SoC03 Cheo cha Katibu Tarafa kifutwe

Stories of Change - 2023 Competition

cilla

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
369
296
Cheo cha Katibu Tarafa kifutwe

Kama tunavyofahamu kwa mujibu wa Mwongozo wa Uwajibikaji wa Maafisa Tarafa katika Wilaya na Halmashauri za Serikali za Mitaa wa tarehe 18 Desemba, 2003 pamoja na Sheria iliyofanyia marekebisho Sheria za Serikali za Mitaa namba 13 ya mwaka 2006 Majukumu ya Afisa Tarafa ni kama ifuatavyo:-​
  • Kumwakilisha Mkuu wa Wilaya katika kutekeleza shughuli za serikali katika Tarafa;
  • Kuandaa na kusimamia taarifa au habari kuhusu ulinzi na usalama katika kata zilizomo ndani ya Tarafa na kuziwasilisha kwa Mkuu wa wilaya na kwa Mkurugenzi;
  • Kusimamia utekelezaji wa maamuzi na Sera za Serikali kuu ndani ya Tarafa;
  • Kuelimisha na kuwahimiza wakazi ndani ya Tarafa kushiriki katika shughuli za maendeleo;
  • Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na wakazi ndani ya Tarafa; • Kushughulikia malalamiko ya wakazi ndani ya Tarafa;
  • Kuandaa taarifa ya utekelezaji ya Tarafa na kuiwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya;
  • Kuratibu shughuli zote zinazohusu majanga na dharura ndani ya Tarafa;
  • Kushiriki kama mjumbe kwenye vikao vya Kamati ya Maendeleo ya Wilaya DCC;
  • Kumwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri na Katibu Tawala wa Wilaya katika kusimamia maendeleo ya eneo lake;
  • Kuandaa ratiba ya kazi yake ili kuonyesha majukumu na muda wa utekelezaji ili kuondoa mgongano wa majukumu unaoweza kutokea kutokana na maagizo mbalimbali ya ngazi za juu na kuziwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya/Katibu Tawala wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji;
  • Kusimamia utendaji wa shughuli za Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji katika eneo lake;
  • Kushiriki na kutoa ushauri kuhusu Upangaji wa Mipango ya Maendeleo katika eneo lake;
  • ratiba ya kazi za Maafisa Watendaji Kata wa eneo lake na kuiwasilisha kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji na kwa Mkuu wa Wilaya/Katibu Tawala wa Wilaya;
  • Kuhudhuria Mikutano ya Baraza la Madiwani la Halmashauri na kutoa ushauri pamoja na taarifa za utekelezaji wa shughuli zilizofanyika katika eneo lake;
  • Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake kama zitakavyopokelewa kutoka kwa Watendaji wa Kata na Vijiji na kuziwasilisha kwa Mkurugenzi wa Halmashauri na nakala kwa Mkuu wa Wilaya/Katibu Tawala wa Wilaya;
  • Kuwa Katibu wa vikao vitakavyowahusisha Watendaji Kata, Madiwani na Wataalam waliopo katika eneo lake;
  • Kusimamia utekelezaji wa sheria ndogo za Halmashauri;
  • Kufanya kazi nyingine kama atakavyoagizwa na Mkuu wa Wilaya.
HOJA
1. Eneo la utawala kwa ngazi ya tarafa ni eneo kubwa wakati mwingine ni nusu au robo tatu ya wilaya nzima. Kwa uhalisia wa majukumu ya katibu tarafa ni wazi kabisa anawategemea watendaji kata kwa taarifa usimamizi na utekelezaji wa masuala yote yanayohusu serikali kwa sabababu watendaji wao ndio wenye vyombo vyote vya utendaji kama maafisa afya, maafisa kilimo nk. Katibu tarafa anapokea taarifa kama ambavyo anapokea mkurugenzi na mkuu wa wilaya.katibu tarafa hana vyombo vinavyo msaidia kufanya ufuatiliaji kwa ngazi ya tarafa isipokuwa anawategemea wataalamu waliopo chini ya mtendaji kata.Katibu tarafa kwa namna majukumu yao yalivyo huyu ni kama kiunganishi tu asiye na madhara.

Sioni athari yoyote kukutokuwa na kiongozi wa ngazi ya tarafa kwasababu bado watendaji kata wanawajibika moja kwa moja wakurugenzi na wanatuma taarifa kwa mkuu wa wilaya japo kuwa taarifa baadhi zinapita kwa afisa taarafa lakini afisa tarafa ni kama mtu anayezikusanya tu nakuzituma kwa mkuu wa wilaya (rejea hapa
Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake kama zitakavyopokelewa kutoka kwa Watendaji wa Kata na Vijiji na kuziwasilisha kwa Mkurugenzi wa Halmashauri na nakala kwa Mkuu wa Wilaya/Katibu Tawala wa Wilaya;
).

Badala ya kuwa na makatibu tarafa zaidi ya mmoja katika wilaya/halmashauri zetu, tutengeneze nafasi moja kwa mkuu wa wilaya ya mtu ambaye atawajibika chini yake kama msaidizi wake ambaye anaweza akawa anakaimu nafasi yake anapokuwa hayupo lakini akawa na uwezo wakumuwakilisha mkuu wa wilaya na kufanya kazi kwa niaba yake, kama kusikiliza kero za wananchi ofisini nakuzifanyia kazi na kuratibu mambo yahusuyo kata.Wakuu wa wilaya na wakurugenzi wana kazi nyingi zakusikiliza na kutatua changamoto za wananchi kwanini isiundwe nafasi ya mtu mwingine wakumsaidia kuliko kuwa na makatibu tarafa wengi ambao hatuoni uwajibikaji wao wa moja kwa moja?

2; Tunaambiwa kuwa moja ya majukumu ya katibu tarafa ni Kushughulikia malalamiko ya wakazi ndani ya Tarafa;Pia tunaambiwa kazi yake ni kuhamasisha wananchi kushiriki katika maendeleo ya tarafa.Kwa sehemu kubwa jambo hili linafanywa na mkuu wa wilaya.Ukienda kwenye ofisi za wakuu wa wilaya utakutana na wananchi wenye malalamiko mbalimbali jambo ambalo ni nadra kuliona kwa katibu tarafa.

Katibu tarafa ni kama kiunganishi tu (compiler) kati ya watendaji kata mkuu wa wilaya na mkurugenzi na ndio maana Tarafa ni sehemu tu ya utendaji katika ngazi ya Halmashauri na wala siyo ngazi ya utendaji inayotegemewa katika Serikali za Mitaa .Tunaweza tukawa na nafasi moja kama hiyo pale pale wilayani au kwa mkurugenzi ambaye atafanya kazi hizo kwa kata zote badala yakuwa na makatibu tarafa wengi katika wilaya.Kwa sasa katibu tarafa ni kama msaidizi wa ofisi au office attendant.​

MWISHO​
 
Kwenye organizational structure katibu Tarafa yupo kwenye Serikali kuu na siyo Serikali za mitaa, kwa hoja yako unamaanisha ata RAS hana majukumu mazito?.
 
Kwenye organizational structure katibu Tarafa yupo kwenye Serikali kuu na siyo Serikali za mitaa, kwa hoja yako unamaanisha ata RAS hana majukumu mazito?.
Hilo linafahamika mkuu Hoja sio muundo.kikubwa hapa tunaangalia tija yakuwa na mtu kama huyo ni nini? Structure zote zimeundwa kwa ajili yakuleta ufanisi na tija na wala sio muundo tu ili mradi na sisi tuseme tuna muundo kama mataifa mengine.Pamoja na hilo muundo pia unaweza kubadilishwa.

Shughuli ya RAS inaonekana hata kwa wananchi wenyewe tofauti na katibu tarafa.

Nchi inataka maendeleo sio structure tu uongozi usio na tija kwa wananchi.
 
Na hisi hapa pamekuchanganya kidogo: Uwajibikaji wa Maafisa Tarafa katika Wilaya na Halmashauri za Serikali za Mitaa wa tarehe 18 Desemba, 2003 pamoja na Sheria iliyofanyia marekebisho Sheria za Serikali za Mitaa namba 13 ya mwaka 2006 Majukumu ya Afisa Tarafa : hapa hatuzungumzii structure, hapa inazungumzia majukumu namna yalivyoainishwa kwa mujibu wa sheria
 
Hoja nambari 1 ina mashiko makubwa.
Sheria za kizamani zifutwe.
Nyaraka zote zinapita Wilayani, katani na mitaani/vijijini.
Tarafa haipo.
Muulize kijana wa Dar ataje tarafa 2 tu ndani ya jiji lake bila kujali wilaya. Hawezi ng'oo
 
Back
Top Bottom