Njaa Dodoma: Wananchi wala wadudu aina ya Viwavi Jeshi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,671
149,852
Wananchi wa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wanaripotiwa kula wadudu aina ya viwavi jeshi wanaojulikana kama fumbili kutokana na tatizo la njaa wilayani humo.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, madiwani wa kata husika wanajuta kugombea nafasi hizo kwani wananchi wanawalaumu na waliyasema hayo katika kikao cha dharura alichokiitisha mbunge wa Jimbo husika lenye kata 14.

Hii ni aibu kubwa na ni fedheha pia.

Hii ndio picha ya kiwavi jeshi katika gazeti husika

viwavi.jpg

========
Habari kamili:

Wakazi wa Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wanakula wadudu jamii ya viwavi jeshi, wanaojulikana kwa jina la fumbili kutokana na njaa kali iliyoikumba wilaya hiyo.

Hata hivyo, chakula hicho huenda kikapotea wakati wowote kutokana na mvua kutonyesha hivyo wadudu hao, ambao huishi kwa kutegemea majani, nao kupotea kwa kukosa chakula.

Mbali na fumbili, chakula kingine ambacho kilikuwa mkombozi kwa wakazi wengi, hususan Tarafa ya Chilonwa, ni matunda ya zambarau ambayo nayo yatakwisha wakati wowote kwani msimu wake umekwisha.

Chamwino ni wilaya iliyoko takriban kilomita 30 kutoka mjini Dodoma, ikikadiriwa kuwa na watu 349,714 na mazao ya chakula yanayolimwa kwenye wilaya hiyo ni mtama, uwele, mpunga, mahindi, mihogo, viazi vitamu, kunde, nyonyo, mbogamboga na choroko.

Juzi, Mbunge wa Chilonwa, Joel Mwaka aliitisha kikao cha dharura cha madiwani wote wa jimbo hilo lenye kata 14 kujadili suala hilo na kila diwani aliyechangia mjadala huo, alionyesha kujuta kugombea kwa kuwa wananchi wanamlilia.

Madiwani hao waliweka azimio la kusafiri kwenda Ikulu, Dar es Salaam kuwasilisha kilio cha wananchi wao.

Akizunguma kwenye kikao hicho, Mwaka alisema hali ya wakazi wa Chilonwa ni mbaya kiasi hakuna matumaini hata ya kupata mlo mmoja na badala yake wengi wanaishi kwa uji na matunda pori na fumbili.

Mbunge huyo alilaani mpango wa Serikali wa kuwapa vibali wafanyabiashara kwenda kuchukua mahindi katika ghala la chakula la Songea kwani bei zinakuwa kubwa.

“Ndiyo maana wanyabiashara wengi walikataa kwa kuwa bei inakuwa ni kubwa ambayo haiwezi kurudisha hata gharama zao, kitendo hicho kimefanya wafanyabiashara wa kawaida kuendelea kuwaumiza wananchi, lakini hakuna mwenye uwezo kipindi hiki, nasema walete mahindi ya bure siyo ya kununua tena,” alisema Mwaka.

Mbunge huyo alihoji ni kwa nini Serikali isiruhusu ghala la mahindi la Kizota, Dodoma kutoa mahindi kwa wafanyabiashara ili bei isiwe kubwa kama ilivyo sasa. Alisema bei ya sasa ya Sh15,000 kwa debe la kilo 20 ni kubwa na wachache ndiyo wanaoweza kuimudu.

Diwani wa Majeleko, Mussa Omari alifika kwenye kikao hicho akiwa na fumbili wengi akisema aliwakamata wakati akishirikiana na wapigakura wake kupata kitoweo.

Hata hivyo, hakuna diwani aliyeonyesha mshangao kwani kila mmoja alisema hata kwake wanakula wadudu hao na ni jambo la kawaida.

Mussa alisema hali ni mbaya zaidi kwenye kata yake na tayari baadhi ya watu wameanza kuvimba miguu kwa kukosa chakula, huku kukiwa na taarifa za vifo vinavyosadikiwa kuwa vimetokana na watu kukosa lishe.

Diwani wa Zajilwa, Farida Maulidi alisema katika eneo lake, kuna kaya 10 ambazo zimeelemewa zaidi na tayari kuna taarifa za vifo viwili. “Kwangu hali ni mbaya sana yaani naomba tuandamane kwenda hata kwa mkuu wa mkoa au niungane na wenzangu twendeni Ikulu tukamuone Rais. Mbona, pamoja na kusema hakuna mtu atakayekufa kwa njaa, huku watu wanateketea na sisi tupo? Kila siku nafanya kazi ya kutafuta uji kunusuru maisha ya watu wangu,” alisema Maulid.

Ofisa kilimo wa wilaya hiyo, Godfrey Mnyamale alikiri kuwa hali ni mbaya wilayani Chamwino na kusema kama juhudi za makusudi hazitachukulia ndani ya wiki moja, kutakuwa na madhara makubwa.

Mnyamale alisema tatizo kubwa lililoikumba Chamwino ni mvua kidogo zilizonyesha msimu wa mwaka jana iliyosababisha watu wasivune chakula cha kutosha.

Alisema ili kukabiliana na njaa iliyoanza wilayani humo tangu Aprili mwaka jana, jumla ya tani 14,377 za mahindi zinatakiwa kwenye vijiji 107, lakini hadi sasa Serikali imepeleka tani 150 tu ambazo ziligawiwa katika vijiji 10 tena kwa idadi ndogo.

Akizungumzia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa alisema Serikali haijalala katika kuwaza namna ya kuwasaidia.

Galawa alisema katika kipindi kilichopita, Chamwino ilipewa msaada wa chakula lakini kilikuwa hakitoshi na ndiyo sababu hakikupelekwa maeneo yote.

“Hata hivyo, lazima watu wajue kuwa huwezi kuomba chakula leo na ukapewa leo. Leo kamati ya mkoa imeshapeleka maombi taifa na juzi niliongea na mhusika kwamba wanalifanyia kazi,” alisema Galawa.

Kuhusu wafanyabiashara kulazimishwa kununua mahindi Songea badala ya Dodoma, alisema jambo hilo liko nje ya uwezo wake kwa kuwa wenye kuwapangia ni mamlaka ya chakula.

Aliwataka wanasiasa kuacha kukuza mambo kuwa kuna watu wamekufa kwa njaa, badala yake watumie muda huo kuwahamasisha wafugaji kuuza mifugo na kununua chakula.
 
Wananchi wa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wanaripotiwa kula wadudu aina ya viwavi jeshi wanaojulikana kama fumbili kutokana na tatizo la njaa wilayani humo.

Chanzo:Mwananchi online

Hii ni aibu kubwa na ni fedheha pia.

Ni kweli inasikitisha sana, na sasa wakati umefika wa kila Mtanzania kujitolea kile alichonacho kusadia ndugu zetu, ni ajabu sana mtu kama fisadi Lowasa anajimilikisha ranchi yetu ya Taifa anajaza ng'ombe maelfu kwa maelfu kwa ajili ya kupiga nao picha tu wakati watu wetu wanakula wadudu, kwa nini kama kweli ni mtenda haki asijitolee lori moja tu lililojaa ng'ombe na kuwampelekea hao wanaokula wadudu?

Inasikitisha sana kwa kweli!

upload_2016-1-10_10-3-23.jpeg
 
Umefilisika!!!!!!!!!!
 
Baada ya kuwaza jinsi gani serikali ya ccm itawasaidia wewe unamuwaza Lowassa tu, akili nyingine ni tatizo
 
Ni kweli inasikitisha sana, na sasa wakati umefika wa kila Mtanzania kujitolea kile alichonacho kusadia ndugu zetu, ni ajabu sana mtu kama fisadi Lowasa anajimilikisha ranchi yetu ya Taifa anajaza ng'ombe maelfu kwa maelfu kwa ajili ya kupiga nao picha tu wakati watu wetu wanakula wadudu, kwa nini kama kweli ni mtenda haki asijitolee lori moja tu lililojaa ng'ombe na kuwampelekea hao wanaokula wadudu?

Inasikitisha sana kwa kweli!

Pointless
Kifupi huna akili hata moja
Kila leo Lowasa mmetuchosha na huyo fisadi wenu mnamwimba kila siku
 
Pointless
Kifupi huna akili hata moja
Kila leo Lowasa mmetuchosha na huyo fisadi wenu mnamwimba kila siku

Lakini angalau nina akili za kujua kwamba ukiwa na ng'ombe maelfu halafu jirani yako anakufa njaa unapaswa kibinadamu na Kimungu pia umgawie angalau ng'ombe wachache ii aweze kupata chakula badala ya kuwatumia ng'ombe hao kupiga nao picha na kusambaza Ulimwenguni kote!

Lowassa-2.jpg
 
Acha waisome number eeeh Ccm mbele kwa mbeleeee
Tokea umesikia kuisoma namba chochote kinachokatizwa mbele yako unakibandika kusoma namba. Kwa Taarifa yako UNFP walishauri watu wale wadudu kwa vile wana viwango vingi vya virutubisho.
 
Ni kweli inasikitisha sana, na sasa wakati umefika wa kila Mtanzania kujitolea kile alichonacho kusadia ndugu zetu, ni ajabu sana mtu kama fisadi Lowasa anajimilikisha ranchi yetu ya Taifa anajaza ng'ombe maelfu kwa maelfu kwa ajili ya kupiga nao picha tu wakati watu wetu wanakula wadudu, kwa nini kama kweli ni mtenda haki asijitolee lori moja tu lililojaa ng'ombe na kuwampelekea hao wanaokula wadudu?

Inasikitisha sana kwa kweli!

CCM imejaza watu wa aina yako kuanzia huko Dodoma mpaka juu kabisa kwenye utawala tangu uhuru ndio maana watu wanakula wadudu wakati dodoma ina ardhi yenye rutuba.

Mbunge wa Bukoba mjini ,mh.Rwakatare alitoa madawa Hospitalini tena kwenye jimbo lake lakini serikali ya CCM ikakataa kupokea hizo dawa. CCM na serikali yake wakaona ni bora watu wafe kuliko kupokea msaada toka kwa mbunge wa chama kingine.
Leo hii unamtaja Lowasa eti atoe ngombe 10. Unataka mzee wa watu wamtoe utumbo kwamba ananipigia kampeni na uchaguzi umeisha.
Kama aliandamwa kwa kutoa sadaka kanisani na misikitini itakuaje akianza tena kusaidia tena kwenye ngome za wasoma namba wa CCM.
Wagogo wana ng'ombe wangi wachinje tu ngombe zao na sio kula wadudu wasio na viwango!
 
Mahala ambapo ni strong hold ya CCM huwezi kosa mambo kama hayo!

Mambo kama haya CCM and its luminaries watajaribu kuyaficha lakini yatasikika tuu!

Kingpins wa siasa na maendeleo ya Dodoma ni kina Ndungai na Malechela hawana msaada wowote?
 
Ccm ni janga LA kitaifa na Dodoma ndio makao makuu ya ccm sasa majanga yatawaandama mpaka muwafukuze hao jamaa Wa Lumumba.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Duuuh! Hiyo kitu nilikuwa naiona wakati mdogo watu wanajaza ndoo.Katika kujikimu na njaa,siku zote mwenye shibe hamjui mwenye njaa
 
Ccm ni janga LA kitaifa na Dodoma ndio makao makuu ya ccm sasa majanga yatawaandama mpaka muwafukuze hao jamaa Wa Lumumba.
Uwe na elimu basi ,uwezo wako Wa kufikili usifungwe na ccm.

Njaa ni natural disaster, the same as mafuriko.

Natural disaster haina chama
 
Back
Top Bottom