Chikawe amvua nguo Tundu Lisu Bungeni!

Chikawe amvua nguo Tundu Lisu Bungeni!

kuna mahali imetajwa adhabu atakayoipata yeyote atakayejifanya ofisa wa tume au kuingilia kazi za tume ! Hebu Makene tuwekee hiyo bhana ! Sipati picha Mwigulu kunyea ndoo aisee !
 
Huyo Lissu sio yule ambaye mke wake anazalia watoto USA ,ili wawe raia wa USA,KWELI kama ni mzalendo mbona wife wake asijifungulie Tanzania kama Watanzania wengine? Pia kuna Waziri mwingine kijana ana mtindo huu...Hawa wanachezea watanzania hawana mapenzi na nchi yetu!
 
Someni vizuri hapa, hakuna mahali ambapo Lissu (au CHADEMA in that context) wamesema Bw. Kipeya ameondolewa. Waziri Chikawe ndiye kajibu vitu visivyokuwepo, tunachelea kusema kadanganya. Someni hapa chini;



Mheshimiwa Spika,

Hata mahali ambapo wananchi wasiokuwa wanaCCM walifanikiwa kupenyeza katika chekecheke la mchujo wa WDC wamefanyiwa mizengwe na wanaCCM ili waondolewe katika orodha ya wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya. Mfano mzuri ni yaliyomkuta Bw. Beatus Kipeya aliyechaguliwa mjumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Arusha Mjini kwa kupitia Kata ya Sombetini. Mara baada ya Bw. Kipeya kuchaguliwa kwenye kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Sombetini cha tarehe 8 Aprili, 2013, siku hiyo hiyo Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha Allan G. Kingazi alimwandikia Mkuu wa Wilaya ya Arusha barua ya malalamiko juu ya kuchaguliwa kwa Bw. Kipeya.

Pamoja na kumpa Mkuu wa Wilaya ‘salaam za Chama’ chao, Katibu wa CCM Kingazi alilalamika kwamba Afisa Mtendaji wa Kata ya Sombetini amemruhusu “... raia wa Burundi Bwana Beatus Ndanyahubwi Kipea (ambaye katika kugombea ametumia jina la Beatusi Kipea ili asijulikane kama ni Mrundi – ila mtu wa Kigoma yaani Muha) kugombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya na akashinda, kinyume na maagizo ya Tume ya Katiba, kwamba Mjumbe ni lazima awe Raia wa Tanzania.”

Baada ya maelezo mengi kuhusu ‘Urundi’ wa Bw. Kipeya, Katibu wa CCM Kingazi anamwambia Mkuu wa Wilaya yafuatayo: “... (N)ashauri matokeo ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Katiba ufutwe na utangazwe upya. Aidha, Afisa Mtendaji huyo achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuvuruga kwa makusudi Uchaguzi wa Muundo wa Baraza la Katiba la Wilaya.”

Mheshimiwa Spika,

Kitu cha kwanza cha kushangaza kuhusu barua ya Katibu wa CCM Kingazi ni kwamba aliyetumiwa malalamiko ni Mkuu wa Wilaya ambaye, kwa mujibu wa ibara ya 42(3), 44(3) na 46(3) ya Katiba ya CCM Toleo la 1982, Mkuu wa Wilaya ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya, Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya na Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya. Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Mwongozo wa Tume, Mkuu wa Wilaya hana mamlaka yoyote kushughulikia jambo lolote linalohusu uchaguzi wa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya. Kwa maana hiyo, sababu pekee ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha kuandikiwa malalamiko haya ni kwa sababu ni kada wa CCM!

