Chimbuko la matatizo yote haya ni Freeman Mbowe

Chimbuko la matatizo yote haya ni Freeman Mbowe

Mbowe kafanya makosa na kubwa kuliko yote ni kumkaribisha yule fisadi Lowassa, lakini kudai yeye ndiye chanzo cha wahuni na wauaji kuendelea kuwa madarakani ni DHANA POTOFU ambayo mwenye akili timamu na mfuatiliaji wa karibu wa uhuni na udhalimu unaofanywa dhidi ya viongozi wa upinzani na wanachama wao hawezi KUHITIMISHA hivyo.
Tatizo lako wewe kukariri!! Hivi ikatokea mgeni kaja tanzania ukimwambia kuna mauaji atakuelewa? Nani aliyeuwawa? Udhalimu udhalimu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
penda chama usipende mtu.kwenye kibaki chadema hauko peke yako na mimi nipo.
 
Kuliko Mbowe na Chama chake waingie madarakani ni bora tuongozwe na JPM hata miaka 20.
Mbowe ni Dikteta mbaya kuliko Hitler.
Mbowe hajawahi kukubali kukosolewa au hata tu mtu kuzungumzia Uenyekiti wake.

CCM ni chma cha kijamaa.
Chama cha Kilibearali kispokua na Demokrasia kama ilivyo Chadema ni hatari kuliko Genge la majambazi wale waliokua wanateka mabasi Biharamulo Kule Kagera.

Mbowe siwezi kumlinganisha na thamani ya Nchi hii na thamani ya ulimwengu wa Demokrasia.

Siku mtakapojua Demokrasia inajengwa kwa gharama kubwa ya kuweka mbali umaarufu,ubinafsi na kupoteza kwa ajili ya Taifa ndio siku mtakapojua kuwa Demokrasia ni kubwa kuliko Mbowe na Chadema.

Nchi za Afrika nyingi kwa kuendekeza watu zimejukuta zinaingiza vyama na watu wa hovyo madarakani kwa kisingizio cha kupigania Demokrasia ya kupata Urais ili waibie nchi.
Mwizi na dikteta kama Mbowe hawezi kamwe kuongoza mageuzi na harakati za kidemokrasia Tanzania.

Mtu yeyote atakayekuja na Hoja za kuipamba Chadema bila kueleza matatizo ya ndani ya Chadema ni lazima nitampinga na kuishambulia hiyo mana na Mbowe mana ndiye Dikteta aliyebaki kuhujumu Demokrasia akishirikiana na kundi Kubwa la Mafisadi ndani ya CCM. Kundi la wafanyabiashara wezi na wauza Unga.
Mbowe nyie mmemjua juzi.

Mimi Mbowe namjua mpaka Kijijini kwake Tangu 1994 . Ni kati ya Watu wasio na huruma na mtu yeyote linapokuja suala la Pesa na Umaarufu na Uhuni wa kila aina. Alipewa chama kwa wema akisogeze na kukabidhi wengine lakini alipogundua Fursa ya kufanya biashara za kuchapisha matisherti ,Kununua vifaa vya Chama kwa Tenda zake,kukikopesha chama na kujilipa mamilioni ya Ruzuku kama madeni hataki tena kuachia chama mpaka Kifie mikononi Mwaka na wajinga wachache wanaendelea kumuunga mkono kwa ubinafsi wao.
Taasisi yoyote isipokua na mabadiliko ya kiuongozi inageuka kuwa na matatizo ya Ukabila au udini!!

Mkumbatieni Mbowe tu mtabaki naye peke yake na Hakuna mtu atakayekubali kutumikishwa na Ziro mwingine. Bora yule ziro wa Kule kwenye mkoa mkubwa mana ameteuliwa tu. Lakini anayoyawaza na kuyafanya hana tofauti na Mbowe.
Mbowe kila siku ni mikakati na mipango na matamko yasiyotekelezeka kama Ziro mwenzake.

