Child Hood Memories

Joeli

JF-Expert Member
Apr 25, 2011
4,941
3,402
nilikuwa naona kina Mwali na wenzie wako bize wanasimuliana kuhusu playstation sijui xbox 360, sasa wakati wetu ilikuwa hakuna izo ndude, kulikuwa na vitu kama hivi
na mimi ndo nilikuwa nashikilia ubingwa maana nilimaliza level zote.....
tumblr_m928wf2Ts51rv4c4zo1_1280.jpg

haya na nyie leteni kumbukumbu zenu za utotoni
 
Last edited by a moderator:
my dear utoto wangu hivi vitu havikuwepo, nakumbuka mimi nilikuwa napika michanga na kuchoma sindano midori hahahaha. Hizi ni dotcom za watoto wangu ndiyo wamecheza.
 
Ha ha haaaa!!! Kumbe wewe ulikuwa unacheza ile michezo ya baba na mama?
 
Young Master na Caroline Danzi ujue enzi izo watoto wajanja tulikuwa ndo tunaacha kucheza kombolela tunahamia kwenye digital world, wakati tuko darasa la tatu mshikaji ndo akaja na nintendo gameboy ebanaeeeh wote tukaanza kuwa marafiki zake, unacheza kidogo anakunyang'anya hahahhahahhaha
 
Hela yote ya kula mihogo ilikuwa inaishia kwenye kununua betri za Game Boy na Brick Game...ha ha haaaa!!!
 
Ha ha haaaa!!! Kumbe wewe ulikuwa unacheza ile michezo ya baba na mama?

Mpaka leo napenda watoto na kuwahudumia. Unajua zamani hizo hatukuwa na michezo mingi zaidi ya kucheza Kombolela, rede, kuruka kamba, kukimbia, kuimba. sasa hivi watu wanaangalia DSTV, game kibao etc. Mimi nimeanza kuona TV ukubwani, kutwa tuliuwa tunasikiliza vipindi vya mama na mwana (Deborah Mwenda). Kila mumamosi saa nane lazima tugombanie radio.
 
You reminded me of ...these phrases
Oooh my god.....carry on ....thats good.​
 
dahhh
mi nakumbuka kutengeneza mipira ya nage na soksi, plastiki bagi halafu unaweka
jiwe katikati
ili mpira uwe mgumu a u travel fast.

halafu tulikuwa tunapenda kweli ku juggle na ndulele.

kitu cha dukani"special" tulicho kuwa nacho ni gololi..

nimemiss maisha yangu ya utoto.. to bad I can't go back :(
 
my dear utoto wangu hivi vitu havikuwepo, nakumbuka mimi nilikuwa napika michanga na kuchoma sindano midori hahahaha. Hizi ni dotcom za watoto wangu ndiyo wamecheza.

wengine walikuwa wanatengeneza watoto kwa kutumia vijiti na maua ya ndizi teketeke
 
Mpaka leo napenda watoto na kuwahudumia. Unajua zamani hizo hatukuwa na michezo mingi zaidi ya kucheza Kombolela, rede, kuruka kamba, kukimbia, kuimba. sasa hivi watu wanaangalia DSTV, game kibao etc. Mimi nimeanza kuona TV ukubwani, kutwa tuliuwa tunasikiliza vipindi vya mama na mwana (Deborah Mwenda). Kila mumamosi saa nane lazima tugombanie radio.

Hadithi za UA JEKUNDU
 
nilikuwa naona kina Mwali na wenzie wako bize wanasimuliana kuhusu playstation sijui xbox 360, sasa wakati wetu ilikuwa hakuna izo ndude, kulikuwa na vitu kama hivi
na mimi ndo nilikuwa nashikilia ubingwa maana nilimaliza level zote.....
tumblr_m928wf2Ts51rv4c4zo1_1280.jpg

haya na nyie leteni kumbukumbu zenu za utotoni

mimi nakumbuka ilikuwa asubuhi siku hiyo sikwenda shule "chekechekea" .. ingawa ilikuwa sio mbali na home ni nyumba ya nyuma tu! ... tulivalishwa kanga "tulikuwa watatu" ... nikapewa hii game na mjomba ilikuwa mpya alikuwa amerudi kutoka ughaibuni ... kila mtu alikuwa mkarimu sana kwetu nyumbani siku hiyo....hadi nikawa nashngaa najiuliza hivi leo sikukuu ama..? jioni akaja rafiki yake mzee alikuwa anafnya kazi muhimbili akaja kutufanyia sunna "kutahiriwa" ... nikiona hii kitu nakumbuka hiyo siku! dah! siku niliyo ingia rasmi katika dunia ya uanaume !.....
 
mambo ya kula furu na ubuyu wa maji ule!dah!enzi izo mlimani primary!wapi mama mndolwa na mwl mlacha,mama semboja,mama mmari,mwl mjwahuzi,mwl elihuruma,!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom