Chato: Rais amwaga misaada kwenye shule aliyosoma

Chato: Rais amwaga misaada kwenye shule aliyosoma

Sasa hivi JPM anapitia wakati mgumu sana,
Wakati ambao wananchi hawataki kusikia chochote kutoka kwake..
Watu wamejazwa hasira zaidi ya mbogo..
Wananchi gani hawataki kusikia chochote kutoka kwake? Muwe mnachinganya na watu wengine jamani. Unakuta mtu ang'ang'ania pale Kijenge juu tu, A town(mfano), anajua hiyo ndio Tanzania.
 
bulldozer,tingatinga,timekeeper,the list goes on and on...viva Magufuli viva!

mshapata a.k.a mpya,enhe?

timekeeper,bulldozer,naona a.k.as zinazidi kuchipuka!

Kwani Magufuli ni Mahakama?
Kwani Magufuli ni NHC?
Lumumba mkianza kufikilia kwa kutumia kichwa, tutafika mbali sana maana mfumo wa kufikilia kwa kutumia tumbo unawazalilisha sana
 
Huyu jamaa mbona kama anapiga kampeni hivi wakati muda bado...
 
Rais Magufuli aimwagia neema shule aliyosomea

Monday , 9th Jan , 2017
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika Shule ya Msingi Chato, ambapo ndipo aliposoma kuanzia darasa la kwanza hadi la saba na kuzungumza na walimu na wanafunzi wa shule hiyo.




JPM%20Chato%20shule%203.jpg

Rais Magufuli (Katikati) akitokelezea na wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato



Rais Dkt Magufuli ameahidi kujenga madarasa matatu na ofisi moja ya walimu katika Shule hiyo kufuatia ombi la walimu kuwa shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi wanaosoma shuleni hapo.

Aidha Dkt. Magufuli amewaasa wanafunzi kutilia mkazo masomo ili waweze kufaulu na kuwataka walimu kuhakikisha wanatumia vyema fedha zinazotolewa na Serikali kila mwezi katika kutoa elimu bila malipo na pasiwe na wanafunzi hewa kama ilivyo kwa baadhi ya shule ambazo zimegundulika kuwa na wanafunzi hewa katika uhakiki uliofanywa na serikali.

JPM%20chato%20shule%202.JPG


Rais Magufuli akigonga kengele ya shule mara baada ya kuwasili shuleni hapo

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chato, Bwana Mwita Chacha amemshukuru Rais Dkt.Magufuli kwa msaada aliowapatia katika kukabiliana na uhaba wa madarasa uliokuwa unaikumba shule hiyo, pia kuitembelea shule yao jambo ambalo limewatia moyo walimu na wanafunzi shuleni hapo.

Rais Magufuli pia ametembelea eneo la Stand ya zamani na kuzungumza na baadhi ya wananchi waliokuwepo eneo hilo na kutoa msaada kwa kikundi cha wasafisha viatu ili kuongeza mtaji wa biashara yao.

Jpm%20chato%20viatu.jpg


Rais Magufuli akiwa kwenye kibanda cha kupigia viatu kiwi pamoja na wakazi wengine wa Chato, katika eneo la stendi ya zamani. Hapo ndipo Rais Magufuli alikuwa akipatumia kusafisha viatu vyake kabla hajawa Rais



ETI AMWAGA MISAADA.MMHHH
 
Kuna shida ukiwa na watu wanaotoka kanda zenye kupenda sifa za kipuuzi,halafu nchi ikawa ina mianya ya kila anayefika juu anaweza fanya apendalo.Nchi kama marekani wana sheria na mifumo mizuri ya kutosha kuzuia tabia binafsi za mtu kuathiri nchi vibaya.
 
Back
Top Bottom