Chifu MKWAWA alimpinga Nyerere Kwa Hili.

Drjacka92

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
445
522
Katika Kuhakikisha anatokomeza Uchifu hapa nchini, Mwalimu Nyerere aliwaza kuwapa madaraka mengine makubwa zaidi Serikalini. Katika Kuhakikisha anafanikiwa aliwataka machifu wakagombee Ubunge kwenye maeneo yao.

Hapo ndipo Utata ulianza MKWAWA alipinga suala la kwenda kuwapigia magoti na kuwasihi wananchi wake wampe kura ,alikataa katakata japo baadhi ya machifu waligombea na wakapata. Nyerere aliamua kumpa Chifu MKWAWA u Spika wa Bunge. MKWAWA ndie Spika wa Bunge aliyeongoza Kwa muda mrefu tangu 1962-1973 kisha akawa waziri, ilipofika mwaka 1975 alipewa tena Uspika mpaka 1994.

Na hali hiyo ndio imepelekea Uspika wa Bunge kupewa mtu yeyote hata asiye MBUNGE, kitu ambacho Kinalalamikiwa kuwa kinapelekea Kulifanya Bunge kuwa Bubu.
 
Siyo kweli,

Machifu wote wa wakati huo, nadhani hata Chief Malleare, walipewa kazi za kiserikali siyo za kisiasa; hawakutakiwa kugombea ubunge. Hao ni pamoja na wale ambao hawakuwa na elimu ya maana; ama walipewa Uwaziri, ubalozi, ukamishina, U-RC, u-DC, Division Secretary (katibu Tarafa) au cheo chochote serikalini kulingana na elimu yake. Machifu maarafu ambao elimu zao ziliruhusu ni pamoja na Chief Adam Sapi wa uheheni aliyepewa uspika, Chief Erasto Mang'enya wa usagara akawa kamishana wa tume ya uchaguzi, Chief Abdallah Fundikira wa unyanyembe akawa Waziri, Chief Michael Lukumbuzya wa ukerewe akawa balozi, Chief Masanja wa usukumani akawa mkuu wa mkoa, Chief Mataba wa ukara akawa DC, Chief Edward Wanzagi Nyerere wa uzanaki akawa mshauri maalumu wa rais, wengine wengi ambao elimu zilikuwa kiduchu kama akina Chief Kingalu wa Matombo na wengineo walibadilishwa vyeo kutoka kuwa Chief na kuwa Division Secretary (yaani katibu Tarafa kwa leo).

Niliwahi kufanyia research topic hii na nilikuwa nataka kuipost hapa ila hali ya hewa imekuwa siyo nzuri siku hizi kiasi kuwa ni vigumu mtu kutumia muda wako mrefu kuandika jambo ulilofanyia kazi halafu ukaambuliwa matusi kutoka watu wasiojua lolote.
 
Siyo kweli,

Machifu wote wa wakati huo, nadhani hata Chief Malleare, walipewa kazi za kiserikali siyo za kisiasa; hawakutakiwa kugombea ubunge. Hao ni pamoja na wale ambao hawakuwa na elimu ya maana; ama walipewa Uwaziri, ubalozi, ukamishina, U-RC, u-DC, Division Secretary (katibu Tarafa) au cheo chochote serikalini kulingana na elimu yake. Machifu maarafu ambao elimu zao ziliruhusu ni pamoja na Chief Adam Sapi aliyepewa uspika, Chief Erasto Mang'enya akawa kamishana wa tume ya uchaguzi, Chief Abdallah fundikira akawa Waziri, Chief Michael Lukumbuzya akawa balozi, Chief Masanja akawa mkuu wa mkoa, Chief Mataba akawa DC, Chief Edward Wanzagi Nyerere akawa mshauri maalumu wa rais, wengine wengi ambao elimu zilikuwa kiduchu walibadilishwa vyeo kutoka Chief kuwa na Division Secretary (yaani katibu Tarafa kwa leo).
Nashukuru kwa mchango wako wa hoja.
 
Siyo kweli,

Machifu wote wa wakati huo, nadhani hata Chief Malleare, walipewa kazi za kiserikali siyo za kisiasa; hawakutakiwa kugombea ubunge. Hao ni pamoja na wale ambao hawakuwa na elimu ya maana; ama walipewa Uwaziri, ubalozi, ukamishina, U-RC, u-DC, Division Secretary (katibu Tarafa) au cheo chochote serikalini kulingana na elimu yake. Machifu maarafu ambao elimu zao ziliruhusu ni pamoja na Chief Adam Sapi wa uheheni aliyepewa uspika, Chief Erasto Mang'enya wa usagara akawa kamishana wa tume ya uchaguzi, Chief Abdallah Fundikira wa unyanyembe akawa Waziri, Chief Michael Lukumbuzya wa ukerewe akawa balozi, Chief Masanja wa usukumani akawa mkuu wa mkoa, Chief Mataba wa ukara akawa DC, Chief Edward Wanzagi Nyerere wa uzanaki akawa mshauri maalumu wa rais, wengine wengi ambao elimu zilikuwa kiduchu kama akina Chief Kingalu wa Turiani na wengineo walibadilishwa vyeo kutoka kuwa Chief na kuwa Division Secretary (yaani katibu Tarafa kwa leo).

Niliwahi kufanyia research topic hii na nilikuwa nataka kuipost hapa ila hali ya hewa imekuwa siyo nzuri siku hizi kiasi kuwa ni vigumu mtu kutumia muda wako mrefu kuandika jambo ulilofanyia kazi halafu ukaambuliwa matusi kutoka watu wasiojua lolote.
Erasto Mang'enya alikuwa chifu wa Wabondei na alikuwa Mbunge wa Muheza kwa miaka mingi.
 
kwaio leo ndio umehisi utahurumiwa na hayo matusi,basi sawa!
 
Erasto Mang'enya alikuwa chifu wa Wabondei na alikuwa Mbunge wa Muheza kwa miaka mingi.
Chief Erasto Mang'enya pia likuwa Balozi wa Kudumu wa Tanganyika na baadae Tanganyika and Zanzibar Umoja wa Mataifa, New York, kuanzia mwaka 1963. Hapa akiwa na UN Secretary General U Thant.

215745.jpg

Chied Adam Sapi Mkwawa alikuwa spika dhaifu kuliko wote waliowahi kutokea, na hii ni kwa sababu aliongoza bunge la chama kimoja.

Nyerere alikuwa akipata idea anaanza kuiandika chini asubuhi, mchana anampa Kawawa makaratsi ayavushe barabara mpaka Karimjee Hall, jioni makaratasi yanarudishwa Ikulu kusainiwa kuwa sheria.

Bunge la Chief Mkwawa lilipitisha sheria ya Muungano kwa staili hii hii, ya asubuhi idea, mchana mjadala bungeni, jioni Sheria, kwa hati ya dharula.
 
Erasto Mang'enya alikuwa chifu wa Wabondei na alikuwa Mbunge wa Muheza kwa miaka mingi.
Sawa, nafikiri nimekosea kidogo kuhusu utemi wake, lakini hakugombea ubunge ili kuacha utemi, bali alikuwa na nafasi kubwa sana serikalini ya kusimamia uchaguzi. Nadhani aliwahi kuandika kitabu kinaitwa Uchaguzi ni wako. Kama baadaye aliamua kugombea ubunge haikuwa ni shinikizo la Nyerere.
 
Kukua kwangu mkuu na kuelewa maana ya mbunge ni kwakuwa Mbunge Mang'enya alisimuliwa sana home na wazee, ninadhani hata ubunge wenyewe hakuwa na mpinzani enzi zile.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom