CHAUMMA yaionya CHADEMA, wasituletee migogoro

Mzee wangu Hashim Rungwe sipunda kakipigania sana hicho chama, naona vijana wake wanatoka nje ya misingi ya chama, sera ya CHAUMA ni ubwabwa na chakula kwa wote, kutibu njaa.

Hawa vijana wakumbushwe sera ya CHAUMA

..Chauma haikukubali matokeo ya uchaguzi ya 2020.

..lakini mwaka jana juu ya yale mauaji ktk uchaguzi Chauma wamesaini kukubali matokeo.
 
..mgogoro mkubwa uliopo ni wa kisiasa.

..kwa msingi, huo vyama vyote vilivyosajiliwa lazima viwepo mezani.
Sio lazima. Majadiliano yanapaswa kuwa ya hiari. Chama kisichotaka kukaa mezani hakiwezi kulazimishwa kukaa mezani. Hivyo hivyo hamna chama chenye haki ya kulazimisha chama kingine kisishiriki katika majadiliano kwa sababu yeyote ile. Kushiriki au kutoshiriki ni uamuzi wa kila chama.
Amandla...
 
..Chauma haikukubali matokeo ya uchaguzi ya 2020.

..lakini mwaka jana juu ya yale mauaji ktk uchaguzi Chauma wamesaini kukubali matokeo.
Kukubali matokeo kunaweza kusababishwa na vitu vingi. Al Gore alikubali matokeo ya Florida ingawa alijua thika kuwa mdogo wake George W amemchezea mchezo mbaya.

Chaumma kinaweza kuamua kukubali matokea kwa nia ya kuepusha balaa ambayo ingeweza kutokea.

Amandla...
 
Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimesema kuwa ili ukweli ujulikane na haki itendeke, ni muhimu kufanyika kwa mazungumzo yatakayowezesha pande husika kuwasilisha hoja zao na kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Novemba 25, 2026 mkoani Dar es Salaam Kaimu Katibu Mkuu wa CHAUMMA, Benson Kigaila, amesema chama hicho hakioni sababu ya CHADEMA kutaka ukweli ujulikane bila kuwa tayari kukaa mezani kwa ajili ya mazungumzo.

Kigaila amesema kuwa iwapo CHADEMA wana hoja binafsi au malalamiko yanayohusu chama chao, wanapaswa kutafuta njia za kuyatatua badala ya kuyachanganya na masuala mengine.

Ameongeza kuwa masuala yanayohusu maslahi ya kitaifa yanapaswa kujadiliwa kwa pamoja kwa kukaa mezani ili kila upande uweze kutoa hoja zake na kusikilizana.

Amesema ni vyema pande husika zikashiriki katika mazungumzo hayo kwa lengo la kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo na kuweka mbele maslahi ya Taifa.
Chaumma wasituletee ujinga
 
..Tundu Lissu awe nje, halafu watazungumza kuhusu msuluhishi.
Chadema inabidi ijipange upya kwenye hili maana inaelekea hakuna nia ya kumuachia wakati wowote hivi karibuni. Ushahidi nk rufaa iliyokatwa na DPP. CCM haina hasara Tundu Lissu akibaku ndani.
..Au kipindi hiki wameomba vyama na taasisi mbalimbali wapendekeze wajumbe wangeomba pia Msuluhishi apendekezwe.
Wajumbe ndio wanatakiwa kupendekeza Msuluhishi.
..lakini pia wanaweza kuwa na mazungumzo ambayo ni "in-direct" kuhusu hoja mbili za Chadema halafu ndio waende rasmi mezani.
Huo ni uamuzi kati ya CCM na Chadema. Vyama vingine havihusiki.

Amandla...
 
Hoja ya Kigaila inaacha swali moja la msingi. Je, mazungumzo ni lengo lenyewe au ni njia ya kutafuta suluhu ya matatizo yaliyopo?

Hakuna anayepaswa kuaminisha umma kwamba kukataa kushiriki mazungumzo kwa masharti yasiyoeleweka ni sawa na kukataa ukweli na haki. Mazungumzo ya kweli yanahitaji mazingira ya kuaminiana, nia njema, ajenda inayokubalika na dhamira ya kutekeleza yatakayokubaliwa.

Pia, haiwezekani kutenganisha matatizo yanayoikabili CHADEMA na masuala ya kitaifa kana kwamba hayana uhusiano. Ikiwa kuna changamoto zinazohusu demokrasia, haki za kisiasa, utawala wa sheria na mustakabali wa taifa, hizo si hoja binafsi za chama bali ni masuala yenye maslahi mapana kwa wananchi.

CHADEMA haiwezi kubebeshwa wajibu wa kuhalalisha mchakato wa mazungumzo kwa kushiriki tu. Wajibu wa kujenga mazingira ya mazungumzo ni wa pande zote.

Kwa hiyo, swali si kwa nini CHADEMA inasita kukaa mezani, bali ni mezani hapo kuna nini, nani anaweka ajenda, kuna dhamana gani ya utekelezaji na je, kuna utayari wa kushughulikia mizizi ya matatizo au tunatafuta tu picha ya kisiasa inayoitwa maridhiano?

Maridhiano bila kushughulikia chanzo cha mgogoro ni kusogeza tatizo mbele, si kulitatua
 
Chadema inabidi ijipange upya kwenye hili maana inaelekea hakuna nia ya kumuachia wakati wowote hivi karibuni. Ushahidi nk rufaa iliyokatwa na DPP. CCM haina hasara Tundu Lissu akibaku ndani.

Wajumbe ndio wanatakiwa kupendekeza Msuluhishi.

Huo ni uamuzi kati ya CCM na Chadema. Vyama vingine havihusiki.

Amandla...

Nani ataongoza hayo maridhiano?
Wanaridhiana katika mgogoro upi?
Samia alishinda Kwa 98% na vyama vya mfukoni vikampongeza
Voters turn out ilikuwa zaidi ya 90%
Mchakato wa upigaji kura, kuhesabu na kutangaza ulikuwa vizuri
 
Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimesema kuwa ili ukweli ujulikane na haki itendeke, ni muhimu kufanyika kwa mazungumzo yatakayowezesha pande husika kuwasilisha hoja zao na kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Novemba 25, 2026 mkoani Dar es Salaam Kaimu Katibu Mkuu wa CHAUMMA, Benson Kigaila, amesema chama hicho hakioni sababu ya CHADEMA kutaka ukweli ujulikane bila kuwa tayari kukaa mezani kwa ajili ya mazungumzo.

Kigaila amesema kuwa iwapo CHADEMA wana hoja binafsi au malalamiko yanayohusu chama chao, wanapaswa kutafuta njia za kuyatatua badala ya kuyachanganya na masuala mengine.

Ameongeza kuwa masuala yanayohusu maslahi ya kitaifa yanapaswa kujadiliwa kwa pamoja kwa kukaa mezani ili kila upande uweze kutoa hoja zake na kusikilizana.

Amesema ni vyema pande husika zikashiriki katika mazungumzo hayo kwa lengo la kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo na kuweka mbele maslahi ya Taifa.
Malaya na misukule wa ccm bado hamjasema , mbwa takataka ninyi .Karidhianeni na nyuchi za mama zenu na Maiti za watu maelfu mliowaua kikatili na kuwatupa kwenye Mashimo kama mizoga ya mbwa na mliowateka na kuwatesa na kuwalawiti na kuwanajisi .Takataka nyie
 
Chadema inabidi ijipange upya kwenye hili maana inaelekea hakuna nia ya kumuachia wakati wowote hivi karibuni. Ushahidi nk rufaa iliyokatwa na DPP. CCM haina hasara Tundu Lissu akibaku ndani.

Wajumbe ndio wanatakiwa kupendekeza Msuluhishi.

Huo ni uamuzi kati ya CCM na Chadema. Vyama vingine havihusiki.

Amandla...

..hiyo Rufaa ambayo Dpp amekata kuhusu Tundu Lissu inapaswa kuwa alert / taa nyekundu kwa vyama vyote kuhusu nia ya serikali kuleta maridhiano.

..chama kimoja cha upinzani kikiumizwa vyama vyote vya upinzani vinapaswa kuchukulia kuwa navyo vimeumizwa.

..Kwa maoni yangu, ushiriki wa Chadema unaongeza nguvu ktk hoja na madai ya upinzani kwa ujumla.

..Ingependeza kama vyama vyote vya upinzani vingetoa msimamo kwamba hoja za Chadema za kuachiwa kwa Mwenyekiti wao na uwepo wa Msuluhishi huru zizingatiwe.

..Madai ya Chadema kwa maoni yangu ni kwa faida ya vyama vyote vya upinzani, na yamelenga kuleta maridhiano ya kweli ktk nchi yetu.
 
Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimesema kuwa ili ukweli ujulikane na haki itendeke, ni muhimu kufanyika kwa mazungumzo yatakayowezesha pande husika kuwasilisha hoja zao na kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Novemba 25, 2026 mkoani Dar es Salaam Kaimu Katibu Mkuu wa CHAUMMA, Benson Kigaila, amesema chama hicho hakioni sababu ya CHADEMA kutaka ukweli ujulikane bila kuwa tayari kukaa mezani kwa ajili ya mazungumzo.

Kigaila amesema kuwa iwapo CHADEMA wana hoja binafsi au malalamiko yanayohusu chama chao, wanapaswa kutafuta njia za kuyatatua badala ya kuyachanganya na masuala mengine.

Ameongeza kuwa masuala yanayohusu maslahi ya kitaifa yanapaswa kujadiliwa kwa pamoja kwa kukaa mezani ili kila upande uweze kutoa hoja zake na kusikilizana.

Amesema ni vyema pande husika zikashiriki katika mazungumzo hayo kwa lengo la kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo na kuweka mbele maslahi ya Taifa.
Unataka wajadiliane na akina nani?????Wenye maamuzi ya uongo uongo kwa ajili ya kunufaisha familia zao????Tanzania ya leo siyo ya wajinga wajinga wapenda vya bure.
 
Bado swali linabaki pale pale. Huyo msuluhishi atapatikanaje bila pande zote kukaa na kukubaliana utaratibu wa kumpata anaekubalika na wote?

Amandla...
Mbona simple tu.Akipatikana kwenye nchi zenye mawazo positive ukiondoa Uganda,Rwanda,Sudani,Mali,Sudani Kusini,Msumbiji,Eritrea,Djibout,Ethiopia na DRC mbona maridhiano yanawezekana???Pia kuna nchi kama Urusi hawastahili hata kidogo kuwa wasuluhishi wa mogogoro yetu.
 
Mzee wangu Hashim Rungwe sipunda kakipigania sana hicho chama, naona vijana wake wanatoka nje ya misingi ya chama, sera ya CHAUMA ni ubwabwa na chakula kwa wote, kutibu njaa.

Hawa vijana wakumbushwe sera ya CHAUMA

..Hashim Rungwe lazima angempigania Tundu Lissu.

..siku mbili kabla Lissu hajapigwa risasi alikuwa Central Police Dsm ambako Mzee Rungwe alikuwa anashikiliwa.

..kwasababu Lissu alikuwa akielekea bungeni Dodoma alimuahidi kulisemea suala la Mzee Rungwe bungeni kama Polisi wasingemfikisha mahakamani, au kumpa dhamana.

..Mzee Rungwe aliachiwa, lakini huko Dodoma Tundu Lissu akashambuliwa kwa risasi na kunusurika kifo.

..Sasa leo hii Mzee Rungwe amekaribisha watu ambao wanaunga mkono mamlaka zinazomkandamiza Tundu Lissu.
 
Sio lazima. Majadiliano yanapaswa kuwa ya hiari. Chama kisichotaka kukaa mezani hakiwezi kulazimishwa kukaa mezani. Hivyo hivyo hamna chama chenye haki ya kulazimisha chama kingine kisishiriki katika majadiliano kwa sababu yeyote ile. Kushiriki au kutoshiriki ni uamuzi wa kila chama.
Amandla...
Huwezi kuja na kauli kama hii huku ukijua fika maridhiano yanalenga kuliunganisha taifa, kisha ukakiacha nje chama chenye uungwaji mkono mkubwa zaidi ya vingine vyote, hayo maridhiano yatakuwa sawa na maigizo tu na tatizo litabaki palepale.
 
Mbona simple tu.Akipatikana kwenye nchi zenye mawazo positive ukiondoa Uganda,Rwanda,Sudani,Mali,Sudani Kusini,Msumbiji,Eritrea,Djibout,Ethiopia na DRC mbona maridhiano yanawezekana???Pia kuna nchi kama Urusi hawastahili hata kidogo kuwa wasuluhishi wa mogogoro yetu.

..Mzee Lazarus Chakwera alipokuja kwa kutumwa na Jumuiya ya Madola, wadau wote walikubali kuzungumza naye.

..Binafsi naamini wako watu Mashuhuri Afrika na Jumuiya ya Madola ambao wanaweza kusaidia mgogoro wetu.

..Bahati mbaya Ccm, na vyama rafiki zake, wanaangalia maslahi ya Ccm, badala ya kutanguliza maslahi ya NCHI.

..Ccm bado wanaamini wana nafasi ya kufanya janjajanja kupitia maridhiano.
 
Back
Top Bottom