Chikawe amvua nguo Tundu Lisu Bungeni!

Chikawe amvua nguo Tundu Lisu Bungeni!

unamuuliza nami? .umuhimu wa LISU ni wabunge 10 wa CCM
 
Hivi kwa kuanzisha uzi mbovu kama huu unalipwa pia...ningekuwa mimi ndio paymaster wenu,leo ungelala njaa.
 
Wakati mwingine si vizuri kujibizana na mtu kama Mzalendo K kwani yeye keshalipwa kwa kupost mada hata kama ni pumba kama ilivyo.
 
Last edited by a moderator:
Wakati mwingine si vizuri kujibizana na mtu kama Mzalendo K kwani yeye keshalipwa kwa kupost mada hata kama ni pumba kama ilivyo.
 
Last edited by a moderator:

hivi kwa kuanzisha uzi mbovu kama huu unalipwa pia...ningekuwa mimi ndio paymaster wenu,leo ungelala njaa.

mbona wenzenu wakija na mada za kukisifu chama kisicho chadema, mara nyingi lazima mseme wanalipwa, kwani hawawezi kuwa wakereketwa kama nyinyi. Wana cdm acheni kasumba vumilieni kipigo , hivyo ndivyo siasa ilivyo.

Mmesahau vurugo ya mtwara wana cdm mlivyotamba hapa jukwani, nikongeza senti zangu mbili, katika bunge hili cdm imebainisha kuwa iko tayari kutumia kila njia ili wawe washindi kila mahali, kwani wametua uongo wa hali duni sana na kujiabisha
 
Lisu anapenda kuonekana kwenye TV na kujifanya mjuaji kumbe hata huku mtaani wapo wanao jua zaidi yake sema nafasi ni ngumu,inaiokosa serikali kwa mengi na anaweka changa moto nzuri ila anazidi paka anakuwa kero.
 
Thread nyingine zimefanana na chakula cha nguruwe.
Hata aliyeanzisha atakuwa anafaa kwa chakula cha nguruwe tu.
Ni kweli kabisa hata maoni yako yanasomeka kinguruwenguruwe, nadhani mwandishi wake pia atakuwa na tabia za nguruwe kama naye si nguruwe, tena nguruwe mweusi.:A S thumbs_down:😛ainkiller:
 
Someni vizuri hapa, hakuna mahali ambapo Lissu (au CHADEMA in that context) wamesema Bw. Kipeya ameondolewa. Waziri Chikawe ndiye kajibu vitu visivyokuwepo, tunachelea kusema kadanganya. Someni hapa chini;



Mheshimiwa Spika,

Hata mahali ambapo wananchi wasiokuwa wanaCCM walifanikiwa kupenyeza katika chekecheke la mchujo wa WDC wamefanyiwa mizengwe na wanaCCM ili waondolewe katika orodha ya wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya. Mfano mzuri ni yaliyomkuta Bw. Beatus Kipeya aliyechaguliwa mjumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Arusha Mjini kwa kupitia Kata ya Sombetini. Mara baada ya Bw. Kipeya kuchaguliwa kwenye kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Sombetini cha tarehe 8 Aprili, 2013, siku hiyo hiyo Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha Allan G. Kingazi alimwandikia Mkuu wa Wilaya ya Arusha barua ya malalamiko juu ya kuchaguliwa kwa Bw. Kipeya.

Pamoja na kumpa Mkuu wa Wilaya ‘salaam za Chama’ chao, Katibu wa CCM Kingazi alilalamika kwamba Afisa Mtendaji wa Kata ya Sombetini amemruhusu “... raia wa Burundi Bwana Beatus Ndanyahubwi Kipea (ambaye katika kugombea ametumia jina la Beatusi Kipea ili asijulikane kama ni Mrundi – ila mtu wa Kigoma yaani Muha) kugombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya na akashinda, kinyume na maagizo ya Tume ya Katiba, kwamba Mjumbe ni lazima awe Raia wa Tanzania.”

Baada ya maelezo mengi kuhusu ‘Urundi’ wa Bw. Kipeya, Katibu wa CCM Kingazi anamwambia Mkuu wa Wilaya yafuatayo: “... (N)ashauri matokeo ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Katiba ufutwe na utangazwe upya. Aidha, Afisa Mtendaji huyo achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuvuruga kwa makusudi Uchaguzi wa Muundo wa Baraza la Katiba la Wilaya.”

Mheshimiwa Spika,

Kitu cha kwanza cha kushangaza kuhusu barua ya Katibu wa CCM Kingazi ni kwamba aliyetumiwa malalamiko ni Mkuu wa Wilaya ambaye, kwa mujibu wa ibara ya 42(3), 44(3) na 46(3) ya Katiba ya CCM Toleo la 1982, Mkuu wa Wilaya ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya, Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya na Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya. Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Mwongozo wa Tume, Mkuu wa Wilaya hana mamlaka yoyote kushughulikia jambo lolote linalohusu uchaguzi wa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya. Kwa maana hiyo, sababu pekee ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha kuandikiwa malalamiko haya ni kwa sababu ni kada wa CCM!

Mheshimiwa Spika,

Ukiacha Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Arusha, watu wengine wote walionakiliwa barua ya malalamiko ya Katibu wa CCM Kingazi ni makada wa CCM. Hivyo basi, nakala za malalamiko hayo zinaonyeshwa kupelekwa kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Katibu wa CCM Mkoa, Mkuu wa Mkoa (ambaye pia ni mjumbe wa vikao vyote vya kikatiba vya CCM katika ngazi ya mkoa), Afisa usalama wa Taifa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha. Wote hawa hawahusiki kisheria kwa namna yoyote ile katika mchakato wa uundaji wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya. Chombo pekee ambacho kinahusika kisheria na mchakato wa kuunda Mabaraza hayo na ambacho kilitoa Mwongozo wa namna ya kuyaunda, yaani Tume, haikuandikiwa wala kunakiliwa barua ya malalamiko ya Katibu wa CCM Kingazi!

Mheshimiwa Spika,

Mara tu baada ya Afisa Uhamiaji Mkoa wa Arusha Bw. R. Gowelle kupata nakala yake, alimwandikia Bw. Kipeya barua ya ‘wito wa kufika ofisi ya uhamiaji Mkoa wa Arusha’, ambapo alimtaka kufika ofisini kwake ‘bila kukosa wala kutuma mwakilishi.’ Cha kushangaza ni barua hiyo imenakiliwa kwa Afisa Mtendaji Kata ya Sombetini, Mwenyekiti wa Mtaa wa Kirika A, Sombetini na Balozi wa Mtaa wa Zurich, Sombetini.

Mbali na Afisa Mtendaji Kata ambaye alikuwa mlalamikiwa, wengine wote walionakiliwa barua ya Afisa Uhamiaji Mkoa ni makada wa CCM na, kwa taarifa za Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ndio walikuwa chanzo cha malalamiko ya Katibu wa CCM Kingazi. Kwa taarifa za Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Bw. Kipeya ni raia halali wa Tanzania anayetoka katika Jimbo la Muhambwe katika Wilaya ya Kasulu ya Mkoa wa Kigoma. Dhambi pekee na kubwa aliyoifanya na kustahili kusumbuliwa na Idara ya Uhamiaji ni kugombea na kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Arusha wakati yeye sio mwanachama wa CCM.
Makene,kuwa katika chama cha upinzani Tanzania ni lazima uwe na moyo wa chuma!!!!!
Maelezo yapo wazi lakini watu wako myopic,hawataki kusoma hata paragraph tatu,hawataki kuchambua mambo,ni aibu kubwa.
Alichoeleza Lisu ni mfumo na jinsi gani unavyoweza kuathiri mchakato na ushahidi katoa.
Sasa naamini kuna mawaziri wanalala baada ya kunywa vidonge vya usingizi vinginevyo watakuwa wanaweweseka kwa kujitahidi kutunga uongo na kuukimbia UKWELI.Kazi ipo!!!!!!!!
 
Mzalendo??? Au mnafiki??? We umejivua nguzo mwenyewe fikiria kati ya anejivua na kuvuluiwa nguo!!!

hapa una malipo tu!! Insatiable kinyaaa mno!!!!

Kwani cdm wamekubali klpi cha ccm?
 
huwa napata shida ninapoona ccm muda wote wanahangaika sio kuendeleza nchi, bali kupambana na wapinzani, muda wao wote mwingi wanautumia kwenye kuhangaika na vyama vya upinzani....ningekuwa ndio mimi, nanyamaza tu nafanya kwa vitendo ili vitendo viwe ushahidi, sasa hadi sasa walichokifanya tangu washita madaraka hakilingani na miaka waliyokaa, walitakiwa kufanya zaidi sana ya walivyofanya sasa, muda mwingiii kupoteza kuhangaika na watu binafsi, badala ya kuongea au kufanya mambo yenye faida kwa taifa. usione hapo amefurahi sana akirudi home kuona amemsema tundu lisu amelidanganya bunge, sio kwamba yeye leo amefanya kitu cha maana sana bungeni kwaajili ya taifa, bali " mama watoto, leo nimemkomoa kweli tundu lisu..."..hahaha.
Wabunge wa Ccm wamesahau kazi wananchi waliowatuma wamesahau sasa wamebaki kuishabikia serekali nakuisafisha , wabunge wote wa Ccm wasirudi tena 2015
 
Mkuu makene, hata kama mimi ndiyo ningekuwa kwenye nafasi ya chikawe nisingethubutu kutetea ujinga wa Migiro alioufanya wa mawasiliano na wasaidizi wake kwani ni ujinga wa mwisho. Hata chikawe mwenyewe inaonyesha amekerwa na hizo taarifa za Migiro kuingilia mchakato wa katiba wakati akijua ni kosa la jinai.Kaamua kupotezea ili migiro ajitetee mwenyewe.Hii inaonyesha mawaziri wamepata fundisho baada ya Nchimbi kutetea JANGILIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII
 
kiswahli ni janga kwa taifa na wewe mleta maada ulifaulu kiswahili na unasema ni lugha yako ya taifa. tafakari na chukua hatua lugha inaonekana ni tatizo kubwa sana kwako
 
Wanakimbia hoja za msingi, wakipata cha kuongea basi wanashupaliiia, tunajua hujuma zilizofanywa ni hivyo vyombo walivyovipatia hilo jukumu la kichama sio kwa manufaa ya waTz, sasa waacheni waongee, Ule mwisho umekaribia, You can fool some people sometime but you cannot fool all the people all the time
 
Back
Top Bottom