisadi.lazima atanyongwa tu hata kama itachukuwa miaka hamsini.
 
TANZANIA imeingiliwa. Mtuhumiwa wa ufisadi ni miongoni mwa wagombea urais Tanzania. Uzembe huu unawezekana Tanzania tu. Huwezi kugombea nafasi yoyote Marekani ukiwa na kashfa kama zinazomkabili Edward Lowassa, mgombea urais kwa tiketi ya Chadema.

China ndio kabisa haivumilii uzembe wa aina hii unaoendekezwa Tanzania. Enzi zile Chadema kikiwa chama cha upinzani kinachojitanabahisha kwa vita dhidi ya ufisadi kilipata kuwa na mbunge machachari wa Jimbo la Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo.

Ndesemburo ni miongoni mwa wabunge makini walioijadili Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza Mchakato wa Zabuni ya Kuzalisha Umeme wa Dharura Ulioipa Ushindi Richmond LLC ya Houston, Marekani 2006, iliyosababisha, Waziri Mkuu, Lowassa, kujiuzulu.

Ndesamburo aliliambia Bunge, “…nchi za wenzetu kama za China, wahujumu wa namna hii siyo kwamba wanajadiliwa, wananyongwa hadharani.” Kwamba wenye kuthibitika kuwa ni mafisadi wananyongwa China.

China, kwa mfano, ilimhukumu kunyongwa Liu Han, Februari 2015. Hii ni pamoja na kwamba Han alikuwa na shilingi trilioni 10. Fedha hizo za kifisadi hazikuweza kuinusuru nafsi yake na kuzimu. Gazeti la Telegraph la Uingereza la Februari 9, mwaka huu wa 2015 liliripoti kuwa Han alikamatwa 2013 na kunyongwa mara moja baada ya kupatikana na hatia ya ufisadi.

Operesheni Fox Hunt; maana yake ni Operesheni Kamata Mbweha. Kamata Mbweha imefanikisha kukamatwa watuhumiwa wa ufisadi 680 waliokimbilia Marekani, Canada, Australia na kwingineko. Walirudishwa China kujibu mashitaka ya ufisadi. Waliopatikana na hatia tayari wamekwishanyongwa. China haitaki porojo kuhusu ufisadi.

Dk. Harrison Mwakyembe, Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge (kwa wakati huo), aliwasilisha taarifa ya Richmond bungeni Februari 6, 2008. Kamati ilimtuhumu Lowassa, pamoja na mambo mengine, kuvunja sheria kwa kushinikiza Tanesco kupokonywa jukumu la kutafuta kampuni ya kufua umeme.

Waziri wa Nishati na Madini, alimwandikia Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Julai 13, mwaka 2006, kuwa, “Nimezungumza tena na Waziri Mkuu (Lowassa) leo, juu ya bei ya mitambo ya Aggreko. Msimamo (wa Lowassa) ni ule ule niliokueleza awali na ameagiza…achukuliwe Richmond.”

Kamati ya Dk. Mwakyembe ilimpa Lowassa masharti mawili. Kwanza, ajipime kutokana na ushahidi uliopatikana dhidi yake. Pili, au Bunge lithibitishe ushiriki wake kama angegoma.

Februari 7, 2008, Spika, Samuel Sitta, alimpa Lowassa nafasi ya kujitetea. Lowassa alikuwa na saa zaidi ya 18 kujipanga kujibu. Badala ya kujitetea alijiuzulu. Lowassa alifahamu kuwa asingeweza kuwababaisha wabunge makini kama akina Dk. Wilbrod Slaa.

Lowassa anadai kuwa alitaka kuvunja mkataba wa Richmond. Siyo kweli. Magazeti yalianika bayana kashfa hiyo. Lowassa anadai kuwa alitaka kuvunja mkataba wa Richmond akiwaeleza wenzake “kuhusu habari za magazeti.” Alihisi kuelemewa?

Lowassa, na wapambe wake, anajitahidi kujionyesha kuwa yeye ni mtu wa uamuzi mgumu. Anatamani umma uamini kuwa Kikwete ndiye aliyekuwa na mamlaka ya kuvunja mkataba wa Richmond. Alipoona kuwa Kikwete havunji mkataba kwa nini hakujiuzulu? Mtu wa “uamuzi mgumu” asingesubiri Kamati Teule ianike uozo wa kashfa ili kujiuzulu.

Jitihada za Lowassa kujinasua katika kashfa ya Richmond iliyotia taifa hasara ya zaidi ya shilingi milioni 152 kwa siku, kwa miaka miwili, zikagonga mwamba. Anadai alionewa. Wakuonewa Lowassa? Wajumbe wa kamati hiyo wako hai.

Wabunge waliokuwa wakali kama akina Christopher Sendeka, Lucas Selelii, James Lembeli, Anna Malecela mpo? Dk. Slaa na wapinzani wenzake waliokuwa bungeni Februari 6 na 7, 2008 wakinyamaza mawe yataongea.

Na kwa jinsi Chadema hasa mwanasheria wake, Tundu Lissu, inavyohaha kumsafisha Lowassa kwa kashfa hii ya Richmond, siku za mawe kuitetea Tanzania haziko mbali.

Akiwa Mtera, Dodoma, Lowassa aliamua kutohutubia mkutano wa kampeni na badala yake aliwaruhusu wananchi wamuulize maswali. Michael Makanyi alimuuliza Lowassa kuhusu Richmond. Lowassa aligoma kujibu. Ukigoma kujibu swali mahakamani unafungwa.

Na siyo Richmond tu. Uadilifu wa Lowassa unatiliwa shaka na watu wengi, wakubwa kwa wadogo. Septemba 15, 2007 pale Mwembe Yanga, Temeke, Dar es Salaam na kwa ujasiri mkubwa Dk. Slaa alimtaja Lowassa katika orodha aliyodai ni ya mafisadi. Na kwa jinsi Lowassa anavyotamani kuwa Rais, japo kwa saa chache tu, angekimbilia mahakamani kama angekuwa msafi. Hakudiriki!

Fredrick Sumaye, Waziri Mkuu wa zamani, alituhumiwa kuwa ni fisadi. Sumaye alielewa kuwa dawa ya tuhuma ni kusafishwa na Mahakama. Aliwashtaki wote waliomtuhumu ikiwa ni pamoja na magazeti kadhaa. Sumaye aliuthibitishia umma, kupitia Mahakama, kuwa siyo fisadi.

Wahariri wa baadhi ya vyombo vya habari waliokutana na Lowassa Dodoma mwezi Mei nao waliutilia shaka na kuhoji utajiri wake. Lowassa aliwajibu akisema kuwa “ana ng’ombe kati ya 800 na 1,000. Kwetu Umasaini unapokuwa kiongozi unapewa ng’ombe ili usipate taabu kwa ajili ya kuwakarimu wageni wanapokuja.” Siyo kweli. Hupewi ng’ombe Maasai ukiwa kiongozi.

Lowassa alikuwa Waziri wa Ardhi hadi mwaka 1995. Kuna tuhuma lukuki za yeye kujimilikisha ardhi kifisadi. Mwaka 2000 aliteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo. Lowassa anadaiwa kujimilikisha na kuwamilikisha rafiki zake ranchi za taifa zikiwamo Mzeri iliyoko Korogwe, Mkata iliyoko Kilosa pamoja na Manyara iliyoko Monduli.

Lowassa anadiriki kuwakashifu wazalendo wanaopinga wizi wa mali za umma. Alisema, “..kudanganya watu kwamba nikiwa maskini ndiyo nafaa kuwa kiongozi ni ujinga.”

Hakuna anayewachukia matajiri waliopata fedha zao kwa juhudi na njia halali, wanaolipa kodi na hawajawahi kupora ofisi za umma. Bilionea Philemon Ndesamburo, kwa mfano, ni kipenzi cha watu. Hakuna anayeutilia shaka utajiri wake. Anamiliki hadi chopa. Bilionea mwingine anayeheshimika ni Dk. Reginald Mengi. Mengi anamiliki hadi vyombo vya habari.

Haiwezekani kuwaorodhesha hapa matajiri wasafi Tanzania. Ni wengi. Hatuna shida nao. Ieleweke pia kuwa, kwa baadhi ya watu, nikiwamo mimi, Lowassa ni adui mkubwa wa sheria na utawala bora. Mwanzoni mwa kampeni zake alijaribu kuonyesha kucha zake akiahidi kuwaachia wabakaji waliopatikana na hatia

mahakamani. Wabakaji hao walikata rufaa lakini majaji wa Mahakama ya Rufaa wakawakuta na hatia. Lowassa angepata bahati ya kuwa rais angeunajisi muhimili wa Mahakama.

