Chato: Rais amwaga misaada kwenye shule aliyosoma

Chato: Rais amwaga misaada kwenye shule aliyosoma

Hapo wanafunzi amewatia MORALI ya kusoma kwa bidii.
Maana hapo ndo msingi wake ulipoanzia.
Nao wangetaka WAFANIKIWE maishani.
Safi sana!
Mwanangu nampeleka kwenye hiyo shule ili aje afanikiwe na kua rais
 
..duh!

..hivi ktk kipindi hiki chato walihitaji msaada kuliko kagera?
 
Rais Magufuli aimwagia neema shule aliyosomea

Monday , 9th Jan , 2017
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika Shule ya Msingi Chato, ambapo ndipo aliposoma kuanzia darasa la kwanza hadi la saba na kuzungumza na walimu na wanafunzi wa shule hiyo.




JPM%20Chato%20shule%203.jpg

Rais Magufuli (Katikati) akitokelezea na wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato



Rais Dkt Magufuli ameahidi kujenga madarasa matatu na ofisi moja ya walimu katika Shule hiyo kufuatia ombi la walimu kuwa shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi wanaosoma shuleni hapo.

Aidha Dkt. Magufuli amewaasa wanafunzi kutilia mkazo masomo ili waweze kufaulu na kuwataka walimu kuhakikisha wanatumia vyema fedha zinazotolewa na Serikali kila mwezi katika kutoa elimu bila malipo na pasiwe na wanafunzi hewa kama ilivyo kwa baadhi ya shule ambazo zimegundulika kuwa na wanafunzi hewa katika uhakiki uliofanywa na serikali.

JPM%20chato%20shule%202.JPG


Rais Magufuli akigonga kengele ya shule mara baada ya kuwasili shuleni hapo

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chato, Bwana Mwita Chacha amemshukuru Rais Dkt.Magufuli kwa msaada aliowapatia katika kukabiliana na uhaba wa madarasa uliokuwa unaikumba shule hiyo, pia kuitembelea shule yao jambo ambalo limewatia moyo walimu na wanafunzi shuleni hapo.

Rais Magufuli pia ametembelea eneo la Stand ya zamani na kuzungumza na baadhi ya wananchi waliokuwepo eneo hilo na kutoa msaada kwa kikundi cha wasafisha viatu ili kuongeza mtaji wa biashara yao.

Jpm%20chato%20viatu.jpg


Rais Magufuli akiwa kwenye kibanda cha kupigia viatu kiwi pamoja na wakazi wengine wa Chato, katika eneo la stendi ya zamani. Hapo ndipo Rais Magufuli alikuwa akipatumia kusafisha viatu vyake kabla hajawa Rais

Hivi Mh. Keshaenda Chato mara ngapi tangia ale shavu la Urais?
 
Tingatinga mzee wa kupigwa katerero
bulldozer,tingatinga,timekeeper,the list goes on and on...viva Magufuli viva!

mshapata a.k.a mpya,enhe?

timekeeper,bulldozer,naona a.k.as zinazidi kuchipuka!

Kwani Magufuli ni Mahakama?
Kwani Magufuli ni NHC?
 
Safi sana JPM, safisha hii nchi hata mwalimu alisema haka ka-inchi kananuka rushwa
 
time keeper,all the time yupo CHATU!!!BAA LA NJAA,litatangazwa from Chatu!!!
 
Safi mh raisi kwa kujichanganya na jamii. Pole sana watu wa usalama kwa kazi zito mnayoipata, nahisi nnashindwa tu kusema jinsi mnavyokuwa ktk wakati mgumu kwa raisi kijumuika namna hiyo.
 
Chato wana mwagiwa neema. Kagera watetemeke wenyewe kujijengea makazi yao
Acha tu, ukimwi wao, tetemeko lao, njaa yao, mvua ya mawe yao, ukame wao, mnyauko kwao, mto ngono wao, gulioni katerero kwao...mwafaaaa
 
Mwanangu nampeleka kwenye hiyo shule ili aje afanikiwe na kua rais
Nisingeshangaa kwa sababu kila mmoja wetu huwa ana model/Mfano wa kufuata maishani.
Kuna wengine walikuwa wakichunga mifugo.
Na walipokuwa wanawaona watoto wenzao wamebeba vitabu wakasema Hata mimi NITASOMA.
Si lazima watoto wawe Marais ila INAMPA MTOTO MOYO wakutaka ELIMU.
Ama mkuu unaonaje?
 
Mbona kama kila siku yupo huko huko tu... nchi kamuachia nani?
 
Rais wa wanyonge Mnaomsema kwani kuna mtu hapapendi kwao ?wacha asaidie shule alisoma hasiposaidia si mtazidi kumponda nyie.
 
Back
Top Bottom