Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Ndugu zangu wa Chelsea niliwaambia ushindi kwetu ulikuwa lazima; wanasema hatuna "mastraika" wakali, ni kweli mastraika wetu ni kwa ajili ya timu kongwe:

Man United = timu kongwe; Chelsea Fc timu bora.:boxing:
 
Claudio Makelele hayupo Chelsea alikwenda PSG France na kwasasa atakua katundika daruga juu kutokana na umri!

jamani mpenzi wangu kumbe alikuwa mzee tayari ila ana minguvu... drogba yupo wapi na kaka?
 
Drogba nae yuko Garatasaray ya Uturuki na Recardo Kaka yuko Real Madrid.

Karibu the Blues uwe shabiki wetu kabisa!

Kuna wachezaji wengi wazuri utawapenda tu na wanacheza mpira Km Makelele.

nani ananguvu kama makelele?
 
nani ananguvu kama makelele?


Kuna viungo wenye ngozi nyeusi mmoja ni mnigeria anaitwa John Mikel Obi Huyu ana nguvu sn tena ukienda hovyo Lazima uning'inie na mwingine Ramires Huyu ni mbrasil ana mwili Wa kawaida lkn king'ang'anizi huyo vibaya! Yani adhibiti mijitu mikubwa sn Km mikina Yaya Toure!

Karibu sn uwe unafatilia game zetu Najua utaipenda tu Chelsea na rangi yetu ya Blue!
 

naipenda chelsea sana ila tu si mtaalamu mzuri wa mpira zaidi ya chenga, faulo, na penati na kanzu sijui tena
 
tufunge
tufungwe
tu-droo

nitakua a man U fan....forever united..
uone Mentor
 
Last edited by a moderator:
naipenda chelsea sana ila tu si mtaalamu mzuri wa mpira zaidi ya chenga, faulo, na penati na kanzu sijui tena



Basi Kumbe unaufahamu mpira! Kwasababu Km unafahamu hivyo vitu ni umeshafahamu mpira!

Alafu Tarehe 3 mwezi ujao tutakua tunacheza na Man City! Usikose kuiangalia hiyo game dada yng na tutakua hapa hapa tukitoa updates live!

Karibu sn kwa Mabingwa watu wenye furaha siku zote!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…