Mheshimiwa Spika,

Ukiacha Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Arusha, watu wengine wote walionakiliwa barua ya malalamiko ya Katibu wa CCM Kingazi ni makada wa CCM. Hivyo basi, nakala za malalamiko hayo zinaonyeshwa kupelekwa kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Katibu wa CCM Mkoa, Mkuu wa Mkoa (ambaye pia ni mjumbe wa vikao vyote vya kikatiba vya CCM katika ngazi ya mkoa), Afisa usalama wa Taifa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha. Wote hawa hawahusiki kisheria kwa namna yoyote ile katika mchakato wa uundaji wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya. Chombo pekee ambacho kinahusika kisheria na mchakato wa kuunda Mabaraza hayo na ambacho kilitoa Mwongozo wa namna ya kuyaunda, yaani Tume, haikuandikiwa wala kunakiliwa barua ya malalamiko ya Katibu wa CCM Kingazi!

Mheshimiwa Spika,

Mara tu baada ya Afisa Uhamiaji Mkoa wa Arusha Bw. R. Gowelle kupata nakala yake, alimwandikia Bw. Kipeya barua ya ‘wito wa kufika ofisi ya uhamiaji Mkoa wa Arusha’, ambapo alimtaka kufika ofisini kwake ‘bila kukosa wala kutuma mwakilishi.’ Cha kushangaza ni barua hiyo imenakiliwa kwa Afisa Mtendaji Kata ya Sombetini, Mwenyekiti wa Mtaa wa Kirika A, Sombetini na Balozi wa Mtaa wa Zurich, Sombetini.

Mbali na Afisa Mtendaji Kata ambaye alikuwa mlalamikiwa, wengine wote walionakiliwa barua ya Afisa Uhamiaji Mkoa ni makada wa CCM na, kwa taarifa za Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ndio walikuwa chanzo cha malalamiko ya Katibu wa CCM Kingazi. Kwa taarifa za Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Bw. Kipeya ni raia halali wa Tanzania anayetoka katika Jimbo la Muhambwe katika Wilaya ya Kasulu ya Mkoa wa Kigoma. Dhambi pekee na kubwa aliyoifanya na kustahili kusumbuliwa na Idara ya Uhamiaji ni kugombea na kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Arusha wakati yeye sio mwanachama wa CCM.

Mkuu Tumaini Makene

Asante kwa kuweka sawasawa kisu kwenye mfupa! Hakika umemaliza ubishi ulio kuwa unalazimishwa na mleta kioja! Samahani nasema ni kioja maana siioni hoja ya kutufanya tuchimbuke kwa tafakuri jadidi ndio maana umemaliza kwa ku-copy na ku-paste sehemu tu ya hotuba ya Lissu.

Kwa kumsaidia mleta hoja naomba kumtuma yafuatayo.

1. Ajiulize kwa nini Mzee Chikawe kakwepa kujibu hoja nyingi za Mh TL? Mfano mmoja. ..."Mh spika, Kambi rasmi ya upinzani inaita serikali itoe kauli mbele ya bunge lako tukufu kama ccm au viongozi na makada wake wamefanya mawasiliano yoyote na vyombo vitakavyo simamia kura ya maoni juu ya katiba mpya kama jinsi nyaraka za ccm zillivyo elezea hapo juu".
Nyaraka anazo eleza TL ni nyaraka ya siri ya mama mwenye heshima ya kimataifa (Migiro) akipeleka maelekezo kwa Nape, Mwigulu, Zakia meghji, na Mohamedi Khatibu akihimiza kazi ya kuwatia hamasa makatibu wa mkoa wasimamie mchakato wa kupata wajumbe wa katiba. Mleta mada haoni kuwa hii ni aibu kubwa kwa mtu mwenye hadhi kama mama Migiro?!

2. Ajiulize kwa nini Chikawe kakwepaa kujibu ile milioni 18 ya special diet kwa ajili ya wajumbe ambao watapata maambukizi ya ukimwi wakiwa kwenye majukumu?! Yaani kodi ya watanzania itumike kuwalisha vizuri watu watakao pata ukimwi kwa starehe zao?! Mleta uzi alitakiwa kujihoji kwa haya kabla ya kuleta vioja.

