Orodha ya Spika wa Bunge waliowahi kuongoza Bunge la Tanzania

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Bwana Job Ndugai ni Spika wa 6 wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tanganyika ilipotangazwa Jamhuri mwaka 1962, Chifu Adam Sapi Mkwawa alichaguliwa kuwa Spika wa kwanza wa bunge la Tanganyika.

Mwaka 1964 baada ya Muungano bunge la Tanganyika na bunge la Jamhuri ya watu wa Zanzibar yakafa na kuzaliwa bunge moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (kabla haijaitwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania). Adam Sapi akawa Spika wa bunge hilo.

Kwahiyo Mzee Sapi alikuwa Spika wa kwanza wa bunge la Tanganyika (kabla ya muungano) na Spika wa kwanza wa bunge la Tanzania (baada ya muungano). Alitumikia nafasi hiyo kwa miaka 11 hadi November 19 mwaka 1973.

November 20 mwaka 1973 Chifu Erasto Mang'enya akachaguliwa kuwa Spika. Huyu alikuwa Chifu wa Wabondei na miongoni mwa watanzania wa mwanzo kupata shahada ya chuo kikuu. Kabla ya uhuru aliongoza kama mkuu wa shule kwenye shule za sekondari Malangali, Old Moshi, na Tanga school.

Baada ya Uhuru aliteuliwa kuwa Waziri wa mawasiliano, kabla ya kuwa Balozi wa Tanzania kwenye umoja wa mataifa mjini New York. Mwaka 1965 alirudishwa nchini na kuteuliwa Waziri wa Maendeleo ya jamii na utamaduni.

Mwaka 1973 akachaguliwa kuwa Spika wa bunge kumrithi Adam Sapi Mkwawa. Akaongoza hadi November 05 mwaka 1975 akapumzishwa. Chifu Adam Sapi akarudishwa tena kwenye nafasi hiyo.

Sapi akaongoza hadi April 25 mwaka 1994 (miaka 19) kisha akakabidhi kiti hicho kwa Pius Msekwa, ambaye alikabidhi kwa Samuel Sitta, kisha Anne Makinda na sasa Bwana Ndugai.

Ukitizama orodha hiyo utagundua Adam Sapi Mkwawa ndiye Spika aliyeongoza bunge kwa muda mrefu zaidi. Amekuwa Spika kwa jumla ya miaka 30 (miaka 11 awamu ya kwanza na 19 awamu ya pili). Lakini leo kwenye tukio la kukabidhiwa majoho kwa maspika wastaafu hakuwekwa kwenye orodha hata familia yake haikutoa mwakilishi.

Chifu Erasto Mang'enya nae ametumikia miaka miwili kama Spika wa bunge, lakini nae hakukumbukwa.

Chifu Adam Sapi na Chifu Mang'enya ndio waliotengeneza mfumo wa bunge letu ulivyo leo. Ni Maspika ambao historia zao zimeandikwa kwa wino wa dhahabu. Lakini hawakutajwa wala kukumbukwa kwenye tukio la leo. Kwanini?

*Malisa G. Jan 28, 2020*
 
Back
Top Bottom