Chapa ya Mpinga Kristo nyuma ya Worldcoin na Crypto currency, AI robot

Surya

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
8,378
12,573
Kabla sijaenda kwenye lengo kuu la mada hii nielezee kwanza Worldcoin ni nini ?
Cypto/Cryptocurrency ni nini ?
na mahusiano yake na AI robot.

Baadhi ya member wa JF nimeona wakigusia mada hii kwa sehemu ndogo..

Worldcoin ni nini?

Worldcoin ni jukwaa la utambuzi wa kidijitali ambalo linalenga kumpa kila mtu duniani njia rahisi ya kuthibitisha kuwa yeye ni binadamu halisi na si roboti au algoriti ya AI.

Kitambulisho cha Dunia

World ID, ambayo kampuni inadai itawawezesha watumiaji "kuthibitisha ubinadamu wao" mtandaoni huku wakidumisha faragha yao. Kinachojulikana kama "uthibitisho wa utu" huundwa na kifaa cha skanning ya iris(Jicho) kinachoitwa Orb.

Kama vile alama za vidole, muundo wa iris wa kila mtu ni tofauti. Orb huchanganua iris ya mtumiaji na kutumia muundo wake kuunda msimbo wa kipekee wa utambulisho unaoitwa IrisCode. Nambari ya kuthibitisha haihusiani na maelezo ya kibinafsi ya mtumiaji - inapatikana tu ili kuzuia watu kupata zaidi ya Kitambulisho kimoja cha Dunia.

Lengo la Worldcoin ni nini?

Kukabiri ulimwengu wa mtandaoni mnamo 2023. Tovuti nyingi zinahitaji kuingia na nenosiri. Walaghai wana kila aina ya mikakati ya kukufanya ubofye viungo na kuwatumia pesa.

Na kutokana na kuongezeka kwa AI robot, uwezo wetu wa pamoja wa kutambua nani ni binadamu mtandaoni na nani sio unakaribia kuwa mbaya zaidi. Mapema mwaka huu, GPT-4 ya OpenAl iliweza hata kumshawishi mwanadamu kutatua CAPTCHA- teknolojia iliyoundwa kutofautisha wanadamu kutoka kwa roboti kwa niaba yake.

Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa AI robot, Sam Altman anawajibika kwa matatizo kama haya. Worldcoin, basi, hutumika kama suluhisho lake kama njia ya kutofautisha kwa hakika kati ya wanadamu na AI. Iwapo wanadamu wote mtandaoni wangeweza kuthibitisha kwamba kwa hakika wao ni wanadamu, basi ulaghai na walaghai wangepungua sana.

Kwa nini watu wanajiandikisha?

Worldcoin ilizinduliwa rasmi mwezi Julai, na mradi unaanza ziara ya kusajili miji mingi. Altman alichapisha video ya mistari mirefu nje ya vituo vya Orb, na akasema kuwa mradi huo ulikuwa unachanganua mtumiaji mpya kila sekunde nane.

Baadhi ya watu wamejiandikisha kwa ajili ya udadisi au ushirika wa teknolojia. Lakini wengi zaidi, inaonekana, walijiandikisha kwa sababu rahisi ni kupata pesa ambazo ni bonus kwa mtu yeyote ambaye alichanganua macho yake kwenye orb.

Kipengele cha cryptocurrency cha Worldcoin kinatumika kama mbinu ya uuzaji, miundombinu ya kifedha ya kimataifa.

Kwanini Worldcoin inakabiliwa na ukosoaji?

Wakosoaji wengi wameita biashara ya Worldcoin ya kukagua mboni kwa kubadilishana na Crypto Currency. na wengine wameilinganisha na hongo. Watu wengi wanasitasita kwa kueleweka kusalimisha data zao za kibayometriki kwa kampuni ya kibinafsi ya kuanzisha faida kwa malengo yasiyo na uhakika.

Hadi hapo itakua rahisi kila mtu kuelewa nini kinaendelea.

Worldcoin ni Digital Identity
Crypto currency ni Digital currency - fedha ya kidigitali

Jambo hili ni Lazima litafanikiwa.
Kwasababu njia rahisi ya biashara duniani ni lazima utumie fedha ya kidigitali. Kwa kasi kubwa sasa duniani katika nchi zilizoendelea watu hawapokei tena fedha mkono.
Pia Credit card za benki zimezidi kuwa na usalama mdogo sana wa kulinda fedha za wateja wake, camera za kisasa zimekua na uwezo mkubwa wa kuiba namba siri ambazo zinapatikana katika card ya benk ya mteja na kuweza kufanya wizi wa fedha. Hata uwe kwenye gari na lipo kwenye mwendo wa kasi bado camera zinaweza kunasa taarifa zako za kibenk katika card.

Sasa watu wanaanza kuamia katika fedha za kidijitali ambazo utaweza kutumia popote nchini kwa usalama zaidi.
Ukiwa china leo hii na Card yako ya CRDB basi utateseka sana.😂😂

Mpinga kristo.
Ufunuo wa Yohana 13:16-17
[16]Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;
[17]tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.

Sasa ufunuo huu umetimia katika maisha ya binadamu na umeanza kufanya kazi.

Video zipo nyingi YouTube.
Chip ndogo kama punje ya mchele inawekwa katika mkono
Screenshot_20230816_123349_YouTube.jpg

Chip hiyo itabeba...
i. ID yako ambayo utaipata kwa kutuma au kutizamwa muonekano wa mboni la jicho lako (Iris)
ii. Funguo au Get pass
iii. Wallet.

Hutahitaji kutembea na Card ya benk wala Simu, ukiwa uchi tu unakimbia na utajiri wako 😂😂

Maswali ya kujiuliza..
Je chip hiyo itakuwa na uwezo gani wa siri katika mwili wa binadamu ?

AI robot ambao wanakuja kurahisisha maisha ya binadamu kwa kiasi kikubwa ni Computer yenye sura na muonekano wa binadamu.
Na sasa Neurolink za Artificial intelligence zimeweza kupandikizwa kwa binadamu na binadamu kuwa na uwezo wa muingiliano mkubwa na AI robot.

AI robot ataweza kumjua au kuingiliana zaidi na binadamu, ataongoza hisia na maamuzi ya binadamu kwa binadamu kuwekewa chip.
Inasemekana chip hiyo itamsaidi binadamu kuondokana na msongo wa mawazo kabisa na kutokujitambua.
Fikra za binadamu zitaweza kuongozwa na AI (your will, Action and Emotion ambazo hutoka nafsini mwa mtu)

Ufunuo wa Yohana 14:9-11
[9]Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake,
[10]yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.
[11]Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake.
 
Mbona kwenye Dollar ya Marekani kuna eye of Providence ambayo mnasema ni Masonic symbol?

1692205018997.png


Uliwahi kuona kuna Pastor au Sheikh anapinga matumizi ya hiyo hela?

Sasa jaribisha kuwapelekea sadaka yako kwa mfumo wa dollar

Ila hiyo Dollar isiwe na hicho kijicho pamoja na piramidi afu wakikuuliza imekuaje waambie hiyo yako ndio halali kwasababu haina mambo ya kishetani.
 
Mbona kwenye Dollar ya Marekani kuna eye of Providence ambayo mnasema ni Masonic symbol?

View attachment 2719176

Uliwahi kuona kuna Pastor au Sheikh anapinga matumizi ya hiyo hela?

Sasa jaribisha kuwapelekea sadaka yako kwa mfumo wa dollar

Ila hiyo Dollar isiwe na hicho kijicho pamoja na piramidi afu wakikuuliza imekuaje waambie hiyo yako ndio halali kwasababu haina mambo ya kishetani.
Dunia inaenda kasi saivi
 
Ufunuo wa Yohana 13:16-17
[16]Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;
[17]tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.
Aliyeandika biblia alikuwa na unabii
 
kila panapotokea uvumbuzi mkubwa wa kiteknolojia, kuna watu wanaona ni mambo ya kishetani, ila ni sayansi tu.... watu wameanza kutabiri mwisho wa dunia tokea zamani sana ila hawafanikiwi, wewe sio wa kwanza
Kinachonishtua hata sio watu kutabiri.. kinachonishutua ni jinsi gani binadamu atakuwa undercontrol na computer.

Binafsi sikuwa interested kabisa kufatilia au kusoma tu mambo haya.
Lakini AI robot zimenistua sana ufanisi wake mkubwa na jinsi gani maisha yanaenda kuwa mepesi.
Dunia ikiongozwa na hivo viumbe ni rahisi sana dunia kuongozwa na serikali moja.
Na shetani akitaka usiuze wa kununua bila ruhusa yake anahitaji Mtu mmoja tu kufanyanae agano.
 
Kabla sijaenda kwenye lengo kuu la mada hii nielezee kwanza Worldcoin ni nini ?
Cypto/Cryptocurrency ni nini...
Hata umeme ulipogunduliwa walisema ni nguvu za shetani. Endeleni kusambaziana ujinga.
 
Back
Top Bottom