Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

beki anahitajika sana pia tupate strike ampe changamoto costa,bashuai nadhani bado hajawa tayari
 
L

Left back huku kwa cahil kuna tatizo kwenye huu mfumo anahangaika sana hasa anapotumia mguu wa kulia
Cahill ni CB na hii 3-4-3 bado inawafanya hao mabeki wote kua ni ma CB tu. Ata km anacheza upande gani bado haihitaji mguu halisi Wa huo upande. Sema Alonso ktk huo upande amekua sio mzuri sn km Moses. Lkn wanayafanyia kz makosa yote kila baada ya mechi so natumaini watakua vzr
 
Kuna haja mkuu, in case kama zitatokea "injuries" pawepo na options za maana.
Anyway ngoja tuone Conte atafanya nini ktk dirisha dogo.

Lkn nijuavyo huyu Azipilicueta hizo pande zote mbili anazicheza vzr sn... Yani kushoto na kulia wakati huo huo nje tuko na Ola Zina na Ivanovic ambao hawa ni ma Right backs wazuri sn na pia huyu Ivanovic ni CB pia mzuri tu na tuna baba Terry nae ni CB mujarabu tu kwahiyo sioni km kuna shida huko nyuma kwa huu mfumo.


Sema tunatakiwa tuwe na pacha wazuri Wa kati km Matic na Kante pale kati ndio maana ktk hawa watu Faby, Oscar, Obi Chalobah wanapaswa kufanya kweli ili ubora uwe pale pale Ata km Matic au Kante wanapokua hawapo ingawa majuzi Faby alifanya vzr sn tena kwa ile game na ilivyokua na presha alijitahidi sn.....


Ni hayo tu mkuu...
 
Kuna Zouma pia mkuu. Hawa wote unaweza kuona km hawako fiti lkn Conte akiwahitaji anawapa nafasi.
 
Pamoja sana
 
Ni kweli mkuu lkn jamaa anajitahidi sn..... Na ninaamini atakaa vzr tu.

Anajitahidi kwa mechi za Hull. Unadhani kwa nini mechi za Tottenham na Man city Hazard hajafikia kiwango chake? Anajikuta anarudi nyuma sana kuchukua mipira wakati angekuwa kifaa chenye spidi kama Kennedy hazard angekuwa anajenga magorofa upande wa wapinzani hahitaji kurudi nyuma sana.
 
Lkn mkuu Ata upande Wa Moses nao ulikua hivyo. Tena kuna wakati niliona km Moses na Alonso hawakupanda kabisa mbele na kufanya ile line ya mabeki kua na watu watano.

Conte anawazuia wasipande hawa jamaa hovyo ktk baadhi ya game hasa hizi game kubwa kubwa.
 
Mkuu, ivanovich sio beki wa kumhesabia/kucheza chelsea ya conte, refer game ya spurz alivoingia ndo tukaanza kuzidiwa, mikel obi ni mzito anakimbia kama mjamzito ndo maana conte hataki hata kumuweka kwenye sub, hao mwakani tu hapo dirisha dogo wajisalimishe wenyewe kwa team za wazee e.g juventus/MLS/CHINA.
 
Game ya Spurs Moses alichoka na km unakumbuka spurs walifanya sub ikaingia ngozi nyeusi ikawa inamsumbua sn Moses ndio maana Conte akamtupia Iva aingie kutuliza hali.

Huu mfumo Wa Conte Wa 3-4-3 unategemea sn nguvu ya viungo Wa kati yaani hao watu 4 Wa kati ktk kushambulia au kukaba. Na km hao ma mid wanakua vzr kabisa on fire mabeki Wa nyuma hasa nafasi km ya Luiz huwezi muona kabisa akiwa uwanjani atakua yupo tu hana kz. Kwahiyo watu km Terry na Ivanovic wanaweza kucheza vzr tu ktk huu mfumo.
 

Moses alichoka maana ilimbidi kuongeza nguvu kwenye kuzuia...wewe angalia hiyo mechi vizuri utaona weakness ya Alonso ilivyotufanya tukawa weak kwingine kote. Ni mchezaji mzuri lakini naamini we can have someone better than him..hicho ndicho ninachosema.


Mechi 5 zinazofuata ni point 15 za nguvu

Nia tunayo...sababu tunayo...uwezo tunao...
 
Huu mfumo bado ni mpya kwetu. Bado tunauboresha, tukikutana na timu kubwa ndivyo mapungufu yanakuwa mengi, na ndivyo Conte atakavyoyarekebisha. Cahil ni dhaifu ndio maana Alonso anaonekana dhaifu pia, Alonso anatumia muda mwingi kumsidia Cahil upande wake. Nafasi ya Cahil awekwe Zouma
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…