Gazeti la Mwananchi la tarehe 26 Mei 2015 lilimnukuu Lowassa akiuelezea uviziaji wake, “Chini ya uongozi wa Rais (Benjamin) Mkapa tukagundua hawa jamaa (City Water) ni matapeli...tulifanya kikao saa tisa alasiri, tukachukua kibali cha kumkamata yule Mzungu wa City Water na tukamfukuza akaondoka siku hiyo hiyo kwa ndege kurudi kwao, tulifanya saa tisa alasiri ili asiende mahakamani kupata zuio, kwa hiyo tulivizia muda huo ili asije kwenda kupata zuio.” Huo ni uviziaji wa kimafia. Au mzungu aligoma kumpa Lowassa asilimia za mgawo?

Lowassa anadaiwa kuomba kura kanisani, Tabora, kwa kuwataka Walutheri wasali ili Tanzania impate Rais Mlutheri. Hii ni aibu. Ni uroho wa madaraka. Hata hivyo, bila shaka wengine iwe Walutheri ama la, wamemsikia na wamemwelewa. Watakuwa wameona rangi yake halisi na wanaweza wakaifanyia kazi kauli hiyo ya Lowassa, Oktoba 25.

Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema kuwa kazi kubwa ya makabila iliyobaki ni kutambika. Hata hivyo, muhusika akipotosha kabila lake inaleta mushkeli na hasa kama anagombea wadhifa mkubwa zaidi nchini.

Waandishi makini wa wasifu wangeshachapisha vitabu vinavyoweka bayana historia ya viongozi wanaosaka madaraka kwa njia yenye shaka kama huyu Lowassa.

Naamini, wale wanaojitahidi kumsafisha Lowassa dhidi ya tuhuma mbalimbali zinazomkabili watakuwa wakifanya hivyo kwa maslahi yao binafsi na si taifa. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, anawatahadharisha Watanzania dhidi ya genge hilo la wasafishaji akisema; “Hao wanaomtaka Lowassa ni wale wanaojua watanufaika binafsi (Lowassa akiwa Rais).” Mbowe anaonya kuwa Lowassa hafai kuongoza Tanzania.

Chanzo: Raia Mwema

Adith yako inatufundisha nni?????
 
Hvi zile fedha za nyumba za umma zikizouzwa bei chee zilienda wap na zilifanyiwa shughuri gan na zilipatikana tsh ngp?Duuuuuuuh tanzania mafisadi wengi sna .
 
Ivi ukondoa ukada kuna pesa kiasi gani kimepotea na hiyo Baada ya lowassa kuondoka au mnafumba macho kwahyo chama kilichoasisi kiasi kikubwa cha wizi ndo kiendelee kutawara na mtu mmoja aondolewe ivi kuna nini vichwani humo kuhusu vivuko vibovu UPOTEVU as pesa wizara ya ujenzi escrow meremeta hayo hamyaoni ila richmond
 
Badala ya kulaumu Chadema na Lowasa kumpitisha Lowasa/yeye kugomea urais wakati ni fisadi tungelaumu serikali ya CCM kuhalalisha jambo hili.

Kwa nini mnashangaa kugombea urais fisadi kwa ubunge ikawa ni sawa tu? Shutma haimzuii mtu kutofanya shughuli za kujenga taifa, criminal kikatiba hawezi kugombea urais na criminal kisheria ni yule alie pelekwa court na kuthibitika.
 

Chagua unachotaka, hilo liko ndani ya uwezo wako lkn

Raisi wa V wa JMTZ ni Dr.Pombe Magufuli!

Mkuu tatizo unafanya siasa kama imani za kidini!! Kwa mtu mwenye akili anaejilewa hawezi kuzungumza kitoto namna hii, maana maamuzi ya nani aongoze TZ yapo mikononi mwa watz! Kama ni bao la mkono linakupa kiburi, hilo sahau na mtalisikia kwenye redio.
 
Angekuwa kishanyongwa, na watu tushasahau. ila na kwa magufuli watanyoooooka tuuu

Hivi unaelewa ulichokiandika ndugu au nawe ili mradi umeandika jamani wa TZ tujaribu kufikiria hata kidogo hizi tuhuma ina maana Tanzania fisadi ni Lowasa peke yake?
 
UMESOMA TAARIFA YA PPRA.? Suitor USHAHIDI KWA gazeti la chama NI UONGO
 
Ivi ukondoa ukada kuna pesa kiasi gani kimepotea na hiyo Baada ya lowassa kuondoka au mnafumba macho kwahyo chama kilichoasisi kiasi kikubwa cha wizi ndo kiendelee kutawara na mtu mmoja aondolewe ivi kuna nini vichwani humo kuhusu vivuko vibovu UPOTEVU as pesa wizara ya ujenzi escrow meremeta hayo hamyaoni ila richmond

CCM mtaji wao ni ujinga wa watanzania na wajinga wapo wengi kweli ambao hawaoni na wala hawasikii ukiwaambia mambo wanayofanya CCM,Mungu ibariki Tanazania,tusaidie tuone mabadiliko ya kweli tuone na hao wengine watatufikisha wapi naamini katika mabadiliko kwani nchi hii si ya CCM peke yao.
 
Kama ndiyo hivyo CCM iondoke tu maana wamemlea wenyewe mpaka hapo alipo.

Watuambie mabaya ya Watu wao wakiwa CCM siyo wasubirie wamehama.
 
Hizo nyumba alihongwa mamako? au ulihongwa wewe kimada. mijitu mingine! ndo maana mnaitwa ma mbumbumbu na malofa kumbe ni kweli

Ndugu jaribu kufiri. kwa undani hata kidogo, hao ma mbumbumbu ndo wanao kuwekeni madarakani kwani wangekuwa km mimi thubutu ma ccm mngekusikia ikulu toka kipindi cha " hali mpya nguvu mpya maisha bora kwa kila mdanganyika"
 
Kwa nchi za wenzetu angenyongwa mwakyembe alafu sita kwa nini walificha ukweli? na kama kweli lowassa ni fisadi kwa nini asipelekwe mahakamani? kwa maneno yako ccm inalea mafisadi na kwa hiyo tusiichague maana tukiichagua itatuongezea mafisadi bora tuipumzimshe mwaka huu
 
Jamani lowasa aliondoka serikalini miaka mingi.bada ya hapo ziliendelea kashfa nyingi kama vile mafamba ya meli na vivuko,uuzwaji wa nyumba za serkali nk.mbona haya hayasemwi na watu wanaendelea na kampeni za kugombea uongozi wa nchi?
 
Naona Raia Mwema siku hizi wamechoka na wanazidi kupauka mithili ya kaniki iliyowekwa muda mrefu juani. Hii ni habari iliyoandikwa kwa kukurupuka, isiyosheheni tafakuri za kina na ya kibabaishaji! Ukweli ni kwamba hata huko China hukumu za kuwanyonga wahalifu hazitolewi kiholela bila ya watuhumiwa kusikilizwa na watuhumiwa kupewa nafasi za kujitetea! Hayo hutendeka pia kwa watuhumiwa wa makosa makubwa kama ya wale vijana wetu wanaotumiwa na makada wa CCM kusafirisha na kusambaza mihadarati ambao CCM wenyewe wanawaita "Punda".

Laiti Lowassa angekuwa kule zaidi ya robo tatu ya viongozi waandamizi wa CCM wangekwishathibitishiwa hukumu zao wanazostahili - kifo. Hii ni pamoja hata na huu mdoli wao ulioshawishi na kusimamia hujuma kubwa ya kupora na kugawana nyumba za serikali - hali iliyosababisha baadhi ya watumishi waliostahili kuishi katika nyumba za serikali kuishi kwenye nyumba za kupanga mitaani hadi leo!

Lowassa na wenzake waliojitambua na kujitenga na genge la wahalifu hawa wanapigwa vita kwa hofu ya kuumbuliwa. Kwa kifupi watanzania hawadanganyiki tena bali wameungana kwa pamoja kama msemo wa vibakauchumi wa CCM unaosema "Umoja ni ushindi" ili kuwang'oa na kuwawajibisha. Subirini 25 Oktoba mtaona tutawafanyaje.

Hakuna jiwe litakalosalia, tutawapelemba mmoja mmoja kuanzia mliomaliza tembo wetu, twiga, mnaosambaza mihadarati, madalali wa uporaji ardhi na wizi wa madini yetu kupitia mikataba ya aibu kwa taifa hadi mliohonga vimada mali na amali za serikali. Tutawabana UKAWA wachukue hatua za kuzirejesha mali za taifa zilizotekwa nyara na genge hili vikiwemo viwanja vya mpira na majumba yaliyojengwa kwa kodi za baba na babu zetu.

Fanyeni mazoezi ya kuchuchumaa sasa ili mnyolewe. Mapambano ndiyo yameanza na kamwe HATUDANGANYIKI.
 
Back
Top Bottom