Chato: Makamu Mwenyekiti UWT Akagua Miradi ya Maendeleo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
Dondoo
  • Mradi wa maji Bilioni 5.6
  • Mradi wa Bwaro Shule ya Sekondari Mil. 100
  • Mradi wa kituo cha Afya. Mil. 526

Viongozi wa UWT Taifa leo Septemba 28. 2023 wamefika wilaya ya Chato katika muendelezo wa Ziara ya kikazi inayoendelea mkoani Geita, yenye lengo la kuzungumza na wana CCM, kuimarisha jumuiya ya UWT na Chama pamoja na kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi 2020-2025.

Makamu Mwenyekiti wa UWT MNEC. Zainab Shomari ametembelea na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Bwalo la chakula katika shule ya Sekondari Zakia Meghji lenye thamani ya shilingi milioni 100, ujenzi wa Mradi wa maji Muganza wenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 5.6 na mradi wa kituo cha Afya Bwongera wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 526.

Makamu Zainab amemshukuru na kumpongeza Rais Samia kwa kutenga pesa kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.

“Rais Samia ameendelea kuleta maendeleo katika sekta zote ikiwemo elimu,bwalo hili ni mkombozi kwa wanafunzi kupata huduma ya chakula katika mandhari mazuri”amesema makamu Zainab alipokagua mradi wa ujenzi wa Bwalo

Akiwa katika mradi wa maji Muganza unaotarajiwa kunufaisha wananchi zaidi ya 73,680 katika kata ya Kigongo,Muganza na Bwongera amesema

“Rais Samia amekuwa na dhamira ya kumtua mwanamke ndoo kichwani,ni wazi mradi huu ni hatua muhimu za kufanikisha azma yake”

Akikagua kituo cha Afya Bwongera amewataka wasimamizi kuongeza kasi ya ujenzi na kuagiza kuanza kutoa huduma za wagonjwa wa nje (OPD) kwa majengo yaliyokamilika.

“Nimesikia kwenye taarifa kukamilika kwa kituo hichi kutapunguza umbali wa kilomita 42 kwa wananchi kufuata huduma katika hospitali ya wilaya Chato,niwaombe jengo la wagonjwa wa nje lianze kutumika ili azma ya serikali ya kusogeza huduma hii muhimu ionekane kwa wananchi”

🗓️28/9/2023 📍Chato-Geita

UWT IMARA.
JESHI LA MAMA.
KAZI IENDELEE.

WhatsApp Image 2023-09-29 at 00.20.29.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-29 at 00.20.29(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-28 at 23.30.52.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-29 at 00.20.30.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-28 at 23.30.44.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-28 at 23.30.43.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-28 at 23.30.42.jpeg
 
“Nimesikia kwenye taarifa kukamilika kwa kituo hichi kutapunguza umbali wa kilomita 42 kwa wananchi kufuata huduma katika hospitali ya wilaya Chato,niwaombe jengo la wagonjwa wa nje lianze kutumika ili azma ya serikali ya kusogeza huduma hii muhimu ionekane kwa wananchi”
tapatalk_1690813690362.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom