Cheche Mitaani Jan 20:Yah: ATCL na majibu yetu kwa Rais

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
toleola23.jpg

Kwa mara ya mwisho kuhusu ATCL tumeweka kesi yetu wazi kwanini kuiharakisha kuruka tena na kuimwagia mabilioni ya fedha siyo tu ni kukosa hekima, lakini ni hatari pia kwani uamuzi huo umefikiwa kisiasa kuliko kibiashara.

Read and be the judge.
 
Attachments

  • TOLEOJIPYA23.pdf
    502.5 KB · Views: 248
Last edited by a moderator:
Sijui kama itawezekana hiyo Ijumaa maana mpaka leo walikuwa wanahangaika kutafuta wapunguze fungu gani katika bajeti ili kupata fedha za kuipatia ATCL kulingana na maagizo ya Muungwana. Watuw a ATCL wenyewe wanasema for sure safari zinaweza kuanza Jumatatu ijayo. But lets wait and see
 
Du kuchoka si kuchoka, usingizi si usingizi, njaa si njaa, hasira mpaka kiunoni - ina maana serikali haiyajui haya au ndio yale mambo ya mwenzetu. Lakini si JK huyo huyo ambaye wanasema yuko veri siriazi kushughulikia mafisadi?
 
Sijui kama itawezekana hiyo Ijumaa maana mpaka leo walikuwa wanahangaika kutafuta wapunguze fungu gani katika bajeti ili kupata fedha za kuipatia ATCL kulingana na maagizo ya Muungwana. Watuw a ATCL wenyewe wanasema for sure safari zinaweza kuanza Jumatatu ijayo. But lets wait and see

wenzio wameshatoa hata ratiba tayari.. .. wanajua fedha zinakuja tu, Rais keshasema ziruke... wao ni kutekeleza tu.
 
We have populist Presidaa ambae siku zote hupenda kusifiwa. Hivyo kuignore kiini cha matatizo ATCL na kukimbilia kuirusha hewani ni uthibitisho wa myopic vision ya Presidaa wetu ambaye ameingia madarakani kwa masifa ya nguvu mpya, kasi mpya na maisha bora kwa kila Mtanzania huku in reality, hakuna lolote.
Ni masifa hayo hayo amewatumia wahindi wa TRC kuwaeleza maamuzi yoyote makubwa lazima serikali iyaridhie huku amewapa asilimia 51% na serikali 49% na mkataba ni wa miaka 20!
Ni masifa hayo hayo kujifanya haelewi kinachoendelea ATCL na kusema kama issue ni pesa, wapeni waruke hewani haraka.
Mzee ameshalewa masifa hivyo anaendesha serikali kwa masifa, siku ya siku itafika na masifa yake yatamtokea puani!.
 
Kwa mtizamo wangu mdogo, kwa kila siku ambayo ndege za ATCL haziruki ni hasara zaidi kuliko zinapokuwa haziruki...

Pamoja na kwamba inabidi viongozi wakae na kujua chanzo na jawabu ya ATCL kuwa ama lifilisiwe au liendeshwe vipi.

Kwa mtu yeyote anayejua biashara ataungana na mh. Rais kwamba ndege kuruka ilikuwa ni kipaumbele kwanza...

Kumbuka urushe ndege au usirushe kodi ya kukodisha ndege lazima ulipe.

Ni mawazo mgando, kufikiri ati uanze na viongozi au uanze na utafiti kwanza ndio urushe ndege... haya ni mawazo ya kisiasa zaidi kuliko hata yale Rais aliyosema.
 
Maagizo ya kusema ndege ziruke tu bila kuangalia tatizo la shirika ni nini ni swa swa na mawazo ya kutaka mtu asifiwe wakati unaona anataka kufa.

Wameshindwa kupitia mikataba ya ndege mbili mbovu zilizokodishwa na hapo hapo Hawajui ni nani aliyesababisha ATCL kufungiwa.

Je PPRA ACT ilifuatwa?

Tunajua kuna uzembe ulifanyika na wao walikiri,Yaani kukiri inatosha tu....Mara nyingine tena nakubaliana na Nyani Ngabu waafrika ndivyo tulivyo..

Who has a clue nani aliagiza hizo ndege zinunuliwe?I know who did that and i will let you know now

Maagizo ya kukodishwa kwa ndege hizi yalikuwa kama yale maagizo ya juzi,Sasa naona umeona tatizo lipo wapi!

Halima Mlacha
Daily News; Wednesday,January 21, 2009 @20:19

Baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa agizo kwa uongozi wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kwamba ndege hizo zianze safari zake haraka iwezekanavyo, ndege za kampuni hiyo zimethibitika kuwa zitaanza safari zake rasmi kesho.

Hayo yalithibitishwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Usafiri wa Anga wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Kirenga Ndemino wakati Kamati ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea ofisi za mamlaka hiyo jana Dar es Salaam.

Akijibu baadhi ya maswali ya wabunge juu ya kusimamishwa kufanya kazi kwa ndege za ATCL na lini zitaanza kazi, Ndemino, alisema taarifa alizonazo ndege hizo zitaanza kuruka tena kesho baada ya uongozi wa kampuni hiyo kupatiwa nyongeza ya Sh bilioni mbili na Wizara ya Fedha.

"Kwa taarifa zilizopo ni kwamba Sh bilioni mbili zinatarajiwa kutolewa leo (jana) na Hazina, zikishatolewa huduma zinaweza kuanza Ijumaa," alisema Ndemino. Awali akijibu maswali ya wabunge wa kamati hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Magreth Munyagi, alisema kampuni hiyo ilinyang'anywa leseni yake ya kurusha ndege baada ya Shirika la Kimataifa la Ukaguzi wa Usafiri wa Anga (IOSA) kugundua dosari katika muundo na menejimenti, ndege, usafirishaji, matengenezo, chumba cha marubani, usimamizi wa mizigo na operesheni za kiusalama.

Alisema kutokana na kubadilishwa kwa kanuni za usalama ambazo zitaanza kutekelezwa Februari mwaka huu, TCAA ilitoa taarifa kwa kampuni zote za usafirishaji wa anga nchini zifanye marekebisho katika operesheni zake na kuyakabidhi kabla ya leseni zao kuisha muda.

Alisema hata hivyo ilipofika Desemba ndipo ukaguzi kutoka IOSA ulipoanza na TCAA iliamua kuchukua uamuzi wa kuinyang'anya leseni ATCL kwa vile ilikuwa bado haijakamilisha kwani iwapo IOSA wangegundua upungufu kwa kampuni moja ingeonekana Tanzania nzima ina upungufu.

Akisoma taarifa ya mamlaka hiyo, alisema moja ya changamoto kubwa zinazoikabili mamlaka hiyo ni ufunguaji wa soko kwenye sekta kwani Tanzania ni moja ya nchi zilizoingia mkataba wa soko huria kwenye usafiri wa anga hali ambayo itaongeza ushindani mkubwa kwa kampuni za usafiri wa ndege nchini.

Naye Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohammed Missanga, alisema awali uongozi wa ATCL ulipatiwa na Serikali Sh bilioni 2.5 hali inayofanya mpaka sasa kampuni hiyo kupatiwa Sh bilioni 4.5 ili kukamilisha taratibu zake na ndege hiyo kuanza safari.

Aliitaka Mamlaka ya TCAA kuhakikisha kuwa inasimamia kampuni za ndege nchini katika suala zima la matengenezo ya ndege zao ili kuepusha ajali za mara kwa mara pamoja na kukatishwa safari hovyo hali ambayo inashusha kiwango cha huduma za ndege hizo.

Wabunge ambao ni wajumbe wa kamati waliouliza maswali kuhusu ATCL na majimbo yao katika mabano ni pamoja na, Suleiman Kumchaya (Lulindi), Paul Kimiti (Sumbawanga), Mtutura Mtutura(Tunduru), Ludovick Mwananzila (Kalambo) na Mbunge wa Rorya , Profesa Philemon Sarungi wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 
Halima Mlacha
Daily News; Wednesday,January 21, 2009 @20:19

Baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa agizo kwa uongozi wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kwamba ndege hizo zianze safari zake haraka iwezekanavyo, ndege za kampuni hiyo zimethibitika kuwa zitaanza safari zake rasmi kesho.

Hayo yalithibitishwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Usafiri wa Anga wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Kirenga Ndemino wakati Kamati ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea ofisi za mamlaka hiyo jana Dar es Salaam.

Akijibu baadhi ya maswali ya wabunge juu ya kusimamishwa kufanya kazi kwa ndege za ATCL na lini zitaanza kazi, Ndemino, alisema taarifa alizonazo ndege hizo zitaanza kuruka tena kesho baada ya uongozi wa kampuni hiyo kupatiwa nyongeza ya Sh bilioni mbili na Wizara ya Fedha.

“Kwa taarifa zilizopo ni kwamba Sh bilioni mbili zinatarajiwa kutolewa leo (jana) na Hazina, zikishatolewa huduma zinaweza kuanza Ijumaa,” alisema Ndemino. Awali akijibu maswali ya wabunge wa kamati hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Magreth Munyagi, alisema kampuni hiyo ilinyang’anywa leseni yake ya kurusha ndege baada ya Shirika la Kimataifa la Ukaguzi wa Usafiri wa Anga (IOSA) kugundua dosari katika muundo na menejimenti, ndege, usafirishaji, matengenezo, chumba cha marubani, usimamizi wa mizigo na operesheni za kiusalama.

Alisema kutokana na kubadilishwa kwa kanuni za usalama ambazo zitaanza kutekelezwa Februari mwaka huu, TCAA ilitoa taarifa kwa kampuni zote za usafirishaji wa anga nchini zifanye marekebisho katika operesheni zake na kuyakabidhi kabla ya leseni zao kuisha muda.

Alisema hata hivyo ilipofika Desemba ndipo ukaguzi kutoka IOSA ulipoanza na TCAA iliamua kuchukua uamuzi wa kuinyang’anya leseni ATCL kwa vile ilikuwa bado haijakamilisha kwani iwapo IOSA wangegundua upungufu kwa kampuni moja ingeonekana Tanzania nzima ina upungufu.

Akisoma taarifa ya mamlaka hiyo, alisema moja ya changamoto kubwa zinazoikabili mamlaka hiyo ni ufunguaji wa soko kwenye sekta kwani Tanzania ni moja ya nchi zilizoingia mkataba wa soko huria kwenye usafiri wa anga hali ambayo itaongeza ushindani mkubwa kwa kampuni za usafiri wa ndege nchini.

Naye Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohammed Missanga, alisema awali uongozi wa ATCL ulipatiwa na Serikali Sh bilioni 2.5 hali inayofanya mpaka sasa kampuni hiyo kupatiwa Sh bilioni 4.5 ili kukamilisha taratibu zake na ndege hiyo kuanza safari.

Aliitaka Mamlaka ya TCAA kuhakikisha kuwa inasimamia kampuni za ndege nchini katika suala zima la matengenezo ya ndege zao ili kuepusha ajali za mara kwa mara pamoja na kukatishwa safari hovyo hali ambayo inashusha kiwango cha huduma za ndege hizo.

Wabunge ambao ni wajumbe wa kamati waliouliza maswali kuhusu ATCL na majimbo yao katika mabano ni pamoja na, Suleiman Kumchaya (Lulindi), Paul Kimiti (Sumbawanga), Mtutura Mtutura(Tunduru), Ludovick Mwananzila (Kalambo) na Mbunge wa Rorya , Profesa Philemon Sarungi wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 
I hope Mh. Rais amedhamiria kutatua matatizo ya ATCL kwa kuanza na hili la kuhakikisha ndege zinaruka.

Ninaamini pia kuwa ndani ya miezi mitatu atakuwa ameendelea kutatua matatizo mengine yaliyobaki ndani ya ATCL.

Mimi ninavuta subira
 
Wanabodi,
Mwanakijiji shukran sana kwani nimeokoteza moja mbili toka taarifa hiyo hapo juu...
Ebu someni maneno haya kisha mfikiri na kutanabahi uzito wake...

1. Alisema:- Kampuni hiyo ilinyang'anywa leseni yake ya kurusha ndege baada ya Shirika la Kimataifa la Ukaguzi wa Usafiri wa Anga (IOSA) kugundua dosari katika muundo na menejimenti, ndege, usafirishaji, matengenezo, chumba cha marubani, usimamizi wa mizigo na operesheni za kiusalama.

Kisha unganisheni na kipande hiki....

2. Alisema:- Hata hivyo ilipofika Desemba ndipo ukaguzi kutoka IOSA ulipoanza na TCAA iliamua kuchukua uamuzi wa kuinyang'anya leseni ATCL kwa vile ilikuwa bado haijakamilisha kwani iwapo IOSA wangegundua upungufu kwa kampuni moja ingeonekana Tanzania nzima ina upungufu.

Jamani sii haya ndiyo tunazungumza kila siku humu JF! -Tanzania nzima ina MAPUNGUFU..sasa badala ya kurekebisha mapungufu yetu badala yake tunafukia vichwa vyetu mchngani kama mbuni!..Hivi tunajarivu kumficha nani hapa!.. kama kweli Tanzania nzima ina mapungufu why tunafagia uchafu wetu chini ya uvungu...
Wananchi wanapopiga kelele, na viongozi wetu kutokubali kuwepo kwa mapungufu ndilo somo naloshindwa kuelewa kabisa!
 
breaking news
ATCL YAFANYA RESHUFLE
DIRECTOR OF OPERAATION ----JOSEPH IBANDA
CFO KUKABIDHI JUMATATU OFFICE.....
MSHAURI WA RAIS SI MARK MANJI TENA.......

TUNOMBA AMBAO BADO TUFANYIE KAZI

WENU

USALAMA WA ANGA(sweetest)
 
huyu ndie yule PILOT ALIEAMUA KUONYESHA PROFFESIONAL YAKE SIKU YULE MHUNI WA ARUSHA NJITI..ALIEKUJA AMEKUNYWA HOI KWENYE NDEGE NASIKIA AKIWA NA MAWAZIR WAKINA BURIAN WAKAMTETEA KWASABABU YA KUSAIDIA CCM..AKAWAAMBIAWASHUKE WOTE KAMA ATAKI KUSHUKA ..AWEZI PANDISHA AMELEWA HIVYO..NASIKIA AKAANZAPIGIWA NA WAKUBWA MKUU W POLISI MWISHO AKAWASHUSHA WOTE NA KUAMURU JAMAA AHIFADHIWE POLISI AKUWEZA KURUDI HIYO NDIO SIFA TULIOISIKIA
JAMAA NA SIKIA MZEE WA STANDARD
 
Mwanakijiji,
Mkuu, mbali na ile ndege ya Liberia, kuna ndege nyingine used Boieng 737 iliyokodishwa au kununuliwa hapa Canada mwaka juzi..
 
Tanzania kichwa cha mwendawazimu Kila mtu anajifunzia kunyoa. Kudos kwa Ethiopia airways kwa kusimama kidede kuvunja dhana kwamba 'waafrika ndio walivyo'. Tatizo tunasahahu kwamba mashirika mengi yanaendeshwa kisiasa zaidi kuliko kibiashara. Tukaa chini tutafanya hizo analysis lakini mwisho wa siku siasa ndio mchawi wa haya mashirika yetu.Kesheni mkiomba lakini kaeni mkifahamu kwamba SI A SA ndio kiini cha vifo vya mashirika yetu kufa!

Swali la kujiuliza ni nini kifanyike kuboresha mashirika yetu ya umma? kuna rushwa, undugunization, na sasa kuna pia sumu za huyu ni mwenzenu katika mashirka yetu, political intervention si mnakumbuka baba mkwe wa mwungwana alivyokwama pale JK Airport na maamuzi ya bodi ya ATCL? Naona tunaitaji wabantu wa kihabeshi kuja kutusaidia hili tuweze keelewa waliwezaje kufika pale walipofika licha ya misukosuko yote nchi yao iliyopitia kama vita vya wenyewe kwa wenyewe.
 
yaani wana-reshuffle management bila kumuondoa CEO mwenyewe?
kweli watu wanapoteza hela za walipa kodi kwa kuhangaika na shirika hili, huwezi kuendesha biashara kisiasa siasa tu...
hopelessix8.gif

By mafisadi
 
Back
Top Bottom