Chatanda azua tena mvutano CCM, Chadema Arusha

Chatanda azua tena mvutano CCM, Chadema Arusha

KOSA ni ccm kuongozwa na Makamba asiye na busara, elimu, na fisadi mkubwa. Sijui anangoza nani huko ccm. ameiua ccm.
 
Huyu mwanamama sijui tumfanyaje?
wewe Mary kuna nini Arusha mpaka uwasababishie mgogoro wenzako? Kwanini usiende kwenu Tanga ulipochaguliwa, ahaaaa! Unaboa sana wewe mwana mama
 
Huyu mwanamama sijui tumfanyaje?
wewe Mary kuna nini Arusha mpaka uwasababishie mgogoro wenzako? Kwanini usiende kwenu Tanga ulipochaguliwa, ahaaaa! Unaboa sana wewe mwana mama

Sijui ana security ya aina gani huyu mama. Inaelekea kuna mkubwa anambanjua ndiyo maana anakiburi na jazba.
 
Suala la arusha halitakiwi kuangalia kanuni au katiba au sheria za ccm au chadema.

Hapa inatakiwa kuangalia utu wa mtu na umwagaji damu ambao haurusiwi na vitabu vyote vya mungu.
Hata kama angekufa mtu wa ccm bado ni dhambi mbele za mungu kumbuka kaini alimuua abel na kumuzika kwa siri kubwa.!!!

Ccm na serikali waache kuwa na kauli za kibabe wala chadema wasichukulie mauaji hayo kama mtaji wa kisiasa bali kila mmoja wao ajitazame kwa makini akiwa peke yake mbele za mungu kama hana hatia!!!!

Kumbuka chadema hawawezi kulaumu ccm na ccm hawanauwezo wa kulaumu chadema hukumu mbele za mungu ni ya haki!!!

Wanadamu wanaweza kukuhukumu lakini mungu akakusamehe!!!
Nawasihi waliohusika katika ghasia hizo wakiwa kama viongozi wa seriakali ama jeshi la polisi ama siasa waache kutumia taalifa za intelejensia kama kigezo za kukwepa watbu haraka mbele za mungu kwa sababu wamemwaga damu isiyo na hatia. Hukumu ya mungu inakuja bila kujali urais wa mtu , hakuna ataye pona!!!
Damu ya waliouawa inamulilia mungu
 
KOSA ni ccm kuongozwa na Makamba asiye na busara, elimu, na fisadi mkubwa. Sijui anangoza nani huko ccm. ameiua ccm.
umetoka usingizini naona huji hata kinachozunguzwa! Issue hapa ni kama chatanda ana haki ya kuhudhuria vikao arusha, ww unaibuka na makamba umeitoa wapi
 
maelezo mazuri sana. Hivi ndo inabidi tujibizane kwa ufahamu wa kanuni, mazoea n.k. Katika maelezo umesema sheria inaruhusu mbunge wa VM kuchagua halmashauri ya kutumikia, ni sheria gani hiyo mkuu?

Polisi,

Unaweza kutumia vifungu hivi ambavyo viko kwenye taarifa ya katibu ya bunge baada ya kuombwa ufafanuzi.

Kulikuwa na madai mawili Arusha. CCM walikuwa wanapinga mama wa viti maalum CHADEMA asipige kura kuchagua meya kwasababu alikuwa hajaapishwa bungeni. Nafikiri ni wale mama walioteuliwa mwisho wakati bunge linafungwa. CHADEMA wao walikuwa wanampinga Chatanda kwamba ni mbunge viti maalum Tanga.

Madai yote mawili yalitupwa. Mbunge kama hajaapishwa haruhusiwi kushiriki majadiliano bungeni lakini anaruhusiwa kutimiza majukumu yake mengine yote kama mbunge. Hivyo alikuwa na sifa ya kushiriki kuchagua meya. Hivyo hivyo hilo dai la Chadema nalo likatupwa kwa sababu ambazo nimezieleza hapo juu.

Taarifa yenyewe ni kama hapa chini:

Naibu Katibu wa Bunge Bw. Eliakim P. M. Mrema alitoa ufafanuzi kwa barua yake Kumb. Na. CEB.77/155/01/79 ya Desemba 17, 2010, akiarifu kuwa kwa mujibu wa Kanuni ya 23 na 30(4) ya Kanuni za Bunge (2007); Ibara ya 59(1) na 66(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; kifungu cha 44, 81 na 86A(6) cha Sheria ya Taifa ya uchaguzi Sura ya 343 na kifungu cha 24(1)(d) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) sura ya 288 na Sheria Na.13 ya mwaka 2006, wabunge hao wawili ni wajumbe halali wa Halmashauri ya Manispaa ya Arusha baada ya kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kupangiwa na vyama vyao – Halmashauri ya Manispaa ya Arusha.
 
Wana JF

Jamani kuhusu hili suala la Chatanda wa viti maalumu ninaona linaanza kupotoshwa na hasa baada ya maelezo ya Tambwe Hiza. Wengi mmeanza kumfananisha Mary Chatanda na akina Grace na Lucy waliopiga kura ktk halmashauri ya Hai. Kwanza kabisa CDM hawana mfumo wa kuwapata wabunge wa VM kupitia mikoa kama CCM.

Baada ya kutokea kutoelewana ktk halmashauri ya Hai CDM waliomba maelezo kutoka kwa AG ni wapi wanastahiri kupiga kura, ndipo AG akaamua wanastahiri kupiga kura Hai. Kwa Mary Chatanda CCM hawakufanya hivyo kuomba ushauri wa kisheria kwa AG. CCM walitumia mambavu kuamua. Kwasababu walifahamu CCM wangeomba ushauri kutoka kwa AG walikuwa likely kushindwa kwasababu Mary amechaguliwa na UWT Tanga hivyo tayari amejifunga kwamba yeye atatumikia UWT Tanga na sio Arusha. Kama ni ukaribu anapofanyia kazi basi angeomba VM kupitia Arusha kwani alijua hilo tangia mwanzo.

Leo kama tume itaacha tu holela wabunge wa VM wa CCM wachague halmashauri za kupigia kura basi hakuna hata halmashauri moja ingeongozwa na CDM bse wako wengi wangeweza kuwagawa ktk halmashauri ambazo CCM ina madiwani wachache kuliko CDM na wakashinda.

Chatanda kama alichaguliwa VM kupitia mkoa wa Tanga inabidi akapigie kura huko, mbona ni yeye tu analeta vurugu hizi. Mfano Vicky Kamata ni mbunge viti maalumu kupitia wilaya ya Geita mkoa wa MZA mbona hakuja kupiga kura jimbo la Nyamagana kuikoa CCM ambayo ilikuwa na madiwani wachache!?

Pamoja na kwamba mahakama zote ni za CCM mimi naona CDM waende mahakamani wana nafasi ya kushinda au basi wamuulize AG Werema ingawa sina imani naye kwani huyu ni mmojawapo pamoja na Kombani waliokataa katiba mpya kabla ya bosi wao kuwaumbua.
 
Kosa ni la KATIBA,mwanasheria mkuu alishatoa maelezo.
 
Na Joseph Ngilisho,Arusha
Posted by GLOBAL on January 11, 2011 at 4:24pm

MBUNGE wa Viti maalum Tanga ambaye pia ni Katibu wa CCM MKoa wa Arusha, Mary Chatanda, anazidi kuvuruga watu, sasa baada ya kuwavuruga Chadema na CCM, ameanza kuwashambulia waandishi wa habari na kuwaita wahuni, huku akiwatishia kuwapiga bastola.

Hali hiyo ya kusikitisha imetokea , wakati Katibu huyo alipoitisha mkutano na waandishi wa habari, kwenye jengo la CCM Mkoa, ili kuelezea tamko la kamati ya siasa MKoa wa Arusha, kuhusina na vurugu zilizotokea januari 5 mwaka huu.

Akitoa tamko hilo alianza kwa kusema, anaipongeza serikali kwa kutumia vyombo vya dola yaani Polisi, kudhibiti wahuni kwa kutumia jeshi la Polisi, kisha akawageukia waandishi wa habari na kuanza kuwafukuza.

Waandishi waliofukuzwa na huku akiwatamkia maneno ya kashfa kuwa wameletwa sababu ya kufuata uchumi, ni mwandishi wa gazeti la Mtanzania, Fortunata Ringo, John Shija wa radio MJ, Rose JAkson wa radio Safina na Wankyo Ghati wa radio five na gazeti la Jamb oleo.

Aidha baada ya kuwafukuza hao, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha naye alilazimika kuingilia kati na kumsihi Katibu huyo awaache kwa kuwa waandishi ni kazi yao kuchukua habari.

Lakini Chatanda aliendelea kushikilia msimamo wake na kusema hapo siyo mahali pa kupata uchumi, watoke nje na waandishi hao walitoka nje ya jengo hilo.

NAye Adamu Ihucha wa gazeti la East Africa, akielezea kwa masikitiko, alisema yeye ni mmojawapo, alipoingia ndani ya kikao hicho, alimuuliza swali Mary Chatanda, kuwa kwanini wanapingana na IGP, kwa sababu IGP alisema kuna askari walitumia nguvu kubwa kupita kiasi na wewe unasema unawapongeza?

Mara baada ya swali hilo, Mary Chatanda aliingilia kati na kumkatisha huku akimkejeli mwandishi huyo kuwa, anamshangaa kuvamia mkutano ambao hakualikwa na alikuwa ametokea wapi.

"Hivi wewe umetoka wapi? Maana hatukujuwi, sisi tunazungumzia mambo yetu na kunyanyuka kutoka nje ya kikao" alisema Ihucha.

NAye Paul Sarwat wa gazeti la Raia Mwema, naye anasikitishw ana kauli za Katibu huyo na kusema awali, alishawahi kumfuata na kumtaka atoe ufafanuzi juu ya habari za CCM, lakini katibu huyo alimjibu kwa kejeli na kumwambia atamchapa makofi akiendelea kuandika habari za CCM.

Alisema Chatanda alimwambia kuwa yeye haoni habari za kuandika sipokuwa habari ni cCM tu, akiendelea atamchapa makofi.

Sarwat alisema kauli kama hizo zinazotolewa na kiongozi mkubwa wa ngazi ya juu ya Mkoa, zinasikitisha sana na zinapaswa kukemewa.

Akizungumzia kuhusu kauli za Mary Chatanda na kuwaukuza waandishi wa habari, MAkamu Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari, APC, Charles Ngereza, alisema yeye amesikitishw ana udhalilishaji wa Mary Chatanda dhidi ya wanahabari.

Alisema kuwa yeye kama kiongozi amekuwa akipata malalamiko ya mara kwa mara ya waandishi kutolewa vitisho na lugha chafu na Mary Chatanda, hivyo kama waandishi wanasikitika sana na hali hiyo ikiendelea italeta mvurugano mwingine kati ya CCM na waandishi wa habari.

Ngereza alisema kuwa mbali ya kuleta mvurugano, pia itahalalisha viongozi na watu wengine kuwadhalilisha waandishi na hiyo tayari imetokea kwa Polisi kuwakamata baadhi ya waandishi kama Musa Juma wa MWananchi, ambaye alikamatwa na Polisi na kupigwa, kasha kunywang'anywa Kamera na kulazimishwa kufuta Picha.

Alisema huo ni unyama na kuingilia kazi za waandhishi wa habari, ambao hawana mipaka na kazi zao, hivyo wanaomba serikali na viongozi wa juu, kuingilia kati na kuwakalisha viongozi wa Arusha, ili waheshimu uhuru wa wanahabari.
 
Hakuna ulevi mbaya kama ulevi wa madaraka, heri kulewa bangi itakuwehusha mwenyew lakini ulevi wa madaraka ni hatari kwa usalama wa raia namali zao kama ilivyotokea hukoArusha,huyu pashkuna Mary Chatanda amefika gatua mbaya mno. NGOMA IKILIA SANA KARIBU ITAPASUKA
 
Hilo jimama linapata wapi jeuri? Kuna mtu kawekeza hapo?
 
Nyie subirini tu .Makamba atakuja kumchukua kwa majonzi.
 
Ziko tetesi kuwa,CCM wamempeleka Zuhura Akbari Haji aka Merry Chitanda Arusha kwa sababu maalum za kuchunguza na kutafuta jinsi ya kuua upinzani pale.

Mama huyu ambaye anatumia jina la kikristo maalumu ili kuifluence na kupata huruma ya wananchi wa mikoa ya kaskazini ambao wengi wao ni wakristo ana historia mbaya sana

Kwanza jina lake halisi ni Zuhura Akbari Haji,na inasemekana ni raia wa Sudani Kusini katika kitongoji cha Kian katika jimbo la Warrap.Na alishiriki katika mauaji ya John Garang aliekuwa kiongozi wa SPLA Julai 30 2005

Merry Chatanda alisoma katika chuo cha Ujasusi Misri miaka ya 90 na kujiunga na mafunzo maalumu huko Urusi na Yugoslavia

Huyu mama ni hatari na CHADEMA mumuangalie vizuri hapa Arusha

kama kuna mtu ana details zaidi za huyu mama tafadhali azimwage hapa nitaendelea kuwapa jinsi nitakavyopata.
 
uhatari wake sijauona. kwa mtazamo wangu ni kuwa hana hata elimu kama Tambwe hiza.
 
Njoo na ushahidi timilifu huu bado hujani-convince
 
Back
Top Bottom