Chilonwa wala magunzi kwa njaa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,782
239,464
Gazeti la mwananchi linaripoti kwamba wakazi wa jimbo hilo lililoko wilayani Chamwino wanakabiliwa na njaa kiasi cha kula Magunzi .

Taarifa zinadokeza kwamba awali wakazi hao walikuwa wanakula viwavi jeshi lakini baada ya mahitaji kuzidi uzalishaji wadudu hao wakaadimika na ndipo wananchi wakaamua kuchemsha magunzi kisha kuyatia chumvi na kuyafanya mlo .

My Take - Msaada wa dharula unahitaji ili kuondoa aibu dhidi ya ubinadamu .
 
Hivi watu wa Chilonwa wana nini kila mara kunakuwa na njaa huko si wahame waende mikoa mingine.
Wamasai na wasukuma wakiona mifugo yao haina malisho wanahama wanahamia mikoa mingine.Wachaga wengi wamehama kwa makundi wakahamia mikoa mingine .

Ni wakati muafaka kuwahamisha hao watu toka Chilonwa hiyo njaa ya kila miaka imeshakuwa kero kwa wengine sasa kila siku wao wa kusaidiwa tu .Nini hicho? MKUU WA MKOA AOENGEE na wakuu wa mikoa mingine iendeshwe operation ya kuhamisha watu wa CHILONWA upesi.Ila huko wanakohamishiwa wakilia njaa tena wakati rutuba ipo itabidi wacharazwe viboko kwa kuendekeza uvivu na uomba omba.
 
CCM wafia chama wenu wanakufa pelekeni chakula mbona tunasoma kwenye magazeti mmeokoa hela nyingi tangu muingie madarakani ? pelekeni unga tu ndugu zangu wana uwezo wa kula ugali hata na chumvi.
 
hilo halitawezekana maana tegemeo kubwa la ccm ni umasikini wa wananchi na njaa ya kuaibisha .
 
CCM wafia chama wenu wanakufa pelekeni chakula mbona tunasoma kwenye magazeti mmeokoa hela nyingi tangu muingie madarakani ? pelekeni unga tu ndugu zangu wana uwezo wa kula ugali hata na chumvi.
inasikitisha sana !
 
Gazeti la mwananchi linaripoti kwamba wakazi wa jimbo hilo lililoko wilayani Chamwino wanakabiliwa na njaa kiasi cha kula Magunzi .

Taarifa zinadokeza kwamba awali wakazi hao walikuwa wanakula viwavi jeshi lakini baada ya mahitaji kuzidi uzalishaji wadudu hao wakaadimika na ndipo wananchi wakaamua kuchemsha magunzi kisha kuyatia chumvi na kuyafanya mlo .

My Take - Msaada wa dharula unahitaji ili kuondoa aibu dhidi ya ubinadamu .
Huko ndiko makao makuu ya chama, ambapo mkoa mzima wabunge wake ni CCM na sasa wanakufa njaa na wala sishangai kusikia hospitali ya milembe ipo huko.
 
Wachaga wengi wamehama kwa makundi wakahamia mikoa mingine .
Hivi unafikiri kuwa wamehama kwa njaa? Kwa hiyo uchagani hakuna watu wanaishi kwa kuwa wamehama kwa makundi,nadhani huu haukuwa mfano sahihi kuutumia.
 
Wakuu mbona kama mnaonekana kushangilia matatizo ya binadamu wenzenu kwa sababu za kisiasa....hata kama watakuwa wamechagua CCM lakini hiyo haiwi sababu ya wewe kushangilia majanga yanayowakuta kwa sababu za kisiasa kwani ukiondoa siasa kando hao ni binaadamu wenzetu na wanahitaji faraja zetu...kama ambavyo wewe ungehitaji kufarijiwa pindi ambapo ungekutana na mitihani......

Mbona wakazi wa ubungo(mimi nikiwa mmoja wapo) wameishi miaka mitano bila ya maji safi na salama licha ya kuwa chini Mnyika na moja ya ahadi zake wake wa kampeni ilikuwa ni kuufanya historia uhaba wa maji ndani ya ubungo....!!

Watanzania tusifikie huko....utu kwanza...
 
hakuna siasa hapa mkuu , tumeweka hapa ili wadau wawasaidie hawa wahanga .
 
Wakuu mbona kama mnaonekana kushangilia matatizo ya binadamu wenzenu kwa sababu za kisiasa....hata kama watakuwa wamechagua CCM lakini hiyo haiwi sababu ya wewe kushangilia majanga yanayowakuta kwa sababu za kisiasa kwani ukiondoa siasa kando hao ni binaadamu wenzetu na wanahitaji faraja zetu...kama ambavyo wewe ungehitaji kufarijiwa pindi ambapo ungekutana na mitihani......

Mbona wakazi wa ubungo(mimi nikiwa mmoja wapo) wameishi miaka mitano bila ya maji safi na salama licha ya kuwa chini Mnyika na moja ya ahadi zake wake wa kampeni ilikuwa ni kuufanya historia uhaba wa maji ndani ya ubungo....!!

Watanzania tusifikie huko....utu kwanza...
We ngojea mbunge akuletee maji kama vile yeye ndiye mwenye vyanzo vya maji na mabomba ya kusambaza maji,maji kwa dar es salaam ni issue kwa sababu miundominu aijakaa vizuri na mmejenga holela na makazi ayajapangwa hilo bomba mnataka lipitishwe kwenye nguzo ya umeme mshushuwe majumbani kwenu,pole sana mpangilio wa mji wa dar ni mbovu sana hata mkitaka msambaziwe gesi majumbani haitakuwa rahisi kama wa maeneo ya sinza,masaki,oysterbay na tegeta au mpaka wajenge new dar es salaam city ndio mambo yatakaa sawa. Pia watu wanatakiwa wajitume kikweli kweli na dodoma wakazi wake walime ufuta,uwele,mihogo,karanga,ulezi ndio mkombozi wao ukifanya kazi umaskini kwako ni historia kama unabisha waulize wachina na taiwani maana ya kuukataa umaskini.Tungekuwa tunawaza mbali maeneo kama ya dodoma maji yangetoka ziwa victoria au tanganyika nakuja maeneo hayo kwa ajili ya kilimo na hili litawezekana tukiamua kuukataa umaskini.Ndio manake mchaga anakimbia huku na huku kutafuta shekeli na akipata hata kama yeye ajasoma,mtoto wake atasoma mpaka chuo kikuu.
 
Back
Top Bottom