Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 61,023
- 36,865
Tutagawana mali maana nina cheti cha ndoa. Pambana umbane mfunge ndoa ili hata akikuacha mgawane mali. Umewahi kuzisikia hizi kauli bila shaka.
Hizi ni kauli na mawazo ambayo wanawake na wazazi wengi wako nayo kichwani na vinywani mwao.
Leo wacha niwaambie ukweli mchungu. Cheti cha ndoa pekee sio automatic guarantee inayokupa umiliki wa sehemu ya mali za mumeo.
Wewe kuolewa na kuwa mke haikufanyi kuwa mmiliki mwenza au shareholder wa mali za mumeo.
Ndoa ni ushahidi wa uhusiano wa mume na mke.
Umiliki wa mali unadhibitishwa na nyaraka.
Kama uliolewa na ukamkuta mumeo anamiliki nyumba, anamiliki biashara, anamiliki mashamba, anamiliki viwanja, anamiliki ukwasi wa pesa benki kwa kifupi ulikuta anamiliki uchumi siku mkatengana au akafa mahakama HAIWEZI kuamuru mgawane hizo mali na HAIWEZI kukurithisha hizo mali kwa sababu tu una cheti cha ndoa. Narudia tena Cheti cha ndoa sio hati ya umiliki wa mali.
Kama ardhi, nyumba, mali au fedha ziko kwa jina la mumeo peke yake, mahakama haitoamuru mgawane hivyo vitu kwa sababu tu umeolewa na una cheti cha ndoa.
Mahakama itaamuru mgawane mali mlizochuma wote kwa ushahidi wa nyaraka si ushahidi wa maneno na hisia.
Mahakama haziendeshwi kwa hisia au kwa kukuonea huruma.
Mahakama zinaendeshwa na Sheria.
Mahakama inatazama nyaraka za umiliki.
Mahakama inatazama umiliki wa mali husika ulianza lini na wewe uliolewa lini? Na wewe ulipoolewa ulichangia nini au kiasi gani kwa nyaraka zipi?
Hii ndio sababu wewe kama MKE unafaa kuwa makini sana
Mkinunua mali au ukinunua mali Sheria inakutaka uiandike kwa jina lako au muiandike kwa majina yenu mawili.
Usiweke hisia na mapenzi katika mali ndani ya ndoa. Kuna kesho nyingi usizozijua zitakazokuja. Ni kweli leo mnaitana honey lakini kesho mnaweza itana mbwa au takataka.
Sheria haihukumu kwa kusikiliza story bali kwa kusikiliza ushahidi.
Ni kweli leo mnapendana sana na kila mmoja wenu hararajii kuwa kuna siku mtachukiana kiwango cha kuachana na kila mmoja kushika njia yake.
Ni upofu wa mapenzi tu unaoleta hisia za ujinga. Hata walioachana na hata kuuana kuna wakati walipendana sana hata kuwazidi ninyi. Acha kujidanganya.
Ni vizuri kupendana na kuaminiana lakini usisahau kuwa tunaumizwa na tuliowapenda sana na kuwaamini sana.
Wakati mzuri wa kujiandaa na vita ni wakati wa AMANI. Na wakati mzuri wa kujihami kwa ajili ya mapambano ya kisheria mahakamani kuisaka HAKI yako ni wakati huu mnaoitana sweetie 🥰. Tumia fursa hiyo kuweka nyaraka zako sawa.
Nasisitiza kama umenunua kiwanja chako ama chagua kuandika jina lako au jina lako na la mume wako. Wewe ukishapewa busu muache aandike majina yake peke yake kwa sababu tu una cheti cha ndoa. Utajifunza kupitia njia ngumu. Utakuwa somo na ushuhuda kwa wengine.
Mapenzi ni mazuri na ni matamu kweli. Ndoa ni tamu pia.
Lakini ukiwa na nyaraka zonazokulinda, kukukinga na kukutetea ni nzuri zaidi.
Ushauri wangu kwa wanawake, kuwa na nyaraka zinazokulinda kisheria ndani ya ndoa huku ukiwa unampenda na kumlinda mumeo.
Mwenyekiti nasemaje, Mumeo anaweza kuwa hana shida na anakupenda kweli lakini umewahi kujiuliza vipi akafariki? Je ndugu zake watasimama na wewe au watasimama kinyume chako? Itoshe kusema cheti cha ndoa sio hati miliki ya mali za mumeo.
Unaweza kupuuza hekima hii ya Mwenyekiti lakini kamwe huwezi kukwepa madhara na gharama za kupuuza hekima hii adimu na adhimu kutoka kwa Mwenyekiti.
Nasema uongo ndugu zangu?