Naomba kuishia hapo.
 
Last edited by a moderator:
Mzalendo??? Au mnafiki??? We umejivua nguzo mwenyewe fikiria kati ya anejivua na kuvuluiwa nguo!!!

hapa una malipo tu!! Insatiable kinyaaa mno!!!!

CDM ni chama cha matukio tu. Kazi yake ni kusubiri serikali ifanye kosa kidogo ili iandae maandamano. Nje ya fujo chadema hawana cha kufanya. Ndio mana hata hapa JF utawaona wanaCDM hata hekima hawana. Wana ubishi wa kitoto na fikra mgando.
 
Nataka kujua zile mil 18 za masuala ya ukimwi

Wanajua kuwa wataambukizana ukimwi kwani hela wanazochukua ni nyingi mno. Lakini watanzania tumejua sasa kuwa kamati ya Warioba ni kitu gani, wanatekeleza maagizo ya nani. Na kiukweli ccm mpaka Raisi anatangaza kukubali kuanzisha mchakato wa kupata katiba mpya, walishapanga nini na mahali gani watafanya hujuma. Mambo haya yatapelekea kura ya maoni kuwa NO na kutulazimisha kuingia gharama nyingine zaidi kuurudia mchakato
 
Hiyo imenitoa jasho, kumbe tayari walijua wanenda kufanya ufusika,da! Hili ajab jingine la dunia

Wangetenga na pesa kwa ajili ya ajali,maralia,kipindupindu,starehe waweke uwezekano wa magonjwa yote,kwanini wameainisha ukimwi tu? Mmmmmmh hii nchi inahitaji kui restart.tumeshakosea kuanza real watz wenzangu
 
Hivi hawa chadema wanajua mwisho wao umekaribia.
 
Chikawe amemuumbua Tundu Lisu bungeni jioni hii kwa kutoa ushahidi kuwa Bw. Beatus Kipeya ambaye Lisu na Chadema wanadai kuwa alienguliwa na WDC ya Sombetini asiwe mjumbe wa baraza la katiba la kata kuwa ni mjumbe halali na hivyo kuthibitisha kuwa Tundu Lisu na Chadema anajaribu kulidanganya bunge na wananchi.

hivi Lisu ule ukichaa alishapona?
Nyie misukule wa mwigulu mna shida sana
 
C bure, kuna chochote kitu unapokea kwa habar uliyoipost hapa
Chikawe amemuumbua Tundu Lisu bungeni jioni hii kwa kutoa ushahidi kuwa Bw. Beatus Kipeya ambaye Lisu na Chadema wanadai kuwa alienguliwa na WDC ya Sombetini asiwe mjumbe wa baraza la katiba la kata kuwa ni mjumbe halali na hivyo kuthibitisha kuwa Tundu Lisu na Chadema anajaribu kulidanganya bunge na wananchi.

hivi Lisu ule ukichaa alishapona?
 
mbona yupo uchi tangu zamani kanjanja wa sheria

jamani mi napata sana shida kwa thread km hz, hv walivomrudisha beatus baada ya kuona wanaaibika ndo kuvuliwa nguo lisu? mbona hawajabisha kuwa walimsumbua kwa kutumia uhamiaji? aibu nyingne kwenu. unasema lisu ni kanjanja wa sheria, vp kuhusu majaji ambao matokeo yao mpaka leo hayaonekani kwny vyuo walivyosoma? km unayoshaka na jambo hili hebu fuatilia thread zilizopita. bt much smale, hv mnaonaje mkitafta kazi halali kuliko kazi mnayofanya ya kuzibua vyoo vinavonuka?
 
kuna mahali imetajwa adhabu atakayoipata yeyote atakayejifanya ofisa wa tume au kuingilia kazi za tume ! Hebu Makene tuwekee hiyo bhana ! Sipati picha Mwigulu kunyea ndoo aisee !

Hii hapa mkuu


Mheshimiwa Spika,

Kwa mujibu wa kifungu cha 56(a) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 ya Sheria za Tanzania, mamlaka inayohusika kupanga vituo vya kupigia kura ni Msimamizi wa Uchaguzi, yaani Mkurugenzi wa Jiji, Mkurugenzi wa Manispaa, Mkurugenzi wa Mji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya. Wasimamizi hawa wa uchaguzi wamelalamikiwa kwa miaka mingi na vyama vya upinzani kwa kupendelea CCM na wagombea wake katika chaguzi mbali mbali. Hawa ndio wanaotakiwa wawasiliane na Makatibu wa CCM Mikoa ili wapange vituo vya kupigia kura ya maoni juu ya Katiba Mpya!

Mheshimiwa Spika,

Mawasiliano haya ya viongozi wa ngazi za juu za CCM yanathibitisha kwamba mchakato wa Katiba Mpya umeiingiliwa na kuhujumiwa kwa kiasi kikubwa na CCM. Aidha, mawasiliano haya yanathibitisha kauli iliyotolewa mbele ya Bunge lako tukufu na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wakati wa mjadala wa hoja ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwamba “...viongozi wa kiserikali kama vile Wakuu wa Wilaya na wa Mikoa waliwahamasisha wenyeviti wa vijiji, mitaa na madiwani kuhakikisha kwamba wagombea wote wasiokuwa wa CCM, hasa wa CHADEMA, wanaenguliwa katika chaguzi za vijiji, mitaa au kata.” Aidha, mawasiliano haya yanathibitisha kauli ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwamba Mabaraza ya Katiba ya Wilaya yaliyochaguliwa kwa utaratibu “...ni mabaraza ya CCM na sio mabaraza ya katiba ya Watanzania wote.”
 
duh.....aisee....hivi vijisent ndio vina haribu mind zenu hivyo....wehu bana
 
Chikawe ni moja ya watu wajinga sana duniani waliowahi kuingia katika baraza la mawaziri, hawezi kujibu hoja yeyote ya Lissu sana sana atatoa matusi ya nguoni.
 
Huyo Lissu sio yule ambaye mke wake anazalia watoto USA ,ili wawe raia wa USA,KWELI kama ni mzalendo mbona wife wake asijifungulie Tanzania kama Watanzania wengine? Pia kuna Waziri mwingine kijana ana mtindo huu...Hawa wanachezea watanzania hawana mapenzi na nchi yetu!

MMMMMH! Jamani humu ndani mbona kuna harufu nyingi xana za magamba? hasa we unasema nini hapa? hoja iliyopo wala haiusiani na jambo unalosema, au umeshaambukizwa ugonjwa wa mwigulu nchemba na lusinde?
 
Chikawe amemuumbua Tundu Lisu bungeni jioni hii kwa kutoa ushahidi kuwa Bw. Beatus Kipeya ambaye Lisu na Chadema wanadai kuwa alienguliwa na WDC ya Sombetini asiwe mjumbe wa baraza la katiba la kata kuwa ni mjumbe halali na hivyo kuthibitisha kuwa Tundu Lisu na Chadema anajaribu kulidanganya bunge na wananchi.

hivi Lisu ule ukichaa alishapona?

Njaa kweli mbaya wewe njaa unaivalia karatasi ya nylon??ifiche wewe hata kuificha kwa gunia umeshindwa?
 
Chikawe ni moja ya watu wajinga sana duniani waliowahi kuingia katika baraza la mawaziri, hawezi kujibu hoja yeyote ya Lissu sana sana atatoa matusi ya nguoni.

watu wa aina hii hayati mwl nyerere aliwahi kuwashangaa na kuwauliza hv walikuwa wanaccm km yeye? ni kwasababu ya kucmama na kubwatuka mambo yaso yamsingi km chikawe anavofanya.
 
Back
Top Bottom