Chanzo cha mauaji ya mfanyabiashara ni hela

Chanzo cha mauaji ya mfanyabiashara ni hela

Nani alikuwa na marehemu kabla hajauwawa ambaye wali hesabu wote zile hela?acheni ushabiki wa ajabu ajabu,marehemu alimjeruhi polisi kituoni kwa hasira za gari lake kukamatwa,kisha akaimbilia kwake,alikuwa amelewa na confused,akaenda kwa jirani akakwapua combat,alipoona nyumba imezingirwa akajipiga risasi tumboni,mkewe aliruka na kumkumbatia akimbembeleza asijue,yeye aakmuamrisha mkewe aondoke mara moja ama sivyo atamuuwa,kitendo cha mkewe kumpa nafasi akajiongeza ya pili usoni.Suala la risasi mbili au tatu mwilini sio issue,inategemea amejipiga wapi.Kama angekuwa na matundu mawili ya risasi kichwani then hio ni habari nyingine,lakini tumboni alafu kichwani ni kitu cha kawaida.Mimi sitetei polisi ila tu nawashangaa mnajadili sana bila kuulizia maendeleo ya askari aliyepigwa risasi kadhaa na marehemu,bila shaka angeuwawa polisi mgesema ni sawa
Uko makao makuu au wamekuhamishia Mtwara afande!?
Mwili umekutwa na matundu ya risasi mbili tumboni na risasi kichwani. Hivi unajua shock mwili inayopata ukijipiga au kupigwa risasi mwilini? Let alone kujipiga risasi mbili tumboni halafu bado ukawa na nguvu ya kujipiga risasi ya kichwa!!! Lini umeshawahi kusikia mtu aliyetaka kujiua akajipiga risasi tatu??? Tumia akili kuchanganua habari Usilete stori za kitoto hapa ukafikiri wote ni wapu.uzi. Kama umezoea kutumia mshale,nenda kaulize vizuri wanaoelewa matumizi ya silaha za moto..."Eti kajipiga risasi ya tumbo na akamuamrisha MKE wake aondoke mara moja AMA sivyo atamuua" unafikiri movie ya kihindi hiyo. Mwili umekutwa na matundu mawili tumboni na moja kichwa ya risasi.Au alikuwa anatumia risasi FEKI kutoka China. Jipange Afande.

Jinsi ulivyoandika habari yako wewe mwenyewe unajikanyaga hujui hata unaongelea nini. Jipange urudi upya.
 
Nani alikuwa na marehemu kabla hajauwawa ambaye wali hesabu wote zile hela?acheni ushabiki wa ajabu ajabu,marehemu alimjeruhi polisi kituoni kwa hasira za gari lake kukamatwa,kisha akaimbilia kwake,alikuwa amelewa na confused,akaenda kwa jirani akakwapua combat,alipoona nyumba imezingirwa akajipiga risasi tumboni,mkewe aliruka na kumkumbatia akimbembeleza asijue,yeye aakmuamrisha mkewe aondoke mara moja ama sivyo atamuuwa,kitendo cha mkewe kumpa nafasi akajiongeza ya pili usoni.Suala la risasi mbili au tatu mwilini sio issue,inategemea amejipiga wapi.Kama angekuwa na matundu mawili ya risasi kichwani then hio ni habari nyingine,lakini tumboni alafu kichwani ni kitu cha kawaida.Mimi sitetei polisi ila tu nawashangaa mnajadili sana bila kuulizia maendeleo ya askari aliyepigwa risasi kadhaa na marehemu,bila shaka angeuwawa polisi mgesema ni sawa

Wewe ulikuwepo wakati haya yakitendeka? Kwa sababu ulivyoelezea kwa ufasaha ni kama wewe ndie mke wa marehemu. Mbona ndugu wa karibu wamekataa kuwa alijiua? Au umetumwa na polisi kuja kueneza uongo baada ya kuona ukweli unaanza kujulikana? Au wewe ni mmoja katika wale waliomuuwa? Nina mashaka makubwa na wewe. Lazima zitumike njia za kukujua wewe ni nani pengine tunaweza kugundua siri kubwa,
 
Kwa nini mtu unakaa na cash nyingi hivi nyumbani?? Milioni 300???

Hivi Geita hauna Benki?

Inawezekana alikuwa kauza mzigo kwa taslimu, alikuwa kwenye process ya kwenda benki. Kuna mambo mengi sana kwenye biashara. Huwezi jua
 
Kwa karne hii hufai kufanya hivyo hata kama una hela zimejaa dunia nzima, sehemu ya kutunzia zipo zimejaa tele kwa nini ku - risk?
Ya nini na kwa mahitaji gani uweke 300 ml home?

na Lucy Ngowi

MBINU mpya ya wizi wa fedha katika mabenki unaofanywa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kompyuta, umeibuka jijini Dar es Salaam na benki kadhaa zimeshakumbwa na wizi huo.

Kutokana na hali hiyo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, amewatahadharisha wenye mabenki kuwa makini wakati polisi imeanza kufuatilia mtandao wa wizi huo.

Manumba alitoa tahadhari hiyo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, kuhusiana na matukio ya aina hiyo yaliyotokea siku za karibuni katika baadhi ya benki nchini, hususan jijini Dar es Salaam.

Alisema aina hiyo ya wizi ni ngeni nchini na wahusika wanaweza kuchota fedha nyingi kuliko wizi uliozoeleka wa kughushi hundi, saini au ule unaofanywa kwa kuvamia na kupora kwa nguvu kwa kutumia silaha za moto.

“Nawatahadharisha wenye mabenki kuwa wizi wa sasa unatokana na matumizi ya kompyuta ambayo hayaepukiki, wizi huo unaweza kuhamisha fedha nyingi kutoka akaunti moja kwenda nyingine na kuzichukua bila wahusika kujua.

“Uchunguzi wa awali umebaini kuwa wizi huo una mahusiano kati ya wezi wa nje na wafanyakazi wa mabenki ambao si waaminifu. Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na menejimenti za mabenki, vyombo vingine vya usalama na wananchi, tunaendelea kufuatilia kwa karibu aina hiyo ya wizi,” alisema Manumba.

Moja ya hatua zilizochukuliwa na polisi ni kujua namna ya kudhibiti wizi huo ili fedha za wananchi zisiingie katika mikono ya wahalifu. Pia kuwatia nguvuni wahalifu hao na kuwachukulia hatua za kisheria.

“Jeshi la Polisi linawaomba wananchi watoe ushirikiano kuwapata wahalifu hao ili wizi wa aina hiyo uishe. Watuhumiwa wa wizi huo wapo wengi lakini hatujawakamata, tunaendelea na uchunguzi,” alisema.

Alisema wizi huo umeanza kujitokeza zaidi kuanzia mwaka jana. Majambazi hayo ya mtandao wa kompyuta yalifanikiwa kuwashawishi baadhi ya wafanyakazi wa benki na watu wa kupitisha fedha hizo kwenye akaunti zao. Matukio hayo yamejitokeza zaidi katika benki za Barclays na CRDB, na kuwa wizi huo unafanyika zaidi Dar es Salaam kwa sababu ni jiji kubwa na lenye mabenki makubwa.

Kwa mujibu wa mkurugenzi, Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wake, hivyo hakutaka kutaja baadhi ya majina ya watu wanaotuhumiwa kuhusika na matukio yao kwa hofu ya kuvuruga uchunguzi.

Alitoa tahadhari kwa uongozi wa benki kutambua kuwa kuna wizi wa aina hiyo, hivyo wachukue tahadhari kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuudhibiti wizi huo. Pia aliwataka viongozi wa benki kufuatilia nyendo za wafanyakazi wao kwa sababu wizi huo hauwezi kutendeka bila kushirikiana na wafanyakazi hao.

Kwa upande wa wananchi, Manumba aliwataka kutambua kuwa wana jukumu la kulinda mali za nchi kwa kuwa fedha zinazoibwa ni za wananchi wa Tanzania.

Wiki chache zilizopita, iliripotiwa kuwa kikundi cha watu wachache walichukua sh bilioni 5, mali ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), zilizokuwa ni malipo ya kawaida kwenda Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kwa mujibu wa taarifa hizo, fedha hizo ziliingizwa kwenye akaunti mbalimbali ikiwamo akaunti ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA). Ziliingizwa zaidi ya sh milioni 671 kwenye akaunti yao iliyopo katika benki ya CRDB, tawi la Lumumba, bila wahusika kujua.

Ilielezwa kuwa fedha hizo hazikuwa za TUCTA wala chama chochote chenye uhusiano na TUCTA, na hawajawahi kufanya biashara yoyote na TTCL kuweza kulipwa kiasi hicho cha fedha.

Kwa mujibu wa habari hizo, TUCTA haijawahi kuwa na bajeti inayofikia kiasi hicho cha fedha, lakini inadaiwa kuna uwezekano wa mfanyakazi mmoja au zaidi walioshirikiana na mtandao huo wa ujambazi wa kisasa, kuziingiza fedha hizo katika akaunti hiyo na kuzitoa kinyemela.
 
Kwa nini mtu unakaa na cash nyingi hivi nyumbani?? Milioni 300???

Hivi Geita hauna Benki?

Ni kwaida ya wabongo kukuza mambo, watu wanaishi na mitambo ya kufyatua uongo. Usishangae hata milion kumi hazifiki watu wanataka warudishiwe 300.
 
Nani alikuwa na marehemu kabla hajauwawa ambaye wali hesabu wote zile hela?acheni ushabiki wa ajabu ajabu,marehemu alimjeruhi polisi kituoni kwa hasira za gari lake kukamatwa,kisha akaimbilia kwake,alikuwa amelewa na confused,akaenda kwa jirani akakwapua combat,alipoona nyumba imezingirwa akajipiga risasi tumboni,mkewe aliruka na kumkumbatia akimbembeleza asijue,yeye aakmuamrisha mkewe aondoke mara moja ama sivyo atamuuwa,kitendo cha mkewe kumpa nafasi akajiongeza ya pili usoni.Suala la risasi mbili au tatu mwilini sio issue,inategemea amejipiga wapi.Kama angekuwa na matundu mawili ya risasi kichwani then hio ni habari nyingine,lakini tumboni alafu kichwani ni kitu cha kawaida.Mimi sitetei polisi ila tu nawashangaa mnajadili sana bila kuulizia maendeleo ya askari aliyepigwa risasi kadhaa na marehemu,bila shaka angeuwawa polisi mgesema ni sawa

Tatizo ni kwamba watanzania wa kawaida tumepoteza imani kabisaa na hili jeshi la polisi! ndio maan kila watakachosema tunaona ni sinema tu! jaribu kutembelea maeneo hayo jichanganye na hao raia uone hao polisi wanavyonyanyasa raia wakitafuta pesa kwa nguvu! Kilio chetu walalahoi ni kuitaka serikali iunde upya jeshi hilo kwani wakiliacha hivi lilivyo basi watakuja kuona uasi wa raia na kuitumbukiza nchi kwenye janga!
 
jamani issue ya kuuwa kwa mwananchi kwa kisa cha kupora pesa yake tena kikifanywa na jeshi la polisi kwa usimamizi wa rpc si la kuleta mizaha eti kwa nini alikuwa na hela yote hiyo nyumbani.

Swala la polisi kuua halafu rpc anawasaidia kutoa statment ya kuwasaidia wauaji eti mfanyabiashara aliamua kujiua eti baada ya kudhani ameua polisi, inakuwaje mtu anayeamua kujiua ajipige risasi mbili sehemu tofauti za mwili yaani tumboni na kichwani na kisha pesa mil.300 zipotee kwa sintofahamu wakati hapakuwa na majambazi?

Na kwa ushahidi wa wazi kuwa rpc amehusika ni pale alipotakiwa kutoa kauli baada ya ndugu wa marehemu kukataa kuzika na kujibu eti anapanga kutoa statment baada ya kujipanga na kupanga uongo leo saa 8 mchana. Hapa inaonekana katika hiyo tsh. 300mil na hivyo lazima adanganye umma.

Ndugu zangu mimi binafsi linapokuja swala la kutegemea wakuu wa mapolisi ma rpc kutoa kauli haraka haraka baada ya matukioa mie huwa siwezi kuamini haraka haraka, kumbukeni wakati wa tukio la ditopile mzuzuri kuuwa konda wa daladala, tibaigana alisema kwamba tiba alisema dito alikuwa anajaribu kupiga piga kioo, pia kumbukeni hadi leo rpc iringa bwana kamhanda hadi leo anakula bata wakati alisimamia mauaji ya mwangosi.

mimi nilitia mashaka taarifa ya polisi ya awali.kwamba aliingia ndani ya nyumba na kuvaa nguo za jeshi za askari aliyekuwa likizo,alijuaje kwenye nyumba hiyo kuna askari aliye likizo na anasare za jeshi?.pili ni kufanya postmoterm kuona alipigwa risasi au alijiua?. Polisi wanatumia rifle na smg na kama alijiua kwa kutumia pistol mapigwa ya risasi ni tofauti.kwa kifupi polisi walimlipua na wananchi simameni kidete kusimamia haki.
 
Nani alikuwa na marehemu kabla hajauwawa ambaye wali hesabu wote zile hela?acheni ushabiki wa ajabu ajabu,marehemu alimjeruhi polisi kituoni kwa hasira za gari lake kukamatwa,kisha akaimbilia kwake,alikuwa amelewa na confused,akaenda kwa jirani akakwapua combat,alipoona nyumba imezingirwa akajipiga risasi tumboni,mkewe aliruka na kumkumbatia akimbembeleza asijue,yeye aakmuamrisha mkewe aondoke mara moja ama sivyo atamuuwa,kitendo cha mkewe kumpa nafasi akajiongeza ya pili usoni.Suala la risasi mbili au tatu mwilini sio issue,inategemea amejipiga wapi.Kama angekuwa na matundu mawili ya risasi kichwani then hio ni habari nyingine,lakini tumboni alafu kichwani ni kitu cha kawaida.Mimi sitetei polisi ila tu nawashangaa mnajadili sana bila kuulizia maendeleo ya askari aliyepigwa risasi kadhaa na marehemu,bila shaka angeuwawa polisi mgesema ni sawa

Kama mazingira ni hayo kuwa kajiua kwa nini RPC alikuwa anazuia mwili usipelekwe kufanyiwa uchunguzi Geita,
ila analazimisha upelekwe mochwari Runzewe na akalazimisha kuwashusha mke wa marehemu na ndugu wengine
kwa nguvu kwenye gari waliyokuwemo na kupakiwa kwenyue gari yake na akawapeleka kituoni.alikuwa anaficha
nini?
 
Sio kwa Bank system ya kiTanzania na Network issues. Hata iwe karne gani Tanzania bado tuko nyuma katika masuala ya Banking. Suala sio sehemu za kutunzia pesa Kibweka. Suala ni upatikanaji wa hela yako kwa haraka pindi utakapohitaji kwa emergency au suala la kibiashara.

Kama nilivyoelezea mwanzo Kutokana na aina ya biashara Marehemu aliyokuwa anafanya hakuna cha ajabu kuwa na pesa hiyo karibu. Tatizo letu Watanzania wengi tumezoea kukremu na kucopy mpaka kwenye maisha yetu ya kila siku...wakati system yetu hapa nchini haijafikia huko. Biashara ya madini sio Kama biashara ya kuuza nguo Kariakoo.
Mimi najaribu kuwasaidia ili muelewe kabla ya kuanza kujudge ulimbukeni wa Marehemu.

...Mkuu, hata bila ya Hayo yote! Kwa Usalama gani ulio huko Bank?? Mtu unaenda ku-draw Milioni 300 hao hao makarani wa Benki ndio watawapigia simu 'Watendaji' ambao utawakuta wanakusubiri barabarani na kuchukua chao?? Mara ngapi tumeishasikia mtu kaenda peke yake Banki kuchukua hela zake nyingi tu na aakaishia kuporwa na majambazi barabarani?? Kwani hawa majambazi pia ni Wanajimu wa kujua nani ataenda kuchukua hela nyingi Banki leo? Ukweli ni kwamba hakuna mahali pa salama pa kutunzia pesa yako. Si benki si Polisi. mwisho wa Siku ni afadhali uiweke tu sandukuni halafu upunguze Mdomo!!!!
 
Kutokana na aina ya biashara aliyokuwa anafanya hakuna cha ajabu hapo. Wafanyabiashara wengi wa madini huwa wanakuwa na pesa Kama hizo au zaidi nje ya mabenki. Ukiletewa mzigo usiku wa milioni 20 utafanyaje na huku mabenki yanakuwa yamefungwa. Mara nyingi hao wauzaji wadogo wadogo wanataka hela hapo hapo hamna habari ya njoo kesho uchukue hela.

Hamna cha ajabu kwa mfanyabiashara wa aina hiyo kuwa na kiasi Kama hicho nyumbani kwake au ofisini. Benki ni wasumbufu sana haswa mikoani...kuna watu wananielewa namaanisha nini hapa
.

huna unachomaanisha zaidi ya upuuzi,300m unaweka chumbsni,aingii akilini
 
huna unachomaanisha zaidi ya upuuzi,300m unaweka chumbsni,aingii akilini[/QUOTE]

Kwani mimi ndio niliyekuwa na hiyo Milioni 300 chumbani mpaka mwerevu wewe ukaniona Mpuuzi!?
Yeye Mwenye pesa zake aliona ni busara kuwa nayo chumbani, wewe ni nani kumpangia jinsi ya kutunza pesa zake!?
Hongera mwerevu wewe kwa kutokuingia akilini kwamba karne hii kuna wafanyabiashara wanakuwa na pesa kiasi hicho majumbani.

Itaingiaje akilini kwa mtu Kama wewe ambaye hauna hata Tsh.50,000 kwenye akaunti yako ya benki...Kama unayo hata hiyo akaunti.
 
Sio kwa Bank system ya kiTanzania na Network issues. Hata iwe karne gani Tanzania bado tuko nyuma katika masuala ya Banking. Suala sio sehemu za kutunzia pesa Kibweka. Suala ni upatikanaji wa hela yako kwa haraka pindi utakapohitaji kwa emergency au suala la kibiashara.

Kama nilivyoelezea mwanzo Kutokana na aina ya biashara Marehemu aliyokuwa anafanya hakuna cha ajabu kuwa na pesa hiyo karibu. Tatizo letu Watanzania wengi tumezoea kukremu na kucopy mpaka kwenye maisha yetu ya kila siku...wakati system yetu hapa nchini haijafikia huko. Biashara ya madini sio Kama biashara ya kuuza nguo Kariakoo.
Mimi najaribu kuwasaidia ili muelewe kabla ya kuanza kujudge ulimbukeni wa Marehemu.

Ukivamia kwa muuza uga ama madini mda wowote lazima ukute mzgo wakutosha ndani
 
wingu la sintofahamu kuhusu kifo cha mfanyabiashara wa madini aliyedaiwa na polisi kujiua mkoani geita (runzewe) baada ya ndugu wa marehemu kukataa kuuzika mwili wa marehemu mpaka uchunguzi(postmortem)ufanyike na hela zinazokadiriwa 300m alizokuwa nazo nyumbani kwake zilichukuliwa na polisi zipatikane,mwili umekutwa na tundu mbili za risasi kichwani na tumboni kitu kinacholeta wacwac kama kweli alijiua..juhudi za rpc wa geita kuwatisha wazike zimeshindikana na marehemu amekwamia geita hospital

kujipiga risasi tatu ni kitu ambacho hakiwezekani,kama kweli angekuwa ni shujaa/mwanaume wa kweli basi zingekuwa tundu mbili,labda kama alianza tumboni na kwa haraka sana akajipiga na kichwani(hii ni kama kweli alikuwa mwanaume wa shoka japokuwa ni kitu ambacho hakiwezekani)
risasi ya kichwa unakata network mara moja,huwezi rudia ya pili,labda kama kuna mtu alimwambia ampige ya pili,otherwise kwa mtu mwenye uelewa na silaha za aina hii haiingii akilini kabisa.r.i.p
 
Polisi wana kazi kubwa ya kujisafisha na hili. Kwa mtiririko wa posts hapa jamvini....ngoma bado imewaelemea polisi...
 
Ukivamia kwa muuza uga ama madini mda wowote lazima ukute mzgo wakutosha ndani
Sio lazima iwe hivyo mkuu. Kuna watu wanajua jinsi ya kuhifadhi hela huwezi hata siku moja kufikiria Kama hizo sehemu mtu anaweza kuweka pesa.

Kwa mfano mimi huwa nikiwa nasafiri na hela huwa nazihifadhi kwenye Emergency Tire ile inayokuwa kwenye mlango wa nyuma kila mtu anaiona,halafu nakuwa na tairi jingine ndani. Nyumbani kwangu bafuni nina heater ya Maji ambayo ilikuwa modified na jamaa pale gerezani kupata storage ya kuwekea emergency money nyumbani. Ukiiangalia hiyo heater huwezi kujua tofauti na heater za kawaida. Pia mara nyingi mdomo ndio huwa unatuponza mkuu. Mtu anaposema anakuwa na hela ndani sio kwamba Mgeni utazikuta sebuleni unywe nazo soda
.
 
huna unachomaanisha zaidi ya upuuzi,300m unaweka chumbsni,aingii akilini
Wengi mnaopinga huyo bwana kuwa na kiasi kikubwa cha pesa hamna exposure na biashara za madini. Sehemu za biashara za madini au mipakani watu mara nying huwa wana deal na cash zaidi kwani biashara huwa zinafanyika on cash basis. Nenda Chunya,Tunduru,Mererani,mipaka ya Tunduma,Namanga Kasumulo nk utayaona haya. Mtu kukulipa mil 50 au mil 100 papo hapo si issue
 
Back
Top Bottom