Chemba ya majitaka round about ya Mwenge kuelekea TRA jirani na Mwenge Sokoni ni kero kubwa sana

Dullah07

JF-Expert Member
Apr 12, 2017
220
473
Kwakweli hii chemba imekuwa kero sana kwa watumiaji wa hiyo njia kwani mara kwa mara inazidiwa uwezo na kupelekea maji taka kutoka katika mfuniko wake na kusambaa katika barabara na kuleta kero kubwa na hatari ya kupata magonjwa ya mlipuko kwani maji yenyewe ni meusi na yananuka sana ukizingatia hayo maeneo watu wanauza matunda na vyakula mbalimbali.

Kuna kipindi kama miezi kadhaa iliyopita nilikuta ile chemba imefumuliwa nkasema yes sasa hapa nadhani haitokuja kufurika tena lakini wapi leo napita nakuta maji taka yamezagaa na yanatoka kwa presha hayo utafikiri ng'ombe kachimbwa hakika mamlaka husika hili mliangalie tena kwa jicho la tatu kwani mtu unajiskia hata kinyaa kutumia njia hiyo.
 
Back
Top Bottom