sulphadoxine
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 2,257
- 649
Natumaini watakutana na Clare Short pia. Nakumbuka alikuja Tanzania na akakutana na Mkapa Dodoma ambako alimweleza kinagaubaga kwamba mpango wa kununua rada haukuwa na faida kwa nchi hii maskini kwa wakati ule. Ningekua mshauri wa bunge ningemwambia Ndugai na wenzie ni aibu kujaribu kuwaambia waingereza waipe serikali hizo hela wakati bado hatujawachukulia hatua wahusika katika kashfa hiyo. Hivi jamani huu kweli ni ujinga au ni kitu gani hiki kinacho endelea?KIKOSI cha wabunge kikiongozwa na Naibu Spika, Job Ndugai, kimesafiri kwenda jijini London, Uingereza, kukutana na Bunge la makabwela la nchi hiyo, ili kuongeza ushawishi na hatimaye mabilioni ya fedha yanayopaswa kurejeshwa nchini kutokana na ununuzi wa kitapeli wa rada, yarejeshwe serikalini.
Sakata hiyo ya rada ilimlazimu waziri wa zamani wa miundombinu, Andrew Chenge, kujiuzulu nafasi yake serikalini baada ya makachero wa Uingereza kukuta zaidi ya dola milioni 1 (bilioni 1.6) kwenye moja ya akaunti za nje za mwanasiasa huyo.
Makachero hao walizihusisha pesa hizo na tuhuma za rushwa ya rada huku Chenge mwenyewe akijitapa kuwa pesa hizo ni "vijisenti tu" kwake.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana mjini hapa, kikosi kinachoundwa na wabunge wengine takriban wanne, kitakutana na viongozi mbalimbali wa Bunge la Uingereza, ambako ndiko mzozo wa mauzo ya rada ya kijeshi ulikoanzia ukiwa na aliyekuwa Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataita wa Uingereza, Clare Short.
nalifikiri ni mimi tu nimepigwa na upofu wa kupambanua, kumbe siv yo. sijaona mahala ambapo chenge anaelekea kuingizwa matataniSijaona huo Utata uliompata Chenge
Sijaona huo Utata uliompata Chenge
Title haijatulia..Hee! Kwahyo utata kwake ni kukutana na wabunge wa uingereza au? Haisomeki.
hivi hizo fedha walizifanyeje ameachiwa?, je ameszitolea justification amezipataje au ndo yamekwisha?
hivi hizo fedha walizifanyeje ameachiwa?, je ameszitolea justification amezipataje au ndo yamekwisha?