utendaji kazi wetu Tanzania ni wa ajabu sana na huu msingi uko tokea mashuleni
yule mtu ambaye alikuwa yeye anajibu maswali sana tulikuwa tunamuita msongo mara tunamuita kiherehere tabia hii hii tumekuja nayo makazini mtu akifanya kazi yake kwa umakini, umaridadi akiwa anaifanya kwa kuipenda kazi yake sie tunamuita anataka sifa mara oooh anataka cheo... ndio maana vita ya kuwapiku wakenya kwa kuongoza kiuchumi East Africa ni kubwa sana ... kwa aina ya askari (wafanyakazi/watanzania) tuliokuwa nao
Huyo askari matendo yake yanafanana na mmoja nilimkuta pale mataa ya Stanbic Ali Hassan Mwinyi road, aisee tulienjoy abiria wote, mara ainame, mara aoneshe ishara ya muda kwamba madereva wafanye fasta, mara atembee kisharobaro yaani tabu tupu.