Chikawe amvua nguo Tundu Lisu Bungeni!

Chikawe amvua nguo Tundu Lisu Bungeni!

Chikawe amemuumbua Tundu Lisu bungeni jioni hii kwa kutoa ushahidi kuwa Bw. Beatus Kipeya ambaye Lisu na Chadema wanadai kuwa alienguliwa na WDC ya Sombetini asiwe mjumbe wa baraza la katiba la kata kuwa ni mjumbe halali na hivyo kuthibitisha kuwa Tundu Lisu na Chadema anajaribu kulidanganya bunge na wananchi.

hivi Lisu ule ukichaa alishapona?

Ndo maana unajiita mzalendo K!! Hiyo K ndo inatafasiri akili yako.
 
Chikawe amemuumbua Tundu Lisu bungeni jioni hii kwa kutoa ushahidi kuwa Bw. Beatus Kipeya ambaye Lisu na Chadema wanadai kuwa alienguliwa na WDC ya Sombetini asiwe mjumbe wa baraza la katiba la kata kuwa ni mjumbe halali na hivyo kuthibitisha kuwa Tundu Lisu na Chadema anajaribu kulidanganya bunge na wananchi.

hivi Lisu ule ukichaa alishapona?

Hapo kwenye red,uyu si ndo mbunge aliye peleka SANDA jimboni badala ya maji?na mwshoni umeamua kutukana au umenukuu?
 
Haya kapokee ujira wako wa buku saba lumumba. Waliokutuma watakuwa wameona bidii yako kwa siku ya leo.
 
Chikawe amemuumbua Tundu
Lisu bungeni jioni hii kwa kutoa ushahidi kuwa Bw. Beatus Kipeya ambaye
Lisu na Chadema wanadai kuwa alienguliwa na WDC ya Sombetini asiwe
mjumbe wa baraza la katiba la kata kuwa ni mjumbe halali na hivyo
kuthibitisha kuwa Tundu Lisu na Chadema anajaribu kulidanganya bunge na
wananchi.

hivi Lisu ule ukichaa alishapona?

Njaa yako itakufanya upewe mimba isiyokua na baba.
 
Someni vizuri hapa, hakuna mahali ambapo Lissu (au CHADEMA in that context) wamesema Bw. Kipeya ameondolewa. Waziri Chikawe ndiye kajibu vitu visivyokuwepo, tunachelea kusema kadanganya. Someni hapa chini;



Mheshimiwa Spika,

Hata mahali ambapo wananchi wasiokuwa wanaCCM walifanikiwa kupenyeza katika chekecheke la mchujo wa WDC wamefanyiwa mizengwe na wanaCCM ili waondolewe katika orodha ya wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya. Mfano mzuri ni yaliyomkuta Bw. Beatus Kipeya aliyechaguliwa mjumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Arusha Mjini kwa kupitia Kata ya Sombetini. Mara baada ya Bw. Kipeya kuchaguliwa kwenye kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Sombetini cha tarehe 8 Aprili, 2013, siku hiyo hiyo Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha Allan G. Kingazi alimwandikia Mkuu wa Wilaya ya Arusha barua ya malalamiko juu ya kuchaguliwa kwa Bw. Kipeya.

Pamoja na kumpa Mkuu wa Wilaya ‘salaam za Chama’ chao, Katibu wa CCM Kingazi alilalamika kwamba Afisa Mtendaji wa Kata ya Sombetini amemruhusu “... raia wa Burundi Bwana Beatus Ndanyahubwi Kipea (ambaye katika kugombea ametumia jina la Beatusi Kipea ili asijulikane kama ni Mrundi – ila mtu wa Kigoma yaani Muha) kugombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya na akashinda, kinyume na maagizo ya Tume ya Katiba, kwamba Mjumbe ni lazima awe Raia wa Tanzania.”

Baada ya maelezo mengi kuhusu ‘Urundi’ wa Bw. Kipeya, Katibu wa CCM Kingazi anamwambia Mkuu wa Wilaya yafuatayo: “... (N)ashauri matokeo ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Katiba ufutwe na utangazwe upya. Aidha, Afisa Mtendaji huyo achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuvuruga kwa makusudi Uchaguzi wa Muundo wa Baraza la Katiba la Wilaya.”

Mheshimiwa Spika,

Kitu cha kwanza cha kushangaza kuhusu barua ya Katibu wa CCM Kingazi ni kwamba aliyetumiwa malalamiko ni Mkuu wa Wilaya ambaye, kwa mujibu wa ibara ya 42(3), 44(3) na 46(3) ya Katiba ya CCM Toleo la 1982, Mkuu wa Wilaya ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya, Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya na Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya. Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Mwongozo wa Tume, Mkuu wa Wilaya hana mamlaka yoyote kushughulikia jambo lolote linalohusu uchaguzi wa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya. Kwa maana hiyo, sababu pekee ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha kuandikiwa malalamiko haya ni kwa sababu ni kada wa CCM!

Mheshimiwa Spika,

Ukiacha Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Arusha, watu wengine wote walionakiliwa barua ya malalamiko ya Katibu wa CCM Kingazi ni makada wa CCM. Hivyo basi, nakala za malalamiko hayo zinaonyeshwa kupelekwa kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Katibu wa CCM Mkoa, Mkuu wa Mkoa (ambaye pia ni mjumbe wa vikao vyote vya kikatiba vya CCM katika ngazi ya mkoa), Afisa usalama wa Taifa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha. Wote hawa hawahusiki kisheria kwa namna yoyote ile katika mchakato wa uundaji wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya. Chombo pekee ambacho kinahusika kisheria na mchakato wa kuunda Mabaraza hayo na ambacho kilitoa Mwongozo wa namna ya kuyaunda, yaani Tume, haikuandikiwa wala kunakiliwa barua ya malalamiko ya Katibu wa CCM Kingazi!

Mheshimiwa Spika,

Mara tu baada ya Afisa Uhamiaji Mkoa wa Arusha Bw. R. Gowelle kupata nakala yake, alimwandikia Bw. Kipeya barua ya ‘wito wa kufika ofisi ya uhamiaji Mkoa wa Arusha’, ambapo alimtaka kufika ofisini kwake ‘bila kukosa wala kutuma mwakilishi.’ Cha kushangaza ni barua hiyo imenakiliwa kwa Afisa Mtendaji Kata ya Sombetini, Mwenyekiti wa Mtaa wa Kirika A, Sombetini na Balozi wa Mtaa wa Zurich, Sombetini.

Mbali na Afisa Mtendaji Kata ambaye alikuwa mlalamikiwa, wengine wote walionakiliwa barua ya Afisa Uhamiaji Mkoa ni makada wa CCM na, kwa taarifa za Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ndio walikuwa chanzo cha malalamiko ya Katibu wa CCM Kingazi. Kwa taarifa za Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Bw. Kipeya ni raia halali wa Tanzania anayetoka katika Jimbo la Muhambwe katika Wilaya ya Kasulu ya Mkoa wa Kigoma. Dhambi pekee na kubwa aliyoifanya na kustahili kusumbuliwa na Idara ya Uhamiaji ni kugombea na kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Arusha wakati yeye sio mwanachama wa CCM.
 
Chikawe amemuumbua Tundu Lisu bungeni jioni hii kwa kutoa ushahidi kuwa Bw. Beatus Kipeya ambaye Lisu na Chadema wanadai kuwa alienguliwa na WDC ya Sombetini asiwe mjumbe wa baraza la katiba la kata kuwa ni mjumbe halali na hivyo kuthibitisha kuwa Tundu Lisu na Chadema anajaribu kulidanganya bunge na wananchi.

hivi Lisu ule ukichaa alishapona?

ati mzalendo??? duh wewe ni kilaza balaa. hakuna kitu cha maana ulichoongea naona umeamua kunya kwa kutumia mdomo.

kavuliwaje nguo. mbona mnajidhalilisha utu wenu kwa kuishi mkiwategemea nnape na nchemba. mwaka huu mtaumbuka mpaka mkome
 
Reply yangu inampa pole jamaa wa magamba anayejaribu kupotosha watu eti chikawe amvua nguo Lisu
 
Magamba bwana, wanaweweseka hadi wanachopost kwenye uzi hata havieleweki. Hivi huwa mnakaguliwa kwamba leo umepost threads ngapi au mmelimitiwa kwa cku zinatakiwa threads 10. Kachukue chako kazi umeshamaliza.
 
Chikawe amemuumbua Tundu Lisu bungeni jioni hii kwa kutoa ushahidi kuwa Bw. Beatus Kipeya ambaye Lisu na Chadema wanadai kuwa alienguliwa na WDC ya Sombetini asiwe mjumbe wa baraza la katiba la kata kuwa ni mjumbe halali na hivyo kuthibitisha kuwa Tundu Lisu na Chadema anajaribu kulidanganya bunge na wananchi.

hivi Lisu ule ukichaa alishapona?

Vakupagate ve chinzehe!!!!
 
Lisu hana hoja zaidi ya kurumbana na watu bungeni
 
Ugonjwa wa akili wanao magamba uwongo wao huufanya kuwa ukweli
 
Hayo ni maoni yake ni lazima kuyaheshimu,lakini yanaukweli ndani yake fuatilia vizuri hotuba ya lisu na chikawe.
 
Kwani chikawe siku hizi anaogesha wenzake?
Anyways, siku ingine itabidi aawambie waheshimiwa wavue wenyewe.
 
Tundu lisu bungeni. Anaongea,anafundisha sheria, anawafundisha mawaziri kazi zao,anamfundisha spika kazi zake, anamfundisha mwanasheria wa serikali kazi zake. SASA SI WAMUONGEZEE POSHO
 
Back
Top Bottom