Ngozi nyeusi tuna matatizo sana!!!mtu anasimama anasema club inaweza kijiendesha kwa kuuza jezi na kutafuta wadhamini?!!hivi kwa nchi hii ambayo asilimia zaidi ya sabini ya wananchi wake wanavaa mitumba second hand,kutoka uko ulaya na Asia ndio wanunue jezi club ijiendeshe?!!! Uyo mshabiki kula yake tu kwa siku matatizo,asilimia kubwa wanaishi chini ya $1.ndio waje waendeshe timu ipate mafanikio?!!tumeua mashirika ya umma karibia yote kwa sababu ya poor management, ndio leo uje useme tutaweza kuendesha vilabu kisasa!!tazama watu wanao jifanya wana uchungu sana na hizo club za kariakoo, ndio utachoka,mzee akilimali, na kilomoni,yaani hawa hata ile sifa ya kuwa tu wakala wa kuuza vocha wa kampuni za simu hawana, ndio utegemee wakupeleke mbele,tazama mwenyekiti wa Yanga ndugu msolwa, na uyu wa Simbasc ndugu nkwabi, tukisimamia ukweli wana weredi gani?!! Ambao unaweza kusema wanaweza kufanya maajabu ya kuzifikisha hizi timu kwenye mafanikio?!!wamewahi kupata mafanikio sekta IPI?!! Walau tuwapime!!! Wapo hapo kwa sababu ya nature ya vilabu hivi wanachama wake wengi ni kama wao tu,watu smart hawawezi kukaa kwenye hivyo vilabu.leo hii uyo nkwambi na msolwa hawawezi kuwa hata ma CEO wa club hata cha mpumalanga hapa South Africa, ndio utegemee wataleta nn kwenye ivyo vilabu.Namsikitikia sana MO atatukanwa ata na wasukuma mikokoteni hata na madereva wa IST,ambao hata uwape mchezaji mmoja tu, kama salamba wamlipe pesa ya usajili na mishahara yake ya mwaka mzima hawawezi, lakini ndio mabingwa wa kutoa matusi,na kejeli!!!hao ndio wanamwita MO tapeli wakati kaka, dada, na ndugu zao wamejaa kwenye viwanda vyake wanapata mkate wao wa kila siku!!Mwafrica kuja kubadilika ni ngumu sana.