kichwamaji
JF-Expert Member
- Dec 1, 2006
- 232
- 13
Mimi naamini kabisa kama Mh.Kikwete ni msafi tena msafi wa uhakika.kama kuna wachafu basi hao walidandia basi la Mh.Kikwete na kutaka kumsaidia wakiweka matumaini kuwa atawapatia lifti ,mara nyingi wanaosaidia kusukuma gari nao hutaka msaada wa kufikishwa wendapo.
Kwa ufupi Mh.Kikwete hakuwa mwizi wa fadhila aliwapa msaada na kuwafikisha waendapo ,kama walikula dawa ili wapate nguvu za kumsaidia hilo litakuwa tatizo lao ,Mh.Kikwete hakutaka kujua jamaa walipata wapi nguvu za kulisukuma gurudumu lake la kupanda kilima cha Uraisi kwa kishindo ,yeye aliona tu kuwa gari limeshika kasi na kuondoka hivyo aliowapakia aliwasaidia kwa kuwalipa shukurani.Sasa kusema Kikwete alishinda kwa sababu wasukumaji wake walikula vidonge vya kuongezea nguvu ili waweze kulisukuma gurudumu na wao wapatiwe lifti ,hilo litawagusa hao waliotumia vidonge si kwa msukumwaji.Kawafikisha safari yao ,sasa kama waliiba fedha za kupata nguvu au hapo walipofikishwa ndipo walipokusudia kuiba ,that will be another case ,fagio la chuma likipitishwa inavyotakiwa Mh.Kikwete asiukumbuke ule wema aliotendewa kwani alikwisha walipa wema ,atimize majukumu ya Uraisi na kuangalia mbele awache sheria ichukue mkondo wake huku yeye akiwa msimamizi na kuwaeleza wasaidizi waliomsaidia kusukuma gurudumu kuwa kama angelijua ni majambazi asingeliwafikisha safari yao.
....rais hawezi kujiweka mbali na kashfa za watu wake wa karibu wa mtandao..hatuwezi kuwa na prof mukandara"s principle eti....rais wetu ni mzuri ila watendaji wabovu......ubovu wa watendaji wa kisiasa hasa mawaziri unamaanisha ubovu wa principle wao...ningeweza kukubaliana na hii principle kama rais angekuwa safi,mawaziri safi alafu watumishi wa umma ndio wawaangushe...hapa tusingemlaumu sana rais kwa kuwa watumishi ni proffessionals ambao reform yao ni process......lakini la hasha watumishi wa umma kwa kiasi kikubwa wamebadilika sana ukilinganisha na mawaziri [wanasiasa]
hii serekali itaendelea kuwa ya kuumbuana na hatua ya mwisho msalabani asulubiwe mwenyewe rais jakaya kikwete...kwa spidi hii ya kudondoka msalabani wateule wake ...ipo siku matope yatamrukia na wananchi watataka asulubiwe.....hadidhi ya mbwa mwitu ...wakila nyama atakayebakiwa na madowa ya damu...nyama ikiisha basi naye hugeuzwa kitoweo.....
Ila wakuu with all that said,, mtakumbuka kuwa alipoteuliwa mara ya pili mwezi February kinyume na matarajio ya wengi, alisema kuwa kwa wale wanaoshangaa wakamuulize aliyemteua (Mh Rais) ...sasa mi naona kama amemdalilisha sana JK katika hili!
Na pia najiulize je, kama JK alikuwa anayajua haya, assuming kuwa lishahabarishwa na RO, je alimwacha kwa makusudi aanguke mwenyewe na yeye akabaki kunawa mikono kama pilato?
Na huu msalaba ataubeba chenge peke yake au kutakuwepo na wa kumsaidia kama ilivokuwa kwa EL?
Tafadhali usimlinganishe Mh.Kikwete na tabia za Udikiteta utakuwa humtendei haki kama tunavyotamani tupate kiongozi anaefuata taratibu za kisheria na hadi hivi sasa kwa muono wangu katika kufuata sheria basi yeye anastahili pongezi,hajamfukuza mtu ,hajamkamata mtu .stili yupo kwenye uvumilivu wa hali ya juu zaidi ya yote anayobambikiwa na wapinga Ufisadi bado Kikwete hajatetereka na kupoteza mwelekeo wa Utawala.Hiyo ni haki yake apewe na tatizo mlilo nalo mnataka afuate amri zenu za yule ndie mkamate ,tawala za aina hiyo hazina nafasi katika ulimwengu wa kileo ,mambo yanakwenda stepu kwa stepu ,au hatuwa kwa hatuwa kipengee kwa kipngee sasa hata kama atamaliza muda wake na vipengee vya kufuatwa havijamaliza bado vitaendelezwa ili kutunza na kujenga utawala wa sheria ,hivi mkisikia utawala wa sheria mnafikiri kila litakalosemwa kuwa huyu na yule ni mafisadi basi wakati huo huo wakamatwe ,wacheni kukengeuka mambo ya watu ,inaonyesha wengi wenu ni wageni katika utawala wa sheria....ni vigumu sana kumtenganisha kikwete na uchafu kwa kuwa ni rais aliyetokana na mbinu chafu...kwa hiyo simply ni mchafu....ni rais mfujaji wa pesa zetu walipa kodi kwa starehe..hata kama hachukui kama wenzake ...ni rais mwenye kiwango kidogo cha uelewa na usimamizi wa serikali yake...hafai!!!!
Kasheshe, kati ya wabunge wote waliochaguliwa na wananchi, kwanini alimchagua Chenge kwenye baraza lake mara mbili.
Phillemon Mikael, wewe umemkazania JK, JK hawezi kutoka mpaka 2010.
In the meantime, since yeye ndio kashika mpini, ni vizuri kudeal na mafisadi ambao JK anaweza kuwabwaga au hata kuwashitaki mahakamani akiamua.
Ikifika 2010, then ndio uanze lawama nzito ili labda akose.
EM
Tafadhali usimlinganishe Mh.Kikwete na tabia za Udikiteta utakuwa humtendei haki kama tunavyotamani tupate kiongozi anaefuata taratibu za kisheria na hadi hivi sasa kwa muono wangu katika kufuata sheria basi yeye anastahili pongezi,hajamfukuza mtu ,hajamkamata mtu .stili yupo kwenye uvumilivu wa hali ya juu zaidi ya yote anayobambikiwa na wapinga Ufisadi bado Kikwete hajatetereka na kupoteza mwelekeo wa Utawala.Hiyo ni haki yake apewe na tatizo mlilo nalo mnataka afuate amri zenu za yule ndie mkamate ,tawala za aina hiyo hazina nafasi katika ulimwengu wa kileo ,mambo yanakwenda stepu kwa stepu ,au hatuwa kwa hatuwa kipengee kwa kipngee sasa hata kama atamaliza muda wake na vipengee vya kufuatwa havijamaliza bado vitaendelezwa ili kutunza na kujenga utawala wa sheria ,hivi mkisikia utawala wa sheria mnafikiri kila litakalosemwa kuwa huyu na yule ni mafisadi basi wakati huo huo wakamatwe ,wacheni kukengeuka mambo ya watu ,inaonyesha wengi wenu ni wageni katika utawala wa sheria.
Kama mpo mnaoishi Marekani au nchi za ulaya mnaona utawala wa sheria ulivyoshika kasi ,una hiari yako kwenda kwa mguu au kupanda gari ya polisi ,una hiari yako kumruhusu polisi aingie ndani kwako kupekuwa au asubiri asubuhi.
Hapo ndipo tunapoelekea na hatutafika ikiwa tutamfanya Raisi aanze kuwakamata watu wote wanaoonekana ni mafisadi kwani akianza hivyo habaki mtu mimi na wewe pia itabidi tukamatwe.Hawa MaCUF na maupinzani wanaomtaka Kikwete awawajibishe wahusika wa ufisadi hawamtakii heri na hawaitakii heri Tanzania ,wao na kujua kwao kote wameona wapi wahusika wa wizi namna hii katika nchi zilizoendelea au huko maulaya wakikamatwa hovyo hovyo kwa habari za magazeti na wapinzani ,ukichukulia Tanzania ndio kwanza tunataka kujenga utawala unaofuatilia sheria ,huko utamsikia mtu kajiuzulu pengine amepelekwa sms tu kuwa unahusika na wizi fulani basi hapo limeshakua jambo la kujiuzulu na wala hangojei kufanywe uchunguzi lakini hapa kwetu Tanzania ndio kwanza tupo kwenye dalasa la vidudu ,mnataka tuanze kusoma vitabu vya dalasa la saba.
Wacheni ufanywe uchunguzi kwa kituo maana kwa nionavyo hata walioko kwenye upinzani basi hawatoki wataingia tu maana watu ndio hawa hawa tokea kwa Nyerere ,kumbukeni tu kuna watu walishiliki kwenye vita na Hitler na walihusika kwa ufisadi wa roho za watu na leo wakipatikana na hatia wanakwenda gerezani ,kuna akina Mrema ,Lipumba ,Sefu ,Mbowe na wengine ambao walikuwemo CCM wakaondoka na wengine wamerudi sasa ikianza kamata kamata mnayoitaka basi hata wapinzani wataathirika na kubaki midomo wazi kwa wafuasi.
Narudia kwa mara nyingine tena, Mheshimiwa JK ni mtu mzuri na ana ubinadamu. Shida na maswali yetu ni kuhusu Uwezo wake wa kupambanua baya na jema tu.
Kule Marekani alikuwepo president aliyeitwa 'Warren G. Harding' ambaye alichaguliwa mwaka 1920 kwa kura za asilimia 61 (popular vote) na 'electoral college of 404' kati ya 531. Ushindi huu ulikuwa ni ushindi wa kishindo kama alioupata rais wetu Kikwete; na hadi sasa hakuna president mwingine yeyote wa Marekani amewahi kupata ushindi kama huo..
Lakini leo hii ukimuuliza Mmarekani mitaani anayemkumbuka rais huyo itakuwa shida kumpata! Na ranking zote za ma-rais wa Marecan huwa anakuwa wa mwisho kabisa.
Harding alikuwa ni mtu mzuri, mnyenyekevu na mpenda watu. Historia yao inasema hakutaka kumuudhi yeyote, na hakutaka kumwambia mtu yeyote aliyemwendea kwa msaada, HAPANA. Na hakupenda kufanya maamuzi yoyote yaliyokuwa mazito; kiasi kwamba ilimuwia vigumu hata kuamua kama Marekani iwe mwanachama wa 'League' of nations.
"He played it safe," kiasi kwamba baba yake mzazi alisikika akisema kwamba alikuwa na bahati kwa vile Harding hakuzaliwa akiwa msichana, kwani asingeweza kusema HAPANA kwa wote waliomtaka kimapenzi!
Kuna viashiria vinavyomfananisha Kikwete na huyu Mmarekani wa miaka ya 1920s
Hili sio tatizo la JK!!! Ni tatizo la kitafa...
Kuwa makini kidogo, Sio kila kitu ni cha Rais vingine ni vya jamii nzima tuliyonanyo!!! sasa imebadilika... lazima tuelewe hivyo... Na JK anatuongoza vyema kwenye mabadiliko haya kwa kukubali wanaojiuzulu wajiuzulu...
- Nani alimchagua Chenge kuwa Mbunge ambayo ndiyo sifa no.1 ya kuchaguliwa kuwa waziri?
- Nani alimchagua Chenge kuwa mjumbe wa NEC ya CCM? JK au wanaCCM?
Narudia kwa mara nyingine tena, Mheshimiwa JK ni mtu mzuri na ana ubinadamu. Shida na maswali yetu ni kuhusu Uwezo wake wa kupambanua baya na jema tu.
Kwenye ile thread ya baraza jpya la mawaziri nilijiuliza sana kuhusu "competency ya mkuu wetu wa kaya" linapokuja suala la kuamua Nani awe waziri katika nchi ya Tanzania yenye watu takribani 38,000,000!! Niliijihoji sana vigezo gani mkuu anatumia kuamua watu wa kumsaidia kazi za kujenga nchi na kulinda watanzania.
Mheshimiwa Chenge (napata shida sana kumuita mheshimiwa, I wish na ubunge aachie)ni mtu ailiye katika FIRST ELEVEN ya Mkuu wa kaya sababu Baada ya mheshimiwa kupata 2nd chance ya kusafisha baraza aliona kuwa Katika hao raia 38M hakuna mchezaji kama Chenge. Piga ua jamaa hakukosa namba. Matokeo ya mechi kwa dakika hizi 10 za mwanzo yananifanya nihisi kuwa Mkuu wa kaya kaishiwa wachezaje. Sioni kama atakuwa na mtu wa kufaa kwenye cabinet hata kwenye benchi la wachezaji wa akiba.
Well, asikate tamaa, hii ni nafasi yake nyingine kusafisha baraza. nafasi ya dhahabu kuepuka fedheha zaidi kama hizi. Heri lawama kuliko fedheha. hatakiwi kuangalia watu usoni katika kuamua nani awe waziri. Watu wa kuangalia usoni ni watanzania wanaoumia kwa dhambi za kina Chenge, Lowasa, Karamagi, Rostam Aziz, Mkapa, Yona, na kadhalika wengi.
UShauri wangu ni kuwa aweke watu ambao hatawaogopa kuwafuta kazi wakiharibu
Labda pia nikurudishie swali?
1. Vigezo vya kumchagua mtu kuwa waziri ni pamoja na representation ya mikoa, kand, na vingine vingi. vya kisiasa... etc. "please don't tell me kupigiwa makelele ni lazima uyasikie hata kama huna ushahid" vitu vingine vinajileta vyenyewe kama ilivyojileta hivi..
2. Wataka kuniambia JK alijua jamaa ana hizo billion huko nje?
3. Kwa hakika ni mpaka kitu kidhibitike ndio unaweza kum-jurge mtu kwa haki zaidi ya hapo ni majungu...
4. Jaribu kujua tatizo linatoka wapi... acheni kuangalia matokea ya tatizo fulani?
Tendeni haki kwenye ku-jaji mambo... Na wakati wa kumpungeza JK kwenye ku-support mapinduzi na mabadiliko haya ya kisiasa... tatizo lenu mnataka asimame aseme so and so... I have fired you... sio lazima hivyo... taratibu tunaenda... lakini tusijisahau bado kwamba adui wetu mkubwa ni kutofanya kazi kwa maarifa na kwa jitihada.
Tafadhali usimlinganishe Mh.Kikwete na tabia za Udikiteta utakuwa humtendei haki kama tunavyotamani tupate kiongozi anaefuata taratibu za kisheria na hadi hivi sasa kwa muono wangu katika kufuata sheria basi yeye anastahili pongezi,.................. ,hivi mkisikia utawala wa sheria mnafikiri kila litakalosemwa kuwa huyu na yule ni mafisadi basi wakati huo huo wakamatwe ,wacheni kukengeuka mambo ya watu ,inaonyesha wengi wenu ni wageni katika utawala wa sheria.
Kama mpo mnaoishi Marekani au nchi za ulaya mnaona utawala wa sheria ulivyoshika kasi ,una hiari yako kwenda kwa mguu au kupanda gari ya polisi ,una hiari yako kumruhusu polisi aingie ndani kwako kupekuwa au asubiri asubuhi.
Hapo ndipo tunapoelekea na hatutafika ikiwa tutamfanya Raisi aanze kuwakamata watu wote wanaoonekana ni mafisadi
utawala wa sheria anaofuata huyu jakaya ni upi....ni pamoja na kuingilia uhuru wa mahakama kumnusuru rafiki yake asishitakiwe kwa mauaji...huku ndugu zao wakiparamia mlango wa majaji kwenda kumtoa kwa kejeli za ukubwa!!!!......
...rais kuchelea kuchukua hatua kwenye baadhi ya mambo ni uzembe wake wa kutaka kila kitu kukifanya political agenda...aliposema waagizaji wa madawa ya kulevya anayo majina alihitaji utaratibu gani....kama si kuwa alikurupuka kutangaza kabla ya kuwa tayari....au pia ni mwaga ...anawaogopa!!!..AMIRI JESHI MWOGA???
ALIPOSEMA ANA MAJINA YA MAFISADI NA MAJAMBAZI na hadi leo hakuna wanaofikishwa mahakamani zaidi ya kubembelezwa warudishe pesa ....je ndivyo sheria ya nchi na katiba inavyosema ...ndio utaratibu wa kawaida wa kushughulikia wahalifu???
ni utawala upi wa sheria anaofuata jakaya zaidi ya kukurupuka kama mrema ??? wanasheria tusaidieni!!
Jamani eeeh! pamoja na makosa yote ya Kikwete lakini inabidi tumpe hongera kwa hili moja kubwa zaidi..FREEDOM of PRESS!
Kama kweli angetaka kutubana kama alivyofanya Mkapa tusingeweza kuona hata moja hapa likitokea kwani jamani kumbukeni tumetoka mbali sana.
Ukitazama kwa makini maswala mengi hapa yametokea wakati wa Mkapa na wakati ulew tulinyimwa hata Pumzi na kuitwa wajinga!
Pengine yawezekana yote hii ni mchezo anaoucheza Kikwete kuhakikisha anaondoa wote mabaki ya Mkapa ambao aliwaahidi kuendelea na ufisadi bu he had a way to stop all these through Media na Wananchi...
Kuna habari za kusadikika kuwa hata lile zengwe la Invinsible aliingilia kati na kumwambia mkuu wa Usalama kuomba samahani...sina Uhakika na habari hizo, yet zimetuongezea nguvu sana ktk nyanja zote za utafutaji haki. Siku hizi hata maandamano yanakuwa hayana migogoro tena. What if nitarudia what if all this was his plan coming 2010... Mafisadi wote nje?..
Hizo habari za kuchukua fedha Iran na kuendesha uchaguzi sidhani kama ni haramu maadam tufahamu hao Wairan wamepata kipi in exchange.. Lobbyists ktk siasa wapo karibu dunia nzima -inakubalika. Na ukitazama hasa nchi zetu za kiafrica mara zote hawa jamaa hutoka nchi za nje waki represent interest za nchi zao ama organization zao. Tumekuwa na Iran toka enzi ya mwalimu wakati Ayatollah akichukiwa dunia nzima!..
Muhimu ni kufahamu hizo fedha zinahusiana vipi na Ufisadi unaotendeka, mathlan kampuni fulani ya Iran imepewa nafuu fulani ya kodi ama ku monopoly biashara fulani bila mshindani. Pia tukumbuke tu wakati wa uchaguzi mkuu uliopita hata mchezo mchafu wa Takrima ilikuwa halali..
Nje ya hapo nambieni kwa kituo Ufisadi wa Kikwete, kwani nafahamu uzembe na Upuuzi wake ambao hauna tofauti na Wadanganyika wengi kati yetu sisi wenyewe.