CCM chini ya Bashiru na JPM ni bora sana ukilinganisha na Chadema ya Mbowe isiyo na Itikadi zaidi ya kurukaruka na matukio.
Akili za vurugu na ubishi ubishi tu ndizo anazoziendekeza na kuziongoza ndani ya Chadema.

Sent using Jamii Forums mobile app
Well said!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kujifanya unanijua wewe! Weye unaishi chini ya jiwe hujui kuna watu wamepotea akina Ben Saanane, Azory Gwanda, miili kuokotwa ufukweni na watu kutekwa na kuteswa na lissu kutaka kuuawa? Ujuha wako wa kuamini ninachoandika humu kuhusu mauaji si kweli ni huko huko kwa majuha wenzio si humu.



Tatizo lako wewe kukariri!! Hivi ikatokea mgeni kaja tanzania ukimwambia kuna mauaji atakuelewa? Nani aliyeuwawa? Udhalimu udhalimu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa unamlaumu Mbowe wkt Lowassa aliletwa Chadema na Slaa akishirikiana na Gwajima,na Gwajima mwenyewe alikiri hilo na kusema Mbowe wala hakua ana mpango na Lowassa.

Slaa hakutegemea kama Lowassa angempindua kugombea urais alitegemea jamaa ataingia Chadema na kum-support Slaa kugombea urais.

Hasira za Slaa kuachana na Chadema sio sababu ni mzalendo sana wala nini bali ni sababu alikosa nafasi ya kugombea urais kupitia CDM.

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha ulofa, kama Slaa na Gwajima walimleta, Nani alikuwa mwenyekiti wa machadema ambaye alimpitisha kumkubali kugombea u raisi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niseme tu ukweli na kwa dhati kabisa kuwa!!
Chimbuko la CCM kuendelea kubaki madarakani,Ugumu Wa maisha pamoja na wakati huu mgumu Tunaopitia kutafta suruhisho la kisiasa pamoja na hamahama inayoendelea!

Chanzo ni mwenyekiti Wa chadema Freeman mbowe; Kosa la mbowe kubwa ni kumpa nafasi lowassa agombee Urais: hapo ndipo alitibua kila kitu, Lowassa ambaye alikuwa na maneno matatu tu unampaje nafas ya kugombea? ( asalam aleikum, tumsifu yesu kristo, naombeni kura), Hakika mbowe hata nikilala njaa sitaacha kukulaumu!
  • Wakati tukitafta manukato na pafyumu nzuri kubadili hali ya hewa ndani ya chadema tutambue huyu mbowe ndiye aliyeruhusu harufu mbaya iingie kwenye chumba cha chadema!
  • Mbowe ndiye aliyepakua kinyesi kutoka nje na kukiingiza ndani,
  • mbowe ndiye aliyeingiza kirusi kwenye ulimwengu Wa siasa ya hamahama,
  • Laiti kama Dr.slaa angeachwa agombee nguvu na imani ya chadema ingedumu.
  • laiti kama Dr. slaa angeachwa agombee Libumba asingejiweka mbembeni na UKAWA
  • Laiti kama Dr. slaa angegombea imani na mshikamano ndani ya ukawa ungedumu
  • Mbowe ndiye aliyesababisha hata CUF kusambaratika.
  • Mbowe ndiye aliyesababisha LIPUMBA awe mamluki hadi kupelekea Maalim sefu kuhamia ACT
  • Mbowe ndiye aliyesababisha CCM ikashinda kwa kishindo
  • Mbowe ndiye aliyesababisha wabunge wengi Wa chadema kusaliti chama.
  • Mbowe ndiye chanzo Machungu na maumivu ndani ya mioyo ya watu wengi!
KUSEMA UKWELI SIKU HIZI NAMCHUKIA SANA MBOWE HAFAI

Sina shaka hata ile audio crip iliyosambaa kipindi kile "Baby can u fly to AR" ilikuwa yake! NAMCHUKIA sana mbowe! KIUFUPI nabaki chadema Kwa heshima ya TUNDU LISSU TU SAHIVI lakini vinginevyo nisingebaki!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom