Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Hawa jamaa wawili Sitta na Mwakyembe ni wamedhihirisha upuuzi wao katika hili kwa kujifanya waongeaji. Km wao wanaamini katika dhana ya kupambana na ufisadi kwanini wasikae kando? Yaani Uwaziri wanautaka na wakati huohuo wanaishambulia serikali ambapo na wao ni sehem ya serikali.
Sitta na Mwakyembe wanajaribu kuficha aibu. Najua hawachomoki katika hili. They were supposed to foresee the repucation of breaching the Dowans contract. Were are paying Dowans b'se of Bunge fail to foresee!!
It's shame to have those kind of people!
mi nadhan wapo sawa cz hwz kuta2a matatz ukiwa mbal nayo "fimbo ya mbali haiui nyoka",acha waendelee kubaki na positions zao hk wakiendelea kupamban na ufisad wa ndg zao kwa ukarb zyd "juen kweli,nayo kwel itawaweka huru"Hawa jamaa wawili Sitta na Mwakyembe ni wamedhihirisha upuuzi wao katika hili kwa kujifanya waongeaji. Km wao wanaamini katika dhana ya kupambana na ufisadi kwanini wasikae kando? Yaani Uwaziri wanautaka na wakati huohuo wanaishambulia serikali ambapo na wao ni sehem ya serikali.
Tatizo JK hakuwapa uwaziri hawa SITTA na MWAKYEMBE kwa roho moja ...aliwapa kwa lengo la kuwaziba mdomo tu ...na wao wanajuwa ...ndio maana hawataacha kuongea pale ambapo wanahisi maoni yao kupuuzwa barazani.
Kwa bahati mbaya hawakulazimishwa na walikuwa na bado wanahaki ya kukataa nafasi zile. Hizi kauli zao zinatofauti gani na wafanyakazi wanaomwibia mwajiri wao? Au marketing officer anayachafua bidhaa za kampuni aliyoajiriwa. Upuuzi wa namna hii haupo. Hapa ninasisitiza aidha watoke serikalini au wafunge midomo yao.
:A S thumbs_up:Hawa jamaa wawili Sitta na Mwakyembe ni wamedhihirisha upuuzi wao katika hili kwa kujifanya waongeaji. Km wao wanaamini katika dhana ya kupambana na ufisadi kwanini wasikae kando? Yaani Uwaziri wanautaka na wakati huohuo wanaishambulia serikali ambapo na wao ni sehem ya serikali.
SAKATA la malipo ya kampuni ya kufua umeme ya Dowans, limeingia hatua mpya baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utawala Bora, Mathias Chikawe, kusema mawaziri wawili waliompinga Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kutangaza serikali kuilipa kampuni hiyo, walikiuka utaratibu wa serikali.
Aidha, amewataka mawaziri hao, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kuacha kutoa maelezo ya sekta zisizowahusu kwani si utaratibu wa utawala bora na ni kuwachanganya wananchi.
Akifafanua kuhusu kauli zilizompinga Waziri Ngeleja, Chikawe alisema mawaziri hao walipaswa kufuata utaratibu wa kufikisha hoja zao kwa Mamlaka husika, au wajiondoe serikalini kabla ya kupingana na waziri mwenzao.
Alisema Waziri Sitta ni mzoefu na wa siku nyingi, hahitaji kufundishwa, kwa kuwa ameshika nyadhifa mbalimbali serikalini na anafahamu namna za kutoa maoni kwa mawaziri bila kuathiri utaratibu.
Kuhusu Mwakyembe, alisema ingawa ni mpya katika uwaziri, lakini ni mwanasheria wa siku nyingi na anajua utaratibu wa sheria ulivyo, hivyo pia hakuhitaji kufundishwa kuhusu namna ya kutoa mawazo yake kuhusu Dowans wakati akiwa serikalini tena Naibu Waziri.
Umefika wakati Sitta na Mwakyembe waache kuendesha mambo kisiasa, bali waangalie sheria zaidi katika suala la Dowans, alisema Chikawe.
Alisema kitendo cha mawaziri hao kumkosoa Waziri Ngeleja, kutokana na kutangaza hadharani kuilipa kampuni hiyo Sh bilioni 94, kimetoa picha kuwa kuna mgongano ndani ya Baraza la Mawaziri.
Alisema jambo zito kama hilo, halikupaswa kutolewa maelezo magazetini, bali wangetumia utaratibu wa kumfuata waziri husika na kutoa maoni na ushahidi walionao na iwapo wangeona waziri huyo hawatilii maanani, wangekwenda kwa Waziri Mkuu au Rais.
Unajua Rais wetu ni mwepesi sana kuwasikiliza mawaziri wake wakati wowote, sasa iwapo wangeona waziri husika hawasikilizi, wangepeleka hoja yao kwake ambaye kama angeridhishwa na hoja zao, angeitisha kikao cha Baraza la Mawaziri kutoa uamuzi wa pamoja, alisema Chikawe.
Chikawe alisema kuna utaratibu wa aina mbili, ambao waziri anaweza kuutumia kutoa uamuzi wa Serikali; kwanza ni kutoa uamuzi unaohusu wizara yake na mwingine, uamuzi wa pamoja.
Alifafanua kuwa waziri wa sekta husika, ana jukumu la kutoa uamuzi wowote wa wizara yake bila kuingiliwa na akiona kuna jambo zito linaloathiri sera za nchi, ndio hupeleka kwenye Baraza la Mawaziri ili lijadiliwe kabla ya kutoa uamuzi wa pamoja.
Chikawe alisema Waziri Sitta na Naibu Waziri Mwakyembe, walikuwa na nafasi ya kumwona Rais na kutoa ushahidi wao na iwapo Rais angeona kuna umuhimu wa kuitisha Baraza la Mawaziri, angefanya hivyo na si kutoa siri za Baraza kuwa hawajalijadili suala hilo.
Alisema maoni binafsi kwa mawaziri hao si tatizo, ndiyo maana katika Baraza la Mawaziri, kikao kinaweza kujadili suala moja kwa siku nzima mpaka wanafikia uamuzi wa pamoja, lakini kuyazungumzia hadharani ni kosa, kwa kuwa wamekiuka utaratibu wa utawala bora kwa kutoa siri za Baraza hilo.
Chikawe alimtetea Ngeleja kuwa inawezekana hakuona sababu ya kupeleka suala la kuilipa Dowans kwa Baraza la Mawaziri kwa kuwa alishirikisha wataalamu mbalimbali wa sheria na
kujiridhisha katika kufanya malipo kwa kampuni hiyo.
Wiki iliyopita, Waziri Sitta alipinga tamko la Waziri Ngeleja la kuilipa kampuni ya Dowans na kusema kuwa inashangaza waziri kutoa tamko hilo kabla hata Baraza la Mawaziri halijalijadili.
Juzi pia Naibu Waziri Mwakyembe, aliibuka na kusema anashangaa kusikia kampuni hiyo aliyoiita ya kitapeli, inalipwa kwa madai kuwa ilirithi mkataba wa kufua umeme kutoka katika kampuni hewa ya Richmond LCC Ltd.
Katika Bunge lililopita chini ya Spika Sitta, Mwakyembe aliongoza Kamati Maalumu iliyochunguza suala la kampuni ya kufua umeme ya Richmond hata kusababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri wawili, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha, kujiuzulu kutokana na kashfa ya kampuni hiyo.
HabariLeo | Dowans yawatafuna Sitta na Mwakyembe
:A S thumbs_up:
JK awatoe basii kwani wao wanabembeeleza kuwemo serikali chafu??wewe chikawe unakiuka kiapo chako cha uwt???unasafisha upuuzi...mamama weee nchi imekwisha ona Membe alivyokuwa shujaaa....kumbuka kiapo chenu kimoja nyie usije ukayalamba matapishi yako siku ifikia??
Ni aibu gani hiyo wanayoificha tuambie seems you are speaking the opposite nani kati ya kina Sitta na mnaotetea Dowans wanaojaribu kuficha aibu, jaribuni kumwogopa Mungu hata siku moja, nyie ndio mlioleta madudu how comes wanaopinga hayo madudu wawe ndio waficha siri tena.Sitta na Mwakyembe wanajaribu kuficha aibu. Najua hawachomoki katika hili. They were supposed to foresee the repucation of breaching the Dowans contract. Were are paying Dowans b'se of Bunge fail to foresee!!
It's shame to have those kind of people!
Chikawe kuwakemea mawaziri wenzake anatumia mamlaka yake vibaya (ultra vires).
Huu ni mtazamo wa "Samaki mmoja akioza wote wameoza"
Chikawe hana madaraka wala uwezo wa kulazimisha nidhamu kwa waziri yeyote. Kama yeye aliona kuwa wenzake wamekosea kwanini na yeye asimwambie Waziri Mkuu au Rais yeye mwenyewe? Sasa kesho kina Mwakyembe nao wakimjibu kwa magazeti ataona wamemvunjia heshima au wamevunja kanuni?