kwa ujumla post yenyewe imekaa ki-udini udini...sijaipenda! Unapozungumzia mch.a.lusekelo amefafanua sana, ulitakiwa ueleze alichofafanua ni nini na si kueleza mitazamo yake ya kisiasa na kutaka kuitunza amani kwa kuvunja sheria, binafsi siku zote huwa naamini 'sheria ni haki' so kama wakristo ... Sheria zetu zipo kwenye biblia na tungependa kusikia kutoka kwake biblia inasemaje kuhusu kuchinja na si vinginevyo ... Kazi yake kubwa ni kutufundisha biblia inasemaje kuhusu kuchinja na si kutoa maoni yake binafsi kuhusu amani na kuchinja.
Siamini kama waislamu wanahitaji upendeleo wa kuchinja, la hasa, wanapigania haki yao iliyoandikwa kwenye vitabu vyao vya dini hivyo kusema waachwe wachinje ni kuwadharau huku wengine tukijifanya ni mambumbumbu, je, sheria za dini zenu (ukristo, buddha e.t.c) zinasemaje kuhusu kuchinja? Vipi kuhusu uchinjaji wa kibiashara wa 'mkuu wa meza' nao ubaki kwa waislamu?! Ningefurahi kuona na watu wa dini nyingine wakichangia kwa kushabikia uzi huu na si tu
mwamakula,
mzimu,
mohamedi mtoi
kwa uliyoyaandika, mch.a.lusekelo seem to be bias, myopia, selfish na pengine anawakilisha mawazo yake binafsi .... Tunahitaji kujua vitabu vya dini nyingine vinasemaje that all. Msisahau, 'two wrongs, dont make it right'.