Channel za ndani Azam TV zinalipiwa siku hizi?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Mwishoni mwa mwaka jana, nilimnunulia mama yangu dishi la Azam. Hivi karibuni nimejulishwa kuwa channel zote zimekata, isipokuwa Hope TV na Azam 2. Hakuna channel zingine zo zote zaidi ya hizo, kwa hiyo hata ITV, TBC1, Star TV, n.k, hazipatikani.

Leo nimeagiza fundi aitwe, lakini alipofika, amedai kuwa hakuna channels zitakazoweza kurudi mpaka zilipiwe. Hivi sasa anasubiria nilipie ndiyo aweze kuendelea na utaratibu wa kuzirejesha channel.

Kwa wazoefu, hilo ni sahihi? Mbona nijuavyo channel za ndani huwa ni bure?

Ninemwambia fundi asubirie nifanye kwanza "mawasiliano" ndipo nimpe mwongozo.

Wakuu mnanishaurije?

Mama yupo mkoa wa mbali na ninakoishi kwa sasa.
 
Wazoefu ningali ninasubiria ushauri wenu. Ni lazima nilipie ndiyo channel za ndani zipatikane?
 
Mwishoni mwa mwaka jana, nilimnunulia mama yangu dishi la Azam. Hivi karibuni nimejulishwa kuwa channel zote zimekata, isipokuwa Hope TV na Azam 2. Hakuna channel zingine zo zote zaidi ya hizo, kwa hiyo hata ITV, TBC1, Star TV, n.k, hazipatikani.

Leo nimeagiza fundi aitwe, lakini alipofika, amedai kuwa hakuna channels zitakazoweza kurudi mpaka zilipiwe. Hivi sasa anasubiria nilipie ndiyo aweze kuendelea na utaratibu wa kuzirejesha channel.

Kwa wazoefu, hilo ni sahihi? Mbona nijuavyo channel za ndani huwa ni bure?

Ninemwambia fundi asubirie nifanye kwanza "mawasiliano" ndipo nimpe mwongozo.

Wakuu mnanishaurije?

Mama yupo mkoa wa mbali na ninakoishi kwa sasa.
Chaneli kurudi hazihitaji fundi, ukilipa zinajifungua zenyewe na usimruhusu fundi kufungua kifaa chochote.
Kwa Dar TBC, ITV, Star Tv, na nyingine za kidini huwa zipo tu.
 
Nafikiri ni kote mkuu. Hata huku niliko, channel zote za ndani ni bure. Nimeshangaa kuambiwa eti iliyopo Arusha napaswa kulipia ili channel za ndani zipatikane. Nina mashaka na ufundi wa fundi aliyeniambaia hivyo.
 
Fanya setting ya dish mpaka signals zifike 80% kwenda juu, intensity hata zikifika 70% sio mbaya . Halafu search channels upya utafanikiwa mkuu
Nashukuru mkuu. Kuna dogo nimemwagiza ajaribu kufanya hivyo kama ataweza. Nasubiria mrejesho.

Shukran sana🙏
 
Za bongo ni free kasoro Wasafi na zile zao za Sports HD na One kasoro UTV pia ZBC 2 kuna muda kukiwa na mechi wanaiminya mpaka uwe na kifurushi kikubwa kuanzia 25k

Ila zinginezo nyingi ukilipia kifurushi cha 25k au kile kidogo yake unapata kwa uzuri kabisa
 
Nafikiri ni kote mkuu. Hata huku niliko, channel zote za ndani ni bure. Nimeshangaa kuambiwa eti iliyopo Arusha napaswa kulipia ili channel za ndani zipatikane. Nina mashaka na ufundi wa fundi aliyeniambaia hivyo.
Fundi ni fundi hawezi kuondoka bure, piga au nenda Azam popote ulipo kwenye ofisi zao au wapigie utapata jibu sahihi.
 
Channel za bure ni pamoja na tbc,safari channel,cluods,Itv,Upendo,Tumaini,Arise and shine,Hope channel,Startv,Imaan, sasa kama kwako huoni hata fisi wakikimbizana kwenye safari channel una shida,ila wamenikera tu kuondoa Mbc 1,mbc 2,mbc action,discovery science nk ambazo nilikuwa nalipia ili nizitazame,hasa discovery science.
 
Za bongo ni free kasoro Wasafi na zile zao za Sports HD na One kasoro UTV pia ZBC 2 kuna muda kukiwa na mechi wanaiminya mpaka uwe na kifurushi kikubwa kuanzia 25k

Ila zinginezo nyingi ukilipia kifurushi cha 25k au kile kidogo yake unapata kwa uzuri kabisa
Wasafi ni ya nchi gani?
 
Et hadi Utv wamenikatia mie maisha yashakua magum sasa
 
Back
Top Bottom