Chezea pesa ila usicheze na mahusiano

Chezea pesa ila usicheze na mahusiano

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2018
Posts
1,403
Reaction score
2,549
Pesa ina umuhimu mkubwa sana katika kuleta mahusiano mazuri ila pesa pekee yake kamwe haiwezi dumisha mahusiano.

Jirani yangu mzee Joseph ana pesa za kutosha. Anamiliki miradi mingi sana. Kuna kipindi alikosana na mkewe mama watoto wake. Sikujua chanzo cha ugomvi ni kipi ila nilichokuja kujua ndoa yao imevunjika na mwanamke akaanza kuishi anapopajua na akawa ameshapata mwanaume mwingine. Hali ya mzee Joseph ilianza kuzorota na haikuchukua miezi minne mzee wa watu aliaga dunia.

Wapo watu mashuhuri wengi tumeshuhudia wote namna gani afya zao zilivyozorota mara baada ya kuachwa na wake zao au waume zao bila kutegemea na badae afya zao zilizolota na hawakuchukua muda wakaungana na wafu.

Usicheze na mapenzi, mapenzi yanaua. Kamwe usidhanie kuwa uliyenae hawezi kukuacha eti Kwa sababu wewe ni tajiri, ni mtu mashuhuri, umeshakuzalia watoto...usijidanganye unaweza achwa na stress zikakuua.

Jamani tuchezeeni pesa, mapenzi tuyaheshimu.

"Tumia komoni sensi"

ASANTENI
 
Unataka kutuaminisha kuwa mapenzi na pesa muhimu ni mapenzi....una matatizo wewe
 
Mleta mada nimekuelewa sana, kwa mfano tu Melaine Trump aamue kuondoka Donald ata shake vibaya mno.
Sana tu...stress za kuachwa ni mbaya sana. Ndio maana kina wenhgne akiona dalili za kuachwa huamua kumuacha mapema ili asionekane kaachwa.

Yaweza kuwa isingekuwa Zama kumuacha muongoza njia labda hadi Leo angekuwepo. Au yaweza kuwa Zari asingemuacha Ivan yaweza kuwa hadi Leo angekuwepo. Stress zinashusha sana kinga ya mwili.

"Tumia komoni sensi"
 
Yani anahela akashindwa kwenda kutafuta mtoto mbichi wa kula nae maisha!
 
Me mwenyewe ni mfano hai wa scenario hiyo.

Hakika sitosahau yalionikuta 10 years back. I swear niliyumba vibaya mno!! Mambo yangu mengi sana yaliharibika vibaya mno.......

Haya mapenzi jamani, tuyaache tu kama yaliyo. Kikubwa tumtangulize tu Mungu, katika maisha yetu.
 
Sana tu...stress za kuachwa ni mbaya sana. Ndio maana kina wenhgne akiona dalili za kuachwa huamua kumuacha mapema ili asionekane kaachwa.

Yaweza kuwa isingekuwa Zama kumuacha muongoza njia labda hadi Leo angekuwepo. Au yaweza kuwa Zari asingemuacha Ivan yaweza kuwa hadi Leo angekuwepo. Stress zinashusha sana kinga ya mwili.

"Tumia komoni sensi"
Hili za Zari linasikitisha mno hata mwenyewe ninadhani linamtesa sana.

Hata lile la Zama kumbe kiongozi alijenga nyumba wayaanze pamoja.
 
Labda kwa waume matajiri lakini sio mume mlevi anaweza mwambia mke wake wa miaka 40 nilikuwa na genye tu ndio maana nikakuowa. Kwendaaaa zako huko na lisula lako baya😁

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Pesa ina umuhimu mkubwa sana katika kuleta mahusiano mazuri ila pesa pekee yake kamwe haiwezi dumisha mahusiano.

Jirani yangu mzee Joseph ana pesa za kutosha. Anamiliki miradi mingi sana. Kuna kipindi alikosana na mkewe mama watoto wake. Sikujua chanzo cha ugomvi ni kipi ila nilichokuja kujua ndoa yao imevunjika na mwanamke akaanza kuishi anapopajua na akawa ameshapata mwanaume mwingine. Hali ya mzee Joseph ilianza kuzorota na haikuchukua miezi minne mzee wa watu aliaga dunia.

Wapo watu mashuhuri wengi tumeshuhudia wote namna gani afya zao zilivyozolota mara baada ya kuachwa na wake zao au waume zao bila kutegemea na badae afya zao zilizolota na hawakuchukua muda wakaungana na wafu.

Usicheze na mapenzi, mapenzi yanaua. Kamwe usidhanie kuwa uliyenae hawezi kukuacha eti Kwa sababu wewe ni tajiri, ni mtu mashuhuri, umeshakuzalia watoto...usijidanganye unaweza achwa na stress zikakuua.

Jamani tuchezeeni pesa, mapenzi tuyaheshimu.

"Tumia komoni sensi"

ASANTENI
Ndoa ya watu wawili, wewe chanzo cha ugomvi unajua ama ulijua ni nini? Unajua kwanini alimuacha? Na unajuaje
 
Ndoa ya watu wawili, wewe chanzo cha ugomvi unajua ama ulijua ni nini? Unajua kwanini alimuacha? Na unajuaje
Chanzo cha ugomvi sikujua ila kuachwa kwao nilijua.
Kuna jingine?

"Tumia komoni sensi"
 
Back
Top Bottom