'ChemChem' ya Pesa Mkoani Ruvuma Yavuta Wengi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'ChemChem' ya Pesa Mkoani Ruvuma Yavuta Wengi

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Apr 20, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  WAKAZI wa wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wamekuwa wakikesha wilayani humo usiku na mchana wakisubiria pesa zinazotoka chini ya mti mithili ya chemchem. Baadhi ya Wakazi wa mji huo inasemekana waligundua maajabu hayo kwenye mti huo na baada ya wakazi hao kuanza kujizolea pesa toka kwenye mti huo habari ghafla zilisambaa mkoani Ruvuma kuwa kuna mti una chemchem ya pesa.

  Ilidaiwa kuwa wakazi hao walipokuwa wakipita chini ya mti huo waliona pesa zikitoka chini ya mti na pamoja na kustaajabishwa na tukio hilo wakazi hao waliamua kuzichukua pesa hizo.

  Taarifa zaidi zilisema kwamba kwa muda wa siku mbili mfulululizo wakazi wa wilaya ya Songea waliendelea kuziokota pesa zilizokuwa zikitoka kwenye mti huo.

  Pesa hizo inadaiwa zilikuwa zikitoka mithili ya chemchem zikiwa ni noti tofauti tofauti zikiwemo na noti za shilingi elfu kumi, tano na kadhalika.

  Baadhi ya watoto waliowahi kuhojiwa na mwakilishi wetu wa nifahamishe kutoka eneo la tukio, watoto hao walidai kuwa walishajizolea pesa hizo na walizipeleka kwa wazazi wao nyumbani.

  Walidai kuwa pesa hizo zilikuwa zikitoka chini ya ardhi na mamia ya watu toka sehemu mbalimbali za mkoani Ruvuma walikuwa wakizigombania kila zilipoanza kuchomoza.

  Watu wazima waliohojiwa na Nifahamishe nao pia walithibitisha kujizolea noti hizo zilizodaiwa kutoka kwenye chemchem hiyo.

  Kwa kuwa pesa pesa hizo zilikuwa zinatumia muda mrefu kutoka kwenye chemchem hiyo, maelfu ya watu kutoka wilaya tofauti wamekuwa wakiweka kambi eneo hilo kusubiria pesa hizo.

  Tukio hilo limethibitishwa na polisi mkoani humo na walisema wanafanya uchunguzi wa kina kubaini kuwa pesa hizo zinakuwa zinatoka wapi.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=4369814&&Cat=1
   
 2. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2010
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hayo yanatokea kwenye nchi ya kusadikika kama Tanzania peke yake. Totally nonsense! Pesa za bure, kweli kabisa! bila kufanya kazi? You gotta be kidding!
  Na hayo mapesa yamo kwenye Currency ya wapi, ya Tanzania? Ningekuwa kiongozi wa serikali ningeenda kustop huo ujinga. Watu wameacha kazi zao za kulima eti wanenda kusubiri pesa za bure.
  Sijui tulilogwa na nani?
   
 3. B

  Bibi Kizee JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2010
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 213
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hahaahaaa! toka wameanza kukesha chemchem inaendelea kumwaga pesa au imegoma?
   
 4. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  mjinga huamini kila alionalo na kulisikia, bali mwelevu huangalia sana aendako
   
 5. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Nashangaa kuona waandishi wa habari wanaandika habari za UONGO na kudanganya kuwa wameongea na wananchi kumbe ni uwongo mtupu. Aliyeandika hiyo habari ni MUONGO. Tukio hilo lilitokea kwa namna tofauti kabisa na jinsi lilivyoandikwa na mwandishi huyo. Pesa zilizookotwa siyo mapesa ni noti za mia tano elfu moja na chache za elfu tano na elfu kumi. Hazikuwa zinatoka kama chemchem, zilikuwa zinaonekana tu kama mtu anavyookota pesa barabarani, wala haikuwa kwenye mti bali ilikuwa kwenye uwanja wa nyumba isiyokamilika kujengwa katika mtaa wa bombambili. Kitu kinachofanya tukio lionekane la ajabu ni kwamba: pamoja na watu kuokota pesa hizo, ndani ya dkika chache zilionekana tena nyingine na kuokotwa! hili tukio si rahisi kulielezea, ila lilitukia katika hali ya ajabu kidogo.
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180

  Hawa ndo waandishi wetu. Habari tofauti na tukio lilivyojiri
   
Loading...