Charles Taylor found Gulity at The Hague

so hiyo court ina mipaka ipi? ni kwamba lazima kiongozi awe kaua wananchi wake pekee, au akiwa kaiba hela anashtakiwa pia au niaje...mipaka iko mpaka wapi...maana tuna akina mugabe, museven. hapa kwetu zenj walishaua watu, pale magomeni kulishatokea vurugu wananchi wakafa, arusha juzi juzi tu so nataka nijue vikwazo wanavovitumia huko hague kwenye kukamata na kushtaki viongozi. Kumbuka hawa viongozi wanaopelekwa huko ni wale ambao walishapigwa chini na wananchi wao so wanakua sio powerful tena...But having said that sioni haja ya kumkamata kiongozi wa nchi yetu aliyeua watu50 wakati kuna kiongozi wa marekani aliyeua watu zaidi ya 100000 na hakamatwi ndio kwanza anapeta huko texas:A S angry:



Taylor amekutwa na hatia ya kufadhili vikundi vya uasi kwa diamond smuggling, kuvunja haki za binadamu-sexual slavely,child soldiers. Kuhusu vigezo wanavyotumia ICC kumshtaki mtuhumiwa sina uhakika lakini kwanza lazima nchi iwe imesaini mkataba wao.
 
Wakuu nimekuwa nafuatilia hii kesi ya Taylor japo mimi sio mwanasheria lakini nimekuwa navutiwa sana na jinsi kesi inavyoendeshwa hasa defensive lawyer Courtenay Griffiths ni makini sana japo hii kesi kushinda si rahisi . Leo hukumu inasomwa live on CNN na Judge Richard Lussick japo yeye Taylor amekana mashtaka yote na kusema yeye ni mwathirika wa njama za wabaya wake.

Binafsi kwajinsi ya uhalifu na mauaji yaliyofanyika Sierra lione wakati wa utawala wake huyu jamaa ana kesi ya kujibu.
Malipo ni hapahapa duniani....huyu anahusika na vita vya Siera leone vilivyouwa maelfu ya watu na pia anahusika na
mauwaji ya Sajent Samwel Doe...ata akatae vipi!!!? niyeye ndiye alimtuma Prince Y.Johnson kumuua Samweli Doe
 
Taylor amekutwa na hatia ya kufadhili vikundi vya uasi kwa diamond smuggling, kuvunja haki za binadamu-sexual slavely,child soldiers. Kuhusu vigezo wanavyotumia ICC kumshtaki mtuhumiwa sina uhakika lakini kwanza lazima nchi iwe imesaini mkataba wao.

Taylor hajahukumiwa ICC, bali na special court for sierra leone kama mahakama Arusha ya mauji Rwanda.
 
kwa habari mpya zilizotoka hivi punde ni kwamba rais wa zamani wa liberia amekutwa na makosa na adhabu yake itatangazo wk ijanyo.
Presiding Judge Richard Lussick
said the 64-year-old warlord-turned-president provided arms, ammunition, communications equipment and planning to rebels responsible for countless atrocities in the 1991-2002 Sierra Leone civil war and was repaid by the guerrillas in so-called "blood diamonds" mined by slave laborers. Lussick called the support "sustained and significant."
"Mr. Taylor, the trial chamber unanimously finds you guilty" of 11 charges, including terror, murder, rape and conscripting child soldiers, Lussick told Taylor.
 
Wondering why Taylor's trial was conducted by special court for sierra leone and not ICC (permanent tribunal) for crime against humanity? Msaada wanasheria.



Mimi si mwanasheria ila nadhani wamefanya ili kuruhuru 'combination ya Laws' za International na za Sierra leone na kuondoa biasness.

MahakamaMaalum ya Sierra Leone ilianzishwa Januari 16, 2002, chini ya mkataba kati yaUmoja wa Mataifa na serikali ya Sierra Leone. Ni imara na inahukumu watuhumiwawa uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu na ukiukwaji wa sheria za kimataifa. Mahakama Maalum yaSierra Leone hutofautiana na mahakama nyingine za kimataifa kama vile: Mahakamaya Kimataifa ya Yugoslavia ya Zamani (ICTY) na Rwanda (ICTR) na ya Kimataifa yaMakosa ya Jinai (ICC). Mahakama Maalum ni mahakama ya mseto kwamba inafanyamchanganyiko wa kimataifa na Sierra Leone ndani ya sheria, pamoja na mchanganyikowa kimataifa na Sierra Leone wawafanyakazi wake. Miongoni mwa majaji kumi na moja wa Mahakama Maalum, sabawalichaguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati nne walichaguliwa naSerikali ya Sierra Leone. Kati ya majaji hao, watatu ni wa Sierra Leone,walioteuliwa na Serikali ya Sierra Leone. Kadhalika, Mwendesha mashtakaaliteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati Naibu Mwendesha Mashitaka,Sierra Leone, aliteuliwa na Serikali ya Sierra Leone.
 
Marekani wajanja, wao mpaka Leo hawajasaini statute inayotambua mahakama ie ICC, kwa Hali hiyo bush hawezi kushitakiwa. Viongozi wetu walirubuniwa na vihela wakasaini haraka haraka. Kumbe wao ni potential victims.

Wajanja ama Wanafiki/Mahabithi?

Kila neno lina maana na upeo wake kamilifu. Ujanja ni halali na huweza kuleta faida kwa binadamu na huweza kurahisisha mambo yaliyo, venginevyo, ni magumu kuyatekeleza. Mjanja haadhibiwi isipokuwa ujanja wake huelekezwa kufaidisha watu. Unafiki na Uhabithi ni haramu na hauleti isipokuwa ufisadi, fitna, chuki na umwagaji damu kwa binadamu. Mnafiki anatakiwa aadhibiwe.

Marekani na washirika wake ni Wanafiki/Mahabithi wenye maguvu tu, sio Wajanja. There is NO tricks whatsoever of what they do, it is very predictible hypocrisy. Hivyo wanapoadhibiwa ki-ujanja ujanja na Wajanja wasio na nguvu, katika namna waijuayo na iliyo ndani ya uwezo wa Wajanja wasio na nguvu, basi wanastahili.

Tatizo ni nyiyi mnaobadilisha lugha, Wanafiki/Mahabithi mnawaita wajanja, na wajanja mnawaita Magaidi kwasababu Wanafiki/Mahabithi wamewaita na kukulazimisheni kuwaita hivyo. Mungu atupe maisha marefu kidogo, utawaona Wanafiki/Mahabithi wataporomoka na Wajanja watanyanyuka.
 
Wajanja ama Wanafiki/Mahabithi?

Kila neno lina maana na upeo wake kamilifu. Ujanja ni halali na huweza kuleta faida kwa binadamu na huweza kurahisisha mambo yaliyo, venginevyo, ni magumu kuyatekeleza. Mjanja haadhibiwi isipokuwa ujanja wake huelekezwa kufaidisha watu. Unafiki na Uhabithi ni haramu na hauleti isipokuwa ufisadi, fitna, chuki na umwagaji damu kwa binadamu. Mnafiki anatakiwa aadhibiwe.

Tatizo ni nyiyi mnaobadilisha lugha, Wanafiki/Mahabithi mnawaita wajanja, na wajanja mnawaita Magaidi kwasababu Wanafiki/Mahabithi wamewaita na kukulazimisheni kuwaita hivyo. Mungu atupe maisha marefu kidogo, utawaona Wanafiki/Mahabithi wataporomoka na Wajanja watanyanyuka.


kwahiyo magaidi wale wanaojilipua na kuua watu wasio na hatia ktk masoko na mikusanyiko ni wajanja na matendo yao huleta faida kwa wanadamu?? aisee...
 
Wamarekani walijua haya wajiepusha nayo, ukweli ni kwamba serikali zote ni ovu sema zinatofautiana viwango tu vya uovu
jamani mfuatilien Taylor vzuri,alipandkizwa na USA kule,ni CIA,labda kwa vile wamarekani ndo zao wakishakutumia wanakutupa kama kondom
 
de993_7fefe8e7489e8e0a48a15b2320b7.jpg



charlestaylor3-590x900.jpg



par2003081049571.jpg

 
Zimesomwa facts za kesi na kwamba mahakama imemkuta na hatia ya makosa lakini hukumu ya adhabu haijatolewa bado,

Sashel,

Kwa ruhusa yako naomba niweke sawa hili jambo. Hukumu imesomwa, hukumu ni uchambuzi wa kesi kuanzia makosa anayobaliana ushahidi uliotolewa na pande zote,uchambuzi wa ushahidi huo kulingana na sheria zilizopo na mwisho ni kutoa uamuzi wa mahakama kuwa mshtakiwa ana hatia au la, hii Ndio hukumu. Kwa kilichotokea Leo the Hague ni hukumu ya mshtakiwa Kukutwa na hatia.

Adhabu, ni pale mahakama inapoketi baada ya kumpata Mtu na hatia na kutamka adhabu Muafaka baada ya kuzingatia shufaa ambazo upande wa mashitaka na utetezi watatoa.

Kisheria hakuna neno hukumu ya adhabu
 
Back
Top Bottom