Watanzania wanapenda kuona sura mpya zinazokuja na mwamko Mpya.
Sio kwa sababu ya Mbowe.
Mbowe angemaliza tu muda wake akapumzika zake na ubunge wake.
Pia angepunguza maadui ambao sasa hawajulikani kuwa ni ndani ya Chama au nje.
Matokeo ya kung'ang'ania madaraka ni kuwa na maadui kila upande wengine wa kutengeneza tu. Ndio maana mpaka ndani ya Chama haamini MTU. Nje ya Chama haamini vyama vingine vya upinzani, kule CCM pia haamini mtu. Serikalini haamini mtu, kwenye vyombo vya dola haamini mtu. Angejua kuwa hakuna mtanzania anayemuunga mkono kwa kuhodhi Chama kama mali yake bali ni watu wenyewe wanaotafuta mabadiliko.
Nitakupa mfano.
Mrema alipofukuzwa Uwaziri na Mzee Ruksa alipotoka alipojiunga na NCCR mageuzi ,jina lake lilivuma sana na kupokelewa na mafuriko ya watu.
NCCR ikapanda Chati kwa kasi ya ajabu. Hapakua na mkakati wowote alioufanya nchi nzima ilivuma kwa kishindo cha mrema kujiunga na NCCR Mageuzi.
Wangetokea mashabiki maandazi kama wa Mbowe wangemsifu na kusema kuwa Mrema ni Mpambanaji mwenye mikakati ya kujenga Chama na blah blah nyingi wakati hakuna mkakati wowote zaidi ya watu kusaka mabadiliko popote wanapoona kuna mtu mpya.
2004 Bob Makani akamwachia Kijana Mdogo Freeman Aikael Mbowe aongoze Chadema kwa nafasi ya Uenyekiti.
Watanzania hasa vijana ambao walikua wamechoka na CCM na wengine hawakua na vyama wakakimbilia Chadema kwa sababu ya kuona ni Chama Pekee Chenye Mwenyekiti Kijana mdogo . Chama kukakimbiliwa na Vijana wengi wasaka mabadiliko ndani na nje ya Tanzania .
Mbowe akaendelea kuimarisha Chama Kwa wakati wake wa miaka Kumi kama walivyofanya waasisi wa Chama Bob Makani na Edwin Mtei ambao waliongoza kabla ya Mbowe.
Chadema kikafanikiwa kuungwa mkono na vijana na wasomi wengi.
Kijana msomi Zito Zuberi Kabwe naye kama Mbowe alikua na ndoto za kupokea Kijiti cha kuongoza Chama na kukipeleka Mbele zaidi.
Kama ilivyo kawaida muda wa Uenyekiti wa Mbowe ulipokaribia kuisha Zito alianza kujipanga kimkakati kutafuta uungwaji mkono.
Mbowe alijua wazi kabisa kuwa Zito alikua na uungwaji mkono mkubwa sana ndani na nje ya Chama kutokana na uwezo wake mkubwa katika kujenga hoja na kuungwa mkono na vijana wengi na wasomi.
Mbowe aliingiwa na hofu kubwa ya kuachia Uenyekiti kwenda kwa mtu mwingine. Kundi lake pia likawa na hofu ya kupoteza nafasi zao ndani ya Chama. Wakati huo pia Chama kilikua kimerudisha Ladha ya Ukabila na kaudini kwa mbali.
Zito akafuatiliwa kila anapokwenda kwa lengo la kumtafutia kisa cha kumwita msaliti ili aondolewe . Na kama sio uimara wa Zito kiroho na kimila nadhani wangekua wamemfanya kitu kibaya kabisa kama Chacha.
Mwaka 2015 Mbowe alicheza na akili za Zito na Lowasa na Kundi la ulipo tupo .
Watu wengi hawalielewi hili wanabaki tu kusema Mbowe amejenga Chama bila kujua kuwa Mbowe ndiye amevuruga Chama kwa kuua Demokrasia ya ndani na kujenga mfumo wa kibabe,kiburu ,matusi,kutishana ,dharau kwa wengine n.k.
Ndio maana vijana wengi wa Chadema ni viburi sana na kuhisi kila mtu ni mjinga hajui chochote isipokuwa wao tu.
Mbowe alipoona Lowasa amekatwa alianza kuingiwa na hofu kubwa juu ya Lowasa kwenda ACT kwa Zito Kabwe.Aligundua wazi kuwa Lowassa angeenda kwa Zito ungekua ndio mwisho wa Chadema kuwa na Mbunge Tanzania.
Mbowe alifanya juu chini kumtafuta Lowasa ajiunge Chadema.
Kwa hiyo 2015 mafriko yale yaliendelea kuwa ni ya Watanzania wenyewe kusaka Mabadiliko.
Namkumbusha Mbowe :-
.....Kila tunapokaribia uchaguzi kunatokea jambo Moja kubwa la kuwavuta watanzania wapenda mabadiliko kumfuata mtu maarufu. ACT wamelamba Dume . Kwa sasa ACT ndiyo habari ya mjini. Tujiulize ni kwa nini Maalim Seif pamoja na kuwa alikua ndani ya ukawa lakini hakujiunga na Chadema?! Bila shaka kila mtu atajua kuwa Uongozi wa Chadema haukubaliki na wapenda Mabadiliko.
Hata 2020 wengi watatoka CCM na CUF lakini hawatajiunga na Chadema chini ya Mbowe.
Labda akubali kuwapa watanzania kile wanachokitaka kwa muda mrefu yaani Sura mpya itakayowavuta wasaka Mabadiliko.
Sent using
Jamii Forums mobile app