Child Hood Memories

nilikuwa naona kina Mwali na wenzie wako bize wanasimuliana kuhusu playstation sijui xbox 360, sasa wakati wetu ilikuwa hakuna izo ndude, kulikuwa na vitu kama hivi
na mimi ndo nilikuwa nashikilia ubingwa maana nilimaliza level zote.....
tumblr_m928wf2Ts51rv4c4zo1_1280.jpg


haya na nyie leteni kumbukumbu zenu za utotoni

Nimecheka C6, Unajua kwa nini. Ni juzi tu nimetoka kumnyanganya mwanangu hii game na kuificha kabisaa maana niliona masomo hazingatii kabisa ni game tu, hata concentration hana tena.
 
Unajua hapa jamvi, kuna vibweka vyake kama sio vituko!
**** members hapa akisema zamani zile unakuta anamaanisha 2002 , 1998 , 2000 na wengine 80"s wapo wa 70"s , na 60"s
kila kundi la members lina zamani yao!
Mf. Hapa zamani ya mtoa mada inaelekea early 90"s
sijui nayo ina sense kuitwa once upon a time ?
Mimi sijui .
 
mimi nakumbuka ilikuwa asubuhi siku hiyo sikwenda shule "chekechekea" .. ingawa ilikuwa sio mbali na home ni nyumba ya nyuma tu! ... tulivalishwa kanga "tulikuwa watatu" ... nikapewa hii game na mjomba ilikuwa mpya alikuwa amerudi kutoka ughaibuni ... kila mtu alikuwa mkarimu sana kwetu nyumbani siku hiyo....hadi nikawa nashngaa najiuliza hivi leo sikukuu ama..? jioni akaja rafiki yake mzee alikuwa anafnya kazi muhimbili akaja kutufanyia sunna "kutahiriwa" ... nikiona hii kitu nakumbuka hiyo siku! dah! siku niliyo ingia rasmi katika dunia ya uanaume !.....

Duh! kwa hiyo kila ukiona hiyo kitu zinakuja hisia za kutahiriwatahiriwa!
 
My darling watu8 umenikumbusha hiyo hadithi niliipenda sana na ile ya Binti Chura

mweeeh mweeeh khaa! yaani ungejua hizo hadhithi zilivyokuwa zinanikuna yaani kila ikifika mida mida sipanduki redioni, uko poa lakini my love measkron
 
Last edited by a moderator:
Michezo ilikuwa mingi wakati ule: kombolela, kujificha, kusaka sungura, kuwinda ndege, kupigana mieleka, "kuiba mapera" kwenye shamba la mtu..............kucheza mpira (gombania goli, mashuti) na vikorombwezo kibao tofauti na sasa wikendi ikifika watoto wanawaza kwenda beach, kuangali katuni, kwenda disko n.k
 
hivi kuna mtu anakumbuka mchezo fulani tulikuwa tuanimba:

ai gudi moooni moooni moooni
ai gudi fatabee fatabee


namtafuta rafiki rafiki rafiki
rafiki yenu nani nani

rafiki yangu xxxxxx
rafiki yangu xxxxxx
 
au kuna mtu anakumbuka ile mnaimba kuomba mvua? mvua njoo katarina usije mvua njoo katarina usije!!!

au kuna mtu anakumbuka mchezo wa mabetri?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom