Chenge asimikwa mtemi wa wasukuma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chenge asimikwa mtemi wa wasukuma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Wayne, Jun 16, 2009.

 1. Wayne

  Wayne JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2009
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 663
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Chenge asimikwa utemi


  na Sitta Tumma, Magu


  [​IMG]
  MBUNGE wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, ambaye amekuwa akiandamwa na kashfa mbalimbali, ametawazwa kuwa mtemi wa kabila la Wasukuma-Bagole, Kanda ya Itilima, wilayani Bariadi.
  Chenge alichaguliwa katika sherehe maarufu za kabila hilo, maarufu kama Bolabo, mwishoni mwa wiki, wilayani hapa, ambazo mbali na viongozi wa kimila, Mkuu wa Mkoa, Abbas Kandoro, alikuwa ni miongoni mwa waliohudhuria.
  Baadhi ya watu waliokuwepo kwenye sherehe hizo, waliuelezea utemi wa Chenge kwa mtazamo tofauti, huku baadhi wakidai kaupata ili kuweka mambo yake sawa, na wengine wakidai anastahili kupata nafasi hiyo kwa kuwa ni miongoni mwa watu wa kabila hilo.
  Mbunge huyo ambaye alilazimika kujiuzulu nafasi yake ya uwaziri alisema, utemi huo ni karama aliyopewa na Mungu na kwamba wajibu huo ni sawa na daraja la kuunganisha jamii ya kabila husika.
  "Utemi niliopewa naweza kusema ni karama iliyotoka kwa Mwenyezi Mungu! Kazi hii ya utemi ni nzito kwa sababu ina masuala yake yanayohusiana na mambo ya kimila pamoja na kuunganisha jamii ya kabila husika," alisema Chenge.
  Sherehe hizo za kabila la Kisukuma, zilihudhuriwa na watu maarufu akiwemo Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, Mshauri wa Watemi, Jaji Michael Bomani, Mwenyekiti wa Watemi wa Wasukuma, Kanda ya Mwanza, Charles Kafipa, mmoja wa washauri wa Watemi Bujora, Jaji Thomas Mihayo, na viongozi watemi wengine kutoka mkoani Shinyanga.


  [​IMG]
  juu[​IMG]
   
 2. Wayne

  Wayne JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2009
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 663
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Napata shida kuelewa hili suala la Mtu kupewa uongozi wa kabila lake.
  Je nini tafsiri yake?????!!!!!
  TULISHAPITA HIYO STAGE YA UKABILA...JE TUNARUDI NYUMA ......?????!!!!

  Wasiwasi wangu mkubwa upo kwa HAO WAUDHURIAJI.

  WHAT ON EARTH IS GOING ON???????????????????????????
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hapo ndio utaelewa kwamba ndani ya TZ kuna watu bado wako in the 60s, kama unabisha kawaulize nyerere wa wa sasa nani??

  Huyo chenge wangemsimika tu kila kitu... yet, he will still be the ol'dirty'ba*t***
   
 4. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2009
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wow!!!. I can't believe it. Even Judge Mark (not Michael) Bomani and Kandoro attending!

  Tanzania tunaporomoka. Au Wasukuma wanataka "vijisenti" kiasi hicho? They will be disappointed kwa vile vijisenti vitakwishia kwenye kulipia defence ktk case ya kusababisha vifo kwa careless driving inayomkabili Mtemi wao mpya.
   
  Last edited: Jun 16, 2009
 5. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Hivi haya nimeyaona kwa macho yangu au naota? yaani enhe! Wanaona kwa wananchi vijijini ndiko kwa kukimbila!?
   
 6. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,219
  Trophy Points: 280
  jamani wanadumisha mila ambazo wengine wameshindwa!wasukuma oyeeee!
   
 7. Joel

  Joel JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 908
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 80
  hawa watu wnajitahidi kutafuta kuungwa mkono na watanzania wengi sasa wanaamua kuanzia kwenye majimbo yao maaana hata mhe. Lowasa na yeye ilikuwa hivyo hivyo.
   
 8. H

  Hongasuta Member

  #8
  Jun 16, 2009
  Joined: Sep 10, 2006
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama hiyo itamsaidia lolote fisadi huyu. Na nyie Wasukuma hebu amkeni kidogo. Loh!
   
 9. shiumiti

  shiumiti JF-Expert Member

  #9
  Jun 16, 2009
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kazi kweli kweli. Mambo ya Wasukuma hao......
  Nahisi Wasukuma wanaweza kudhalilika sana kwa jambo hili...maana vigezo vya mtu kuwa mtemi naamini vimekiukwa.

  OK! MWISHO WA SIKU, PESA NDIO INAONGEA...
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Jun 16, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  "Sidhani kama hiyo itamsaidia lolote fisadi huyu. Na nyie Wasukuma hebu amkeni kidogo. Loh!"
  __________________________

  HONGASUTA:

  Ati nani aamke? Miafrika si ndivyo ilivyo? Miaka karibu 50 baada ya Kambarage kutufunua mablanketi na kutufumbua macho, bado tuanapigania kudhalilishwa tu. Inatapisha kweli kweli!

  Inashangaza hadi sasa naye RA anaogopa nini kuamrisha atawazwe mtemi wa Wanyamwezi wa Igunga. Au hamjui yeye ni mjukuu wa Humbi Ziota, aliyekuwa mtemi wa mwisho wa maeneo hayo?

  Katika utitiri wa majina yake niliyosoma kwenye gazeti anayotumia kwenye kampuni zake, nadhani kuna moja linfanana na Humbi -- HUMDI nadhani ilikuwa!
   
 11. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #11
  Jun 16, 2009
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45

  Kandoro yuko Mwanza lakini na bariadi iko Shinyanga, ama kwa sababu wasukum,a wana-cut across Mwanza na Shinyanga then iliamuliwa Kandoro ndo awepo kumwakilisha na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga?

  Je, Chenge cheo chake hicho kipya ni hadi wasukuma wa mwanza, ama????????
   
 12. Wayne

  Wayne JF-Expert Member

  #12
  Jun 16, 2009
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 663
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nani atathubutu "KIMILA" KUMNYIMA KURA MTEMI 2010?
   
 13. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #13
  Jun 16, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hivi Viongozi wetu hawaoni mafisadi hawa wanavyoturudisha kwenye utawala wa machifu/watemi/laiboni iliyofutwa miaka ya 60.Ingekuwa si uoga wa Viongozi wetu mafisadi hawa wangeshitakiwa kwa kukiuka sheria za nchi.
   
 14. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #14
  Jun 16, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mimi nampa ushauri wa bure JK kuwa asipoangalia mafisadi wanaandaa pigo kwake.Kwa vipi? ni kuwa maana ya kiongozi wa kabila fulani laiboni/mtemi/chifu ni kwamba wakati wa uchaguzi watagawa vijisenti vyao na kumuapiza kila watakayempa fedha ili wawe na uhakika wa kupigiwa kura na utaratibu huo huratibiwa na viongozi wenzake wa mila.Utaratibu huu hutumiwa sana na Viongozi wanaojiona wana hatimiliki ya kiti cha ubunge hapa TZ.
   
 15. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #15
  Jun 16, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ahsante sana ndugu yangu COUNTERPUNCH. Kwa kweli tuna kazi kubwa ya kubadilisha mindset za WADANGANYIKA. Hivi tumerogwa au?
   
 16. T

  Tujisenti JF-Expert Member

  #16
  Jun 16, 2009
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nasikia tangu Chenge apate kashfa ya Ufisadi wasukuma walikiona kama sifa au cheo kikubwa.Before alikua akienda na gari moja baada ya kashfa akasindikizwa na magari ishirini halafu kila siku yuko kwenye vyombo vya habari.Kazi kweli kweli!!!!!!!!!1
   
 17. kui

  kui JF-Expert Member

  #17
  Jun 16, 2009
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 6,478
  Likes Received: 5,146
  Trophy Points: 280
  iiiiiiii, wagosha!...
   
 18. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #18
  Jun 17, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ameamua kuwekeza kwenye Bajaj

  [​IMG]
   
 19. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  SANAHANINI WATANI ZANGU ILA HAPO WANANCHI WATAELEWA KWA NINI MTU AKIFANYAGA KITTU CHA KISHAMBA NAAAMBIWA YUKO AU ANAKUWA KAMA MSUKUMA. They are short minded. Samahani sijawatukana
   
 20. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #20
  Jun 17, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Fedha inaweza kumdhalilisha mtu yeyote mwenye njaa na umasikini. Chenge ametumia kikamilifu hali hiyo kupata utemi huo FEKI FEKi hivi.
   
Loading...