simplemind
JF-Expert Member
- Apr 10, 2009
- 16,409
- 9,183
Judge anasoma hukumu Hague
Wakuu nimekuwa nafuatilia hii kesi ya Taylor japo mimi sio mwanasheria lakini nimekuwa navutiwa sana na jinsi kesi inavyoendeshwa hasa defensive lawyer Courtenay Griffiths ni makini sana japo hii kesi kushinda si rahisi . Leo hukumu inasomwa live on CNN na Judge Richard Lussick japo yeye Taylor amekana mashtaka yote na kusema yeye ni mwathirika wa njama za wabaya wake.
Binafsi kwajinsi ya uhalifu na mauaji yaliyofanyika Sierra lione wakati wa utawala wake huyu jamaa ana kesi ya kujibu.
huyu na george w bush wana tofauti gani? mbona bush hawajamkamata? give me a break!!! waonevu tu hao
Kwa jinsi ushahidi unavochambuliwa na kuhusishwa na Taylor namini kabisa hata yale mauji Zanzibar yakifanyiwa special court kama hii ya sierra Leone atrocities kweli hapatoki mtu.
Taylor ana kesi ya kujibu,sentencing may 30.
Jahazi lake linazama, haponi kabisa.
Ushahidi hauko vizuri sana upande wake.
Viongozi wetu matumbo Yao ya moto, Aliyofanya Taylor na makosa yanayomkabili, ushahidi unavyochambuliwa ni Kama ambavyo viongozi wetu wanafanya.
ICC itapata wateja wengi sana.
Marekani wajanja, wao mpaka Leo hawajasaini statute inayotambua mahakama ie ICC, kwa Hali hiyo bush hawezi kushitakiwa. Viongozi wetu walirubuniwa na vihela wakasaini haraka haraka. Kumbe wao ni potential victims.
Amepatikana na hatia. Kuwa na kesi ya kujibu ni pale upande wa mashitaka ukimaliza kutoa ushahidi basi mahakama inabidi ichambue ushahidi kuona Kama ushahidi huo umejenga kesi kumfanya mshtakiwa ajitetee
Mshtakiwa akijitetea nod mahakama unaweza sema amstakiwa ana hatia au la.
huyu na george w bush wana tofauti gani? mbona bush hawajamkamata? give me a break!!! waonevu tu hao
Wamarekani walijua haya wajiepusha nayo, ukweli ni kwamba serikali zote ni ovu sema zinatofautiana viwango tu vya uovu
Sio uonevu hii inaitwa Justice, kusema kwamba Taylor asihukumiwe makosa yake kwasababu Bush nae ana makosa hiyo hoja haina uhai
Hivi Christopher Mtikila hawezi kufungua kesi huku, maana yeye ni mzee wa Kesi. Ila siku hizi ni kimya kabisa, amelishwa nini? Yamini au? Wenye taarifa zake watupatie wakuu.