Kuna rafiki yangu mmoja mshabiki wa Man United. Anaipenda mno timu hii. Hataki kuambiwa chochote kibaya kuhusu Man U. Na ndivyo tulivyo mashabiki wengi duniani, tunapenda kujipa matumaini sana hata mahali matumaini yanapopotea waziwazi.
Nilimwambia mwanzoni wa mwezi mwishoni wa mwezi Oktoba 2013 kuwa hakuna namna yoyote Man U inaweza kutwaa ubingwa mbele ya Man City, Chelsea, Arsenal na Liverpool. Alibisha sana sasa hivi anaona aibu. Na ndivyo napenda kuwajulisha mashabiki wa Arsenal, hakuna namna yoyote Arsenal hii inaweza kuwa bingwa wa EPL msimu huu mbele ya Liverpool, Man City na Chelsea. Kataeni, nuneni, tukaneni lakini Arsenal ina nafasi ndogo sana ya kuwa bingwa msimu huu. Na sababu ni ndogo tu. Uwezekano wa Arsenal kuchukua alama tatu tatu kutoka Chelsea, Man City na Liverpool ni mdogo kuliko timu hizi kuchukua alama kutoka kwake.
Kwa hiyo, Man City ina nafasi kubwa zaidi ya kuchukua ubingwa, na chelsea inafuatia kwa karibu zaidi.
Kama mambo yatakwenda kama yalivyo, mtazamo wangu mimi mwishoni wa msimu kuna uwezekano mkubwa wa msimamo wa EPL ukawa:
1. Man City 80%
2. Chelsea 78%
3. Liverpool 65%
4. Arsenal 62%
5. Totenham 50%
6: Man United 50%