brave one
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 4,879
- 7,393
Mwenyekiti wa Simba upande wa wanachama Swedi Mkwabi na mwekezaji Mo Dewji kwa Sasa hawapikiki chungu kimoja na kupelekea sintofahamu ndani ya Simba.
Chanza
Mo Dewji hana Imani na Mkwabi kutokana kuonekana kuwapa nguvu kundi linalompinga likiongozwa na Mzee Kilomoni , Mo anaamini Mkwabi anavujisha Siri za vikao ndani ya Simba kwa kina Mzee Kilomoni kiasi kwamba imekuwa ngumu kupata hati inayoshikilia mzee Kilomoni
Siku chache zilizopita ugomvi ulipamba Moto zaidi baada ya Simba kuingia mkataba na moja ya makampuni ya Mo inayosimamia Dada yake Fetima Dewji kupitia kinywaji Cha Mo Extra. Mwaka Jana Simba iliingia mkataba na kampuni hiyo ya A one kupitia kinywaji Cha Mo Energy wenyw thamani ya milioni 250 na pesa yote ilitangwaza itapelekwa kwenye ujenzi wa uwanja Bunju na mwaka huu mwezi wa pili Simba ilipaswa kuanza mazoezi kwenye uwanja huo kitu ambacho hazijakamilika mpaka sasa.
Mkwabi alilalamika kwa wazee wa Simba kwamba timu imeingia mkataba mpya hata yeye Mwenyekiti upande wa wanachama hajui Wala hajashirikishwa wakati mkataba wa awali pesa haijulikani ilivyotolewa na kutumika (Kama screenshot inavyojieleza). Mkwabi amekuwa akililalamika kumekuwa na mgongano wa maslahi kwenye kubageini Kati ya Mo Dewji Mwenyekiti wa bodi na Mo Dewji mdhamini kupitia kampuni yake ya A one, imekuwa rahisi kwa Mo kupitisha kamapuni yake kwenye udhamini kwa pesa kidogo maana yeye pia ndo Mwenyekiti wa bodi ya Simba.
Mo anaamini Mkwabi anatumia nafasi yake kuwapa nguvu wanaompinga maana wamekuwa wanajua Kila hatua wanaopiga
Mpaka Sasa Mo amesema ameshatumia bilioni 5 na amesema akijitoa hata dai pesa hizo atasemee tu na kuendelea na Mambo yake mengine.