Maspika wa Bunge waliomtangulia Job Ndugai

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,358
1- Spika wa kwanza wa Bunge la Tanzania huru, Adam Sapi Mkwawa, aliyeongoza kwa takribani miongo mitatu - alikuwa na sifa kubwa mbili; kwanza alikuwa Chifu mwenye heshima kubwa kutoka katika kabila la Wahehe lakini pia akiwa na historia ya kuwa mmoja wa watu weusi wa kwanza kuingia bungeni katika historia ya Tanganyika (Tanzania). Yeye na Chifu Abdieli Shangali wa Uchagani ndiyo walikuwa weusi wa kwanza kuingia bungeni wakati huo likiitwa Baraza la Kutunga Sheria mnamo mwaka 1947.
Mkwawa alikuwa akiheshimika kwa sababu hakukuwa na mbunge mwingine aliyekuwa amewahi kuingia bungeni kabla yake. Hata Baba wa Taifa, Julius Nyerere, alianza kujihusisha na siasa wakati Mkwawa tayari mbunge na mwanasiasa anayejulikana. Hili lilijenga heshima baina ya wawili hao - ikisadifu pia kwamba Nyerere alitoka katika ukoo wa kichifu pia.

2- Spika wa Bunge wa pili, Chifu Erasto Mang'enya, naye alikuwa kiongozi wa kijadi wa kabila la Wabondei lakini aliyekuwa na sifa ya kushiriki katika harakati za kuwania Uhuru wa Tanganyika; akiwa mmoja wa Watanzania wa awali kabisa kuwa na elimu ya shahada ya kwanza (degree). Mwalimu Nyerere alimheshimu kwa elimu yake na maarifa aliyokuwa nayo.

3- Spika wa Bunge wa tatu, Pius Msekwa, hakuwa Chifu wala mbunge kama Mkwawa. Lakini wakati anaanza kuwa Spika kwenye miaka ya 1990, tayari alikuwa akionekana kama mtu anayelifahamu Bunge la Tanzania pengine kuliko yeyote mwingine. Alikuwa Katibu wa Bunge baada ya Uhuru na hivyo alikuwa kama mkunga wa taasisi hiyo kiutawala. Hakukuwa na mtu aliyekuwa na shaka juu ya umahiri wake kwenye Bunge.

4- Spika wa Bunge wa nne, Samwel Sitta, alikuwa na faida ya kuwa swahiba wa kisiasa wa Rais Jakaya Kikwete aliyeshiriki katika mapambano ya kumwingiza madarakani. Kwa sababu hiyo, Uspika wake ulikuwa na mamlaka kwa sababu alikuwa na nguvu kama swahiba wa Rais lakini pia mwanasiasa mkongwe aliyeingia bungeni miaka 30 kabla hajawa Spika.

5- Spika wa Bunge wa tano, Anne Makinda, hakuwa na ukaribu na Kikwete kama ule aliokuwa nao sita, lakini yeye alikuwa na uzoefu wa takribani miongo 4 ndani ya Bunge - akiwa ametumikia takribani mawaziri wakuu watatu - Edward Sokoine, Salim Ahmed Salim na Cleopa Msuya - kama Waziri wa Nchi (Bunge) na CCM ikimnadi kwamba ilitaka Spika wa Bunge mwenye jinsia ya kike. Hakukuwa na mwanasiasa mwanamke aliyekuwa na 'sifa' zilizotakiwa wakati ule kuwa Spika kumzidi Makinda.

6- Spika wa Bunge wa sita, Job Ndugai, huyu ndiye sipika aliye achia ngazi alikuwa spika toka mwaka 2015 katika awamu ya Magufuli mpaka sasa alipo jihuzulu tarehe 6 mwezi wa kwanza,2022.
Ndugai alipata Uspika kwa sababu ya siasa za uchaguzi za Bunge. Hakuwa na Uchifu wa Mkwawa, uzoefu wa Msekwa, bahati na umahiri wa Makinda wala ushawishi wa Sitta. Alikuwa amewahi kuwa Naibu Spika wa Bunge - sifa mojawapo ya watangulizi wake wawili waliokuja kuwa maspika baadaye; lakini Unaibu pekee si sifa ya moja kwa moja ya kumfanya mtu kuwa Spika. Hayati Sitta alikuwa Spika pasipo kuwahi kuwa Naibu.

Hili lilimaanisha kwamba Ndugai hakuwa na pa kushika kama ngome yake na baadaye alifanya uamuzi wa kuamua kuegemea kwenye mamlaka ya Rais Magufuli. Lakini, tofauti na Sitta ambaye alishiriki kwenye kumpambania Kikwete ashinde urais - Ndugai hakuwa sehemu ya kampeni ya Magufuli wala mmoja wa watu wake wa karibu. Kifo cha Magufuli Machi mwaka jana kilimaanisha kuanguka kwa nguzo kuu ya ukubwa wake bungeni.
 
Active Mhariri Diversity Moderator Cookie niunganishie Uzi huu

Uwe pamoja na huu uliyo tangulia
 
Umesahau sifa yake kuu kuwa ndye supika mboovu kuliko wote nchi hii
1- Spika wa kwanza wa Bunge la Tanzania huru, Adam Sapi Mkwawa, aliyeongoza kwa takribani miongo mitatu - alikuwa na sifa kubwa mbili; kwanza alikuwa Chifu mwenye heshima kubwa kutoka katika kabila la Wahehe lakini pia akiwa na historia ya kuwa mmoja wa watu weusi wa kwanza kuingia bungeni katika historia ya Tanganyika (Tanzania). Yeye na Chifu Abdieli Shangali wa Uchagani ndiyo walikuwa weusi wa kwanza kuingia bungeni wakati huo likiitwa Baraza la Kutunga Sheria mnamo mwaka 1947.
Mkwawa alikuwa akiheshimika kwa sababu hakukuwa na mbunge mwingine aliyekuwa amewahi kuingia bungeni kabla yake. Hata Baba wa Taifa, Julius Nyerere, alianza kujihusisha na siasa wakati Mkwawa tayari mbunge na mwanasiasa anayejulikana. Hili lilijenga heshima baina ya wawili hao - ikisadifu pia kwamba Nyerere alitoka katika ukoo wa kichifu pia.

2- Spika wa Bunge wa pili, Chifu Erasto Mang'enya, naye alikuwa kiongozi wa kijadi wa kabila la Wabondei lakini aliyekuwa na sifa ya kushiriki katika harakati za kuwania Uhuru wa Tanganyika; akiwa mmoja wa Watanzania wa awali kabisa kuwa na elimu ya shahada ya kwanza (degree). Mwalimu Nyerere alimheshimu kwa elimu yake na maarifa aliyokuwa nayo.

3- Spika wa Bunge wa tatu, Pius Msekwa, hakuwa Chifu wala mbunge kama Mkwawa. Lakini wakati anaanza kuwa Spika kwenye miaka ya 1990, tayari alikuwa akionekana kama mtu anayelifahamu Bunge la Tanzania pengine kuliko yeyote mwingine. Alikuwa Katibu wa Bunge baada ya Uhuru na hivyo alikuwa kama mkunga wa taasisi hiyo kiutawala. Hakukuwa na mtu aliyekuwa na shaka juu ya umahiri wake kwenye Bunge.

4- Spika wa Bunge wa nne, Samwel Sitta, alikuwa na faida ya kuwa swahiba wa kisiasa wa Rais Jakaya Kikwete aliyeshiriki katika mapambano ya kumwingiza madarakani. Kwa sababu hiyo, Uspika wake ulikuwa na mamlaka kwa sababu alikuwa na nguvu kama swahiba wa Rais lakini pia mwanasiasa mkongwe aliyeingia bungeni miaka 30 kabla hajawa Spika.

5- Spika wa Bunge wa tano, Anne Makinda, hakuwa na ukaribu na Kikwete kama ule aliokuwa nao sita, lakini yeye alikuwa na uzoefu wa takribani miongo 40 ndani ya Bunge - akiwa ametumikia takribani mawaziri wakuu watatu - Edward Sokoine, Salim Ahmed Salim na Cleopa Msuya - kama Waziri wa Nchi (Bunge) na CCM ikimnadi kwamba ilitaka Spika wa Bunge mwenye jinsia ya kike. Hakukuwa na mwanasiasa mwanamke aliyekuwa na 'sifa' zilizotakiwa wakati ule kuwa Spika kumzidi Makinda.

Back
Top